Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 4 Rabi' I 1447 | Na: HTS 1447 / 18 |
M. Jumatano, 27 Agosti 2025 |
Ripoti ya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Wanamtembelea Mkuu wa Chama cha Democratic Unionist mjini Al-Obeid
(Imetafsiriwa)
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, ukiongozwa na Ustadh Al-Nazir Muhammad Hussein - Mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan - akifuatana na Ustadh Issam al-Din Abdul Qadir, walimtembelea Ustadh Khalid Hussein, Mkuu wa Chama cha Democratic Unionist, katika afisi yake katika mji wa Al-Obeid, mnamo Jumanne 3 Rabi’ al-Awwal sawia na tarehe 26 Agosti 2025 M, kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ili kutibua mpango wa kuitenganisha Darfur.
Ustadh Al-Nazir alizungumza kuhusu mpango wa Marekani wa kuisambaratisha Sudan kulingana na ramani ya Jenerali Mstaafu wa Marekani Ralph Peters, akichochewa na mawazo ya afisa wa ujasusi wa Kiyahudi wa Marekani Bernard Lewis, mwanzilishi wa fikra ya “Mipaka ya Damu” - yaani, kukichana kile ambacho tayari kimechanika kwa misingi ya kikabila, kikanda, na kimadhehebu - ambao ni wa muundo ule ule ambao Amerika uliufuata hapo awali katika kuitenganisha Kusini, na sasa inaufuata kuitenganisha Darfur! Miongoni mwa hatua mashuhuri za kisiasa ambazo zimetekelezwa katika suala hili ni tangazo la kuundwa kwa serikali sambamba huko Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini, inayoongozwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan imeweka mpango wa kufichua na kutibua njama hii.
Ustadh Khalid alitoa shukrani zake kwa ziara hiyo, kuthamini kwake programu mahususi za Hizb ut Tahrir, uboreshaji wa fikra zake, na kazi yake ya kuhifadhi umoja wa nchi, akithibitisha kwamba anaunga mkono jitihada hii, na kwamba afisi yake iko wazi kwa kazi yoyote inayotumikia mwelekeo huu.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |