Alhamisi, 28 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  20 Jumada II 1447 Na: HTS 1447 / 65
M.  Alhamisi, 11 Disemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Vituo vya Mafuta Vina Thamani Zaidi na Hadhi Kubwa Zaidi kuliko Watu?!
(Imetafsiriwa)

Imeripotiwa katika habari kwamba Vikosi vya Ulinzi vya Wananchi wa Sudan Kusini vilianza kupeleka vikosi vyake kulinda Uwanja wa Mafuta wa Heglig kufuatia makubaliano ya pande tatu kati ya Mwenyekiti wa Baraza la Uhuru la Utawala la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit, na kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), Mohamed Hamdan Dagalo. Mkuu wa Majeshi ya Wananchi wa Sudan Kusini, Paul Nang, alielezea katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ndani ya uwanja wa mafuta wa Heglig kwamba makubaliano hayo yalibainisha kuondolewa kwa jeshi na kuondoka kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka kutoka eneo hilo, na alithibitisha kwamba lengo la makubaliano hayo lilikuwa kuhakikisha kwamba hakuna hujuma yoyote inayotokea kwenye vituo vya mafuta!!

Swali zito linalojitokeza ni: ni kipi kinachostahili makubaliano zaidi kwa ajili ya ulinzi wake, mwanadamu ambaye kwa ajili yake vituo hivi vya mafuta viliasisiwa, au vituo vya mafuta vyenyewe?! Au je, damu ya Muislamu nchini Sudan imekuwa duni kuliko vituo vya mafuta?! Kwa nini basi al-Burhan hakukutana na Hemedti ili kuwalinda raia huko Geneina, El-Fasher, Al-Jazirah, Bara, Kalogi, Babnusa, na maeneo mengine ambayo yalikiukwa na RSF, ambao waliwaua maelfu ya watu wasio na hatia wasio na silaha, walikiuka heshima, na kupora mali maadamu kuna uwezekano wa kukaa na kufikia makubaliano?!

Hakika, Uislamu umemheshimu mwanadamu, yeyote yule. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلاً]

Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.” [Al-Isra’:70]. Na Mwenyezi Mungu akajaalia kuua nafsi bila ya haki miongoni mwa madhambi makubwa. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[مَن قَتَلَ نَفْساً بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعاً]

aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote.” [Al-Ma’idah:32].

Basi vipi ikiwa nafsi hiyo ni nafsi ya Muislamu? Uharamu ni mkali zaidi na utakatifu ni mkubwa zaidi. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِناً مُّتَعَمِّداً فَجَزَآؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِداً فِيهَا وَغَضِبَ اللّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَاباً عَظِيماً]

Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” [An-Nisa’:93].

Na Mtume (saw) amesema: «لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عَلَى اللَّهِ مِنْ قَتْلِ رَجُلٍ مُسْلِمٍ» “Uangamivu wa dunia ni mwepesi zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kumuua Muislamu. Na akasema (swt):

«لَهَدْمُ الْكَعْبَةِ حَجَراً حَجَراً أَهْوَنُ عَلَى اللَّهِ مِنْ قَتْلِ الْمُسْلِمِ» “Kuvunjwa Ka‘bah jiwe kwa jiwe ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kumuua Muislamu.”

Hivyo basi, nafsi iliyoamini siku zote imekuwa ya thamani kuliko kila kitu duniani, haijalishi thamani yake ni kubwa kiasi gani. Lakini chini ya tawala hizi zilizoundwa na wanadamu ambazo ni vibaraka wa mkoloni kafiri Magharibi, damu ya Muislamu imekuwa duni kuliko damu ya shomoro!

Hivyo basi, watu wa Sudan lazima wawe na dola inayofanya damu yao kuwa na thamani zaidi kuliko vituo vya mafuta na mengineyo, na kuwapa maisha yenye staha chini ya utiifu wa Mwenyezi Mungu. Dola hii ndiyo ambayo Uislamu uliiamua kuwa dola: Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo inaregesha hadhi yetu, inahifadhi damu yetu, inalinda heshima yetu, inalinda mali yetu, na inatufanya watumwa wa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu, ili tuweze kuwa miongoni mwa waliofanikiwa katika dunia hii na Akhera.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu