Al-Waqiyah TV: Kwa Mukhtasari “Je, Unamjua Yeye ni Nani?!"
- Imepeperushwa katika Al-Waqiyah TV
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Al-Waqiyah TV: Kwa Mukhtasari “Je, Unamjua Yeye ni Nani?!"
Al-Waqiyah TV: Kwa Mukhtasari “Je, Unamjua Yeye ni Nani?!"
Serikali ya Misri ilitangaza kusherehekea utekelezwaji wa mpango wa Trump mjini Gaza. Sisi alimwalika Rais wa Marekani kusherehekea kwa sababu yeye ndiye mwanzilishi wa mpango wa Gaza: [Rais Trump wa Marekani alisema mnamo Alhamisi kwamba mateka waliosalia wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza wataachiliwa huru mnamo Jumatatu au Jumanne ya wiki ijayo, na kwamba bado analenga kuzuru eneo hilo kusherehekea hafla hii... “Ni muhimu kutaja kuwa Rais Sisi wa Misri alikuwa amemwalika Trump kushiriki katika sherehe ambazo zitafanywa nchini Misri ili kuadhimisha kutiwa saini kwa makubaliano, akiyachukulia kuwa makubaliano ya kihistoria ambayo yanazifisha taji juhudi za Misri, Marekani, na wapatanishi katika kipindi cha hivi karibuni.” (CNN Arabic, 9/10/2025)]
Mnamo Jumapili, 12 Oktoba 2025, Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Tunisia iliandaa kikao cha mazungumzo kwa kichwa “Mradi wa Ukombozi... Katika Mizani ya Hukmu za Sheria ya Kiislamu” katika eneo la Kairouan. Kikao hicho kilihudhuriwa na idadi kubwa ya wakaazi wa eneo hilo.
Al-Waqiyah TV: Lau Wangekuwa Wakweli kwa Mwenyezi Mungu ﷻ... watawala wetu hawangekuwa na kiburi!
Al-Waqiyah TV: Kwa Mukhtasari... Kuwadhibiti Wanaodhulumiwa... Kwa Dhulma Zaidi?!
Mnamo Ijumaa, 10 Oktoba 2025, matembezi makubwa yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, kutoka Msikiti wa Al-Fath kufuatia swala ya Ijumaa. Matembezi hayo yaliandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia kuinusuru Palestina na Al-Aqsa iliyo mateka ambapo ulinganizi ulielekezwa kwa watu wa Tunisia watoe wito wa haraka kwa maafisa na wanajeshi chini ya kichwa, “Nyinyi ndio wenye Uwezo zaidi wa Kulitokomeza Umbile la Kiyahudi!”
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwasilisha kwa wafuasi na wanaozuru kurasa za Afisi Kuu Habari DVD mpya katika lugha tatu yenye kichwa: “Nasheed za Khilafah 1447 H - 2025 M”
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miaka miwili kamili, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo hadi sasa yamesababisha kuuwawa shahidi, kujeruhiwa, na kupoteza zaidi ya wanaume na wanawake wa Kiislamu 240,000, Hizb utTahrir/Wilayah Uturuki, iliandaa matembezi makubwa ya halaiki katika mji mkuu wa Ankara na katika mji wa Istanbul na mji wa Şanlıurfa, yenye kichwa: Wito wa Umoja kutoka Viwanjani kwa ajili ya Gaza katika Mwaka Wake wa Pili: “Wito wa Umoja kwa Watawala: Miaka Miwili Imepita! Hatungojei Maneno, Bali Vitendo!”
Trump alisema katika chapisho kwenye jukwaa lake la Kijamii la Ukweli: “Ninafuraha kuripoti kwamba tuna mazungumzo yenye msukumo na yenye natija na Jumuiya ya Mashariki ya Kati kuhusu Gaza,” na kuongeza kuwa, “mazungumzo makali yamekuwa yakiendelea kwa siku nne, na yataendelea kwa muda mrefu iwezekanavyo ili kupata Makubaliano Yanayokamilishwa kwa Mafanikio.” (Truth Social; TRT Kiarabu, 27/9/2025)
Jana Ijumaa, tarehe 26 Septemba 2025 M / 04 Rabi' al-Akhir 1447 H baada ya swala ya Ijumaa Hizb ut Tahrir / Tanzania iliandaa kampeni ya nchi nzima kukumbusha Majeshi ya Ulimwengu wa Kiislamu, Wanazuoni wa Kiislamu na Ummah kwa jumla juu ya wajibu wao wa kuiokoa Gaza na kutoitelekeza.