- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hotuba ya Rais Erdoğan ya Umoja wa Mataifa: Maneno Yaso Vitendo
(Imetafsiriwa)
Habari:
Rais Recep Tayyip Erdoğan, katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, alielezea kile kinachotokea Gaza kama “mauaji ya halaiki,” alisisitiza kuwa Israel inaua watoto kila siku, na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua. Akisambaza picha kutoka Gaza, Rais Erdoğan alisema: “Hakuna vita mjini Gaza ... Huu ni uvamizi, uhamishaji, ufukuzaji, mauaji ya halaiki na uharibifu wa maisha.”
Pia alisisitiza maneno yake maarufu, “Dunia ni kubwa kuliko tano,” akikosoa muundo wa Umoja wa Mataifa, alitangaza kuwa mahusiano pamoja na NATO na Marekani yanaimarika, na kwamba Uturuki itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa NATO mwaka 2026. Mambo mengine muhimu ya hotuba yake ni pamoja na msisitizo juu ya mazingira, akili unde, kuzuia uchafu, na familia.
Maoni:
Katika hotuba yake kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, rais Erdoğan aliangazia masuala mengi ya kimataifa, hasa Palestina. Hata hivyo, kwa mtazamo wa Kiislamu, maneno haya yanabakia kuwa matupu, yaliojitenga na vitendo madhubuti, na yalibaki kuwa maneno tu, kamwe yasiyoweza kujikomboa kutokana na vikwazo vya mfumo wa kikoloni wa kilimwengu.
Huenda maneno ya rais Erdoğan yaligusa dhamiri, hasa kuhusu Palestina. Hata hivyo, kwa mtazamo wa Kiislamu, upungufu mkubwa wa hotuba hii ni kwamba maneno makali hayafasiri vitendo halisi. Wakati watoto mjini Gaza wanakufa kwa njaa na ukanda huo umegeuka kuwa kambi ya vifo na uharibifu chini ya kufungiwa kikamilifu, kuwa “sauti ya wanaodhulumiwa” sio chochote zaidi ya maneno.
Ukosoaji wake kwa UN pia ulikuwa wa juu juu. Umoja wa Mataifa unatolewa wito “kujirekebisha” wenyewe ni mfumo ulioanzishwa na wakandamizaji. Wajibu wa Ummah si kuhuisha mfumo huu ulioporomoka bali ni kusimamisha mfumo mpya wa dunia juu ya msingi wa Kiislamu. Maneno ya Erdoğan yanayorudiwa rudiwa kwa muda mrefu, “dunia ni kubwa kuliko tano,” yanaonekana kama ukosoaji wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama watano. Ingawa hii inahusiana vyema na watu wanaochukia mfumo wa kilimwengu, uhalisia ni kwamba Marekani yenyewe haijaridhishwa na mfumo wa baada ya Vita vya Pili vya Dunia iliouunda na inataka kuubadilisha. Kwa hivyo, wito wa Erdoğan wa mageuzi unawiana na maslahi ya Amerika yenyewe.
Zaidi ya hayo, sifa za Rais Erdoğan za kuimarisha mafungamano na NATO zinaashiria udhalilifu, sio heshima, kwa Waislamu. Kushirikiana na shirika ambalo limeua mamilioni ya Waislamu kutoka Afghanistan hadi Iraq, kutoka Syria hadi Libya si jambo la kujivunia bali ni jambo la aibu.
Mazungumzo ya “dola mbili” pia ni zao la fikra ya kikoloni. Katika mazingira ya Palestina na pamoja na Cyprus, msemo huu haumaanishi chochote ila kutambua uwepo wa Mayahudi kwenye ardhi ya Palestina na uwepo wa Wagiriki kwenye kisiwa cha Cyprus. Ilhali wote wawili ni wavamizi. Suluhisho halipo katika kuhalalisha na kutambua vamizi hizi bali katika kuzimaliza.
Ingawa hotuba ya Rais Erdoğan ya Umoja wa Mataifa ilijumuisha maneno ya kuvutia na uchunguzi, haina uzito wowote inapoangaliwa dhidi ya msimamo halisi wa kisiasa wa Uturuki katika kipindi cha miaka miwili iliyopita huku kukiwa na mauaji ya halaiki yanayoendelea Gaza.
Maelezo ya mkutano wa Erdoğan na Trump kufuatia hotuba yake ya Umoja wa Mataifa yanaonyesha jinsi, licha ya nafasi kubwa ya kimkakati ya Uturuki na mienendo ya dola kubwa, nchi imetumbukia katika hali ya hatari. Mikataba mikuu na Marekani—ambayo upeo wake kamili bado haujafichuliwa—imefanywa. Katika ajenda ni ujenzi wa vituo vya nyuklia vya kiraia nchini Uturuki, ununuzi wa mamia ya ndege za abiaria wa Shirika la Ndege la Uturuki kutoka Marekani, ndege za kivita za F-35 na F-16, vifaa vya kijeshi, LNG zitakazosafirishwa na meli za Marekani, na hata ugavi wa baadhi ya madini adimu ya ardhini ya Uturuki kwenda Marekani.
Trump kumkaribisha Rais Erdoğan mlangoni, matumizi yake ya itifaki ya ngazi ya juu, kumvutia kiti chake akae, kukaa naye sako kwa bako, kufanya mkutano wa faragha uliochukua zaidi ya masaa mawili, na kumsifu mara kwa mara hayo sio bila ya sababu. Maneno ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio yanaeleza vyema: “Nchi hizi nyengine zote, ikiwemo Uturuki, zinatuomba tuhusishwe ... Ukweli wa mambo ni kwamba tuna viongozi ... Wanapiga simu na kusema: Je, tunaweza kujumuishwa? Mnaweza kutuingiza? Mnaweza kutupatia dakika tano za kushikana mkono na Rais?”
Wakati viongozi wengi wa dunia wanaomba kushikana mkono kwa dakika tano na Trump, mkutano wa Erdoğan wa masaa mawili unaonyesha makubaliano makubwa yaliyofanywa na Uturuki na dori mapya ambazo inatazamiwa kuchukua katika kutekeleza mipango ya kikanda ya Marekani!
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Remzi Özer