Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
| H. 13 Jumada I 1447 | Na: 1447/06 |
| M. Jumanne, 04 Novemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mazoezi ya Phoenix Express 2025
Sura Nyingine katika Sura za Utiifu kwa Utawala wa Marekani
(Imetafsiriwa)
Maandalizi ya Tunisia kuandaa toleo jipya la mazoezi ya kijeshi ya pande nyingi, Phoenix Express 2025, katika mwezi huu wa Novemba yanakuja, na hili ndilo zoezi ambalo Komandi ya Marekani ya Afrika imeanza kuandaa kila mwaka baada ya mamlaka iliyopo sasa nchini Tunisia kuihusisha nchi yetu kwa kutia saini pamoja na Marekani, mnamo tarehe 30/09/2020, makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi, ambayo Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper aliyataja kama ramani ya utendakazi inayoendelea kwa miaka kumi.
Makubaliano haya, ambayo yanawakilisha moja ya hatua za utekelezaji wa kivitendo wa makubaliano yaliyotiwa saini na mamlaka ya Beji Caid Essebsi na ambayo yanatoa nafasi ya kukubali hadhi ya Tunisia kama mshirika wa kimkakati wa Amerika nje ya muungano wa NATO, ni kwa ajili ya kuunga mkono sera yake katika kukabiliana na “washindani wetu wa kimkakati China na Urusi” kwa mwenendo wao “mbaya” kulingana na usemi wa Waziri wa Ulinzi wa Marekani.
Katika suala hili, tunakumbusha kwamba sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia tuliweka wazi wakati wa kusaini makubaliano haya hatari kwamba jambo hilo linazidi makubaliano ya kawaida, kwani Amerika inaandaa mradi mkubwa unaohitaji miaka kumi kamili kukamilika, na kwamba ramani ya utendakazi kulingana na dai la Amerika inahusu ufuatiliaji wa mipaka na ulinzi wa bandari, kupambana na itikadi kali, na kukabiliana na Urusi na China, na hii ina maana, kwa ushupavu wote, kupungua kwa ubwana wa Tunisia na kwa hakika ni udhibiti wa moja kwa moja juu ya nchi yetu.
Pia tumetoa wito kwa kila tukio kukomesha uwepo huu wa kijeshi katika ardhi zetu, ambao unampa adui uzoefu wa kivitendo wa umuhimu mkubwa ambao matokeo yake yataakisiwa kwenye uhai, damu, na heshima ya Waislamu. Na tumethibitisha kila wakati utakatifu wa kushirikiana na adui wakati wa vita, haswa baada ya Oktoba 7, 2023, ambapo Amerika ilifichua uadui wake na ushushaji thamani wa damu ya Waislamu kuanzia Gaza na Ukingo wa Magharibi hadi Lebanon, Iran, Yemen na Syria, kwa kweli ilimsaliti baba yake mkuu Qatar na vivyo hivyo Hamas, na kutangaza waziwazi uungaji mkono wake kwa umbile la Kiyahudi katika kila sehemu ya ardhi za Waislamu ambayo mkono wake msaliti unafikia.
Kwa hivyo, sisi, Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia, licha ya kero, kukamatwa, na kesi za kijeshi ambazo wanachama wetu wamekabiliwa nazo kwa sababu ya kusema kwetu neno la haki, tunathibitisha tena wito wetu wa kufutiliwa mbali makubaliano haya maarufu ya kikoloni ambayo kwayo nchi hii na Maghreb nzima zinakusudiwa kuburuzwa na kuwekwa chini ya sera chafu za Marekani, na tunarudia wito wetu kwa watu wenye nguvu na uwezo katika nchi yetu na katika nchi zote za Waislamu kujihadhari na kile ambacho maadui wa Ummah wanapanga dhidi yao na kuwavutia ndani yake, na kwamba wajibu wa Sharia unawataka kunusuru Dini yao na kumfukuza adui anayejificha katika nchi yao na Umma wao, na kuinua neno la Mwenyezi Mungu kwa kuwanusuru wale wanaofanya kazi kutabikisha Shariah Yake na kusimamisha dola Yake – dola ya pili ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, iliyoahidiwa hivi karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
[وَلَيَنْصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ]
“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Al-Hajj:40]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |



