Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 23 Rabi' I 1447 | Na: 1447/01 |
M. Jumatatu, 15 Septemba 2025 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi Salih bin Muhammad al-Shafrah
(Imetafsiriwa)
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Surat Al-Aḥzāb: 23]
Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia inaomboleza mmoja wa Mashababu wake, ndugu Salih bin Muhammad al-Shafrah, aliyefariki mnamo Jumamosi, tarehe ishirini na moja ya Rabi’ al-Awwal 1447 H sawia na 13/09/2025 M. Alikuwa miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika eneo la al-Qayrawān, ambaye alifanya kazi katika safu zake wakati wa zama zenye giza kuu za ukandamizaji na dhulma. Hakika alikuwa ameshikilia imara da‘wah yake, akijitolea katika kuibeba, akilingania Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, mwenye kuiamini ahadi ya Mola wake Mlezi na bishara njema ya Mtume wake Mtukufu (saw), mpaka alipofariki dunia. Hivyo ndivyo tunavyomhisabu, na wala hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amkubali miongoni mwa watu wema, aipandishe daraja yake katika viwango vya juu zaidi, na awatie moyo familia yake, jamaa na wapenzi wake kwa subira, uthabiti, na malipo.
[إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah: 156]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |