Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 12 Rabi' II 1447 | Na: 1447/16 |
M. Jumamosi, 04 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Misri Imenaswa Kati ya Kiu na Mafuriko!
Gharama ya Miongo Kadhaa ya Uzembe na Mapuuza
(Imetafsiriwa)
Mgogoro wa mafuriko ambayo yalisomba baadhi ya vijiji vya Misri, na kuzamisha nyumba za makumi ya familia, ni sehemu moja tu ya mgogoro mkubwa na hatari zaidi. Mgogoro huu ni uzembe wa serikali juu wa haki za maji za Misri na kupuuza kwake kwa muda mrefu masuala ya wananchi na usimamizi wa rasilimali za nchi kwa ajili ya kulinda usalama wake na maslahi ya wananchi wake. Mgogoro huu haukutokea ghafla. Badala yake, ni matokeo ya mrundikano mtawalia wa sera zilizofeli ambazo zimekausha serikali zana zake za ulinzi wa maji na kufungua mlango kwa Ethiopia kudhibiti njia ya uhai wa Misri na Sudan kupitia Bwawa Kuu la An-Nahdha la Ethiopia.
Sera za ukaidi za Misri zimeiwezesha Ethiopia kumiliki silaha ya kimkakati ambayo haijawahi kushuhudiwa katika historia ya eneo hili: udhibiti wa Mto Blue Nile, ambao unaipatia Misri zaidi ya 80% ya mahitaji yake ya maji. Tangu wakati Bwawa la Kuu la An-Nahdha la Ethiopia lilipotangazwa, Misri ilitabanni mwelekeo tete wa mazungumzo kwa msingi wa kutambua hali halisi ilivyo na kutegemea ahadi za kimataifa, badala ya kuchukua misimamo thabiti inayohifadhi haki zake na kulinda Misri na watu wake.
Baada ya Ethiopia kukamilisha hatua za kujaza bwawa hilo moja baada ya nyingine bila makubaliano ya kisheria, sasa inadhibiti mtiririko wa maji kwenda Misri na Sudan, kufungua na kufunga milango yake kulingana na maslahi yake, au kama baadhi ya maafisa wa Ethiopia wanavyosema, “kulingana na kile Addis Ababa inachoona kinafaa,” au kama inavyoelekezwa na Marekani. Kwa hivyo, bwawa hilo limekuwa silaha ya shinikizo la kisiasa, kiuchumi, na kiusalama ambalo linaweza kuelekezwa dhidi ya Misri wakati wowote Ethiopia na mabwana zake wanapotaka hivyo.
Silaha hii inaweza kutumika katika pande zote mbili. Ya kwanza ni kiu, pindi Ethiopia inapofunga bwawa au kupunguza utoaji wa maji, na kutishia Misri na upungufu mkubwa wa maji ambao utaathiri vibaya kilimo, viwanda na maji ya kunywa. La pili ni mafuriko, wakati kiasi kikubwa cha maji hutolewa kwa muda mfupi, kama ilivyotokea hivi karibuni, kuzamisha vijiji, nyumba zinazoanguka, na kutishia pakubwa Bwawa la High Dam. Udhibiti wa maji ya Nile hauko tena mikononi mwa Misri; imekuwa mateka kwa ushawishi wa nje, kutokana na serikali hii kufuja nguvu zake na kusalimisha kwa hiari haki za maji za Misri.
Kinachofanya athari za mafuriko ya sasa kuwa mabaya zaidi ni kwamba miundombinu ya maji ya Misri, ambayo ilikuwa na uwezo wa kunyonya mafuriko yoyote yanayoweza kutokea, imeharibiwa. Mikondo, mifereji ya maji na mitaro ya maji iliunda mtandao jumuishi wa kimaumbile na ulioundwa kwa ajili ya kutiririsha na kusambaza maji ya ziada, kulinda ardhi ya kilimo na vijiji dhidi ya mafuriko. Walakini, katika miongo kadhaa iliyopita, mitandao hii imepuuzwa sana na, mara nyingi, ilijazwa kwa makusudi.
Ripoti rasmi pia zinaonyesha kuwa makumi ya maelfu ya kesi za uvamizi na uregeaji nyuma wa maji taka zimerekodiwa katika miongo miwili iliyopita. Zaidi ya kesi 18,000 za uvamizi wa Mto Nile zilirekodiwa mwaka 2025 pekee, pamoja na zaidi ya majengo 20,000 haramu yaliyojengwa ndani ya mipaka ya Mto Nile na “ardhi ya mto.” Uvamizi huu haukutokea kwa siri; badala yake, ulitokea chini ya uangalizi wa asasi za serikali, ambazo zilisita kuwaondoa au kuwaruhusu kimya kimya kupitia ufisadi, upendeleo, au uzembe wa kiutawala.
Badala ya kupanua chaneli za mto na kufungua tena vijito vya zamani ili kunyonya mafuriko na kuyatumia kuregesha ardhi mpya, serikali ilichagua njia tofauti: Ilijaza mikondo na mitaro ya maji na kuruhusu wengine kutumia mkondo wa Nile kwa kilimo na ujenzi, na kupunguza uwezo wa mfumo wa maji kunyonya mafuriko yoyote ya ghafla.
Ardhi zilizotengwa hapo awali kwa ajili ya mifereji ya maji zimegeuzwa kuwa makaazi yasiyo rasmi au ardhi ya kilimo isiyo na leseni, na kuwaweka katika hatari wakati wowote kina cha Nile kinapopanda. Bila mipango madhubuti ya tahadhari ya mapema, wakaazi wengi hujikuta wakikabiliana na maji yanayopanda kwa kasi na nyumba zinazoporomoka, bila ulinzi wowote wa kweli kutoka kwa serikali.
Utelekezaji huu sio wa pekee katika utelekezaji mpana wa kilimo cha Misri. Badala ya kuendeleza mifumo ya umwagiliaji, kudumisha mitandao ya mifereji ya maji, na kupanua ardhi ya kilimo ili kuhifadhi usalama wa chakula, serikali imekuwa ikijishughulisha na miradi ya juu juu ambayo haina uhusiano wowote na kufufua ardhi. Kwa kweli, imeruhusu ardhi yenye rutuba kuharibiwa kwa ajili ya miradi ya uwekezaji au makaazi. Misri imepoteza mamilioni ya ekari za ardhi ya kilimo katika miongo ya hivi karibuni, na hivyo kupunguza uwezo wake wa kukabiliana na uhaba wowote wa maji.
Maji ni moja ya mahitaji makubwa ya maisha, na Uislamu unaitaka serikali kuyahifadhi na kuyasimamia vyema. Ni wajibu wa serikali kutumia nguvu na uwezo wake wote kuhifadhi rasilimali za maji na kuwalinda watu kutokana na hatari, iwe mafuriko au ukame. Kukosa kufanya hivyo sio tu kosa la kiutawala; ni khiyana ya amana ambayo Mwenyezi Mungu amemkabidhi mtawala, na adhabu ya kushindwa huko duniani na akhera ni kali.
Uislamu hauruhusu utegemezi au kusalimu amri kwa shinikizo la kigeni. Bali, unahitaji kuchukua misimamo madhubuti ya kisiasa na kijeshi ili kulinda rasilimali za Ummah na kuzuia nchi yoyote kudhibiti uhai wa Waislamu. Kuliacha Bwawa la An-Nahdha la Ethiopia kupanuka hadi liwe “mshipa wa uhai” mikononi mwa Ethiopia ni uzembe mkubwa wa kisiasa unaogongana na wajibu wa mtawala wa kulinda maslahi ya taifa.
Matokeo yake ni kwamba Misri imekuwa hatarini kwa vitisho vya maji kutoka nje, na leo inakabiliwa na mlingano mkali:
• Miundombinu chakavu ya maji kutokana na miongo kadhaa ya kupuuzwa na ufisadi.
• Njia ya Mto Nile imepunguzwa na vijito vyake vimejazwa.
• Vijiji na vitongoji vimejengwa ndani ya mipaka ya mto bila kizuizi chochote.
• Dola ambayo imepoteza uwezo wake kuhusu masuala ya maji na imeukabidhi kwa Ethiopia.
Kuendelea kwa hali hii kutamaanisha tu mafuriko zaidi wakati wa misimu ya kuachiliwa maji, kiu zaidi wakati wa misimu ya kizuiwa maji, na utegemezi zaidi kwa matakwa ya nje ambayo yanadhibiti mto ambao Mwenyezi Mungu amewabariki nao watu wa Misri.
Suluhisho la kweli haliji kupitia mazungumzo rasmi, au kusubiri ruzuku na ahadi za kimataifa kutoka Benki ya Dunia. Badala yake, linakuja kupitia serikali kuchukua kikamilifu majukumu yake halali kwa kujenga upya mfumo wake wa maji katika misingi thabiti, kuachilia huru maamuzi yake ya kisiasa kutoka kwa utegemezi, kwa kutumia njia zote za uwezo wake kulinda haki ya maji ya taifa, kuondoa ufisadi wa kiutawala, kufungua tena mikondo na mitaro ya maji, kukataza ujenzi katika ardhi ya Mto Nile na kudhibiti usimamizi wa maji kwa njia inayoendana na maslahi ya watu wote, sio tu kikundi kidogo. Hili haliwezi kupatikana na serikali unayotekeleza ubepari fisadi. Bali, inahitaji dola ambayo inawajali watu kikweli kwa mujibu wa Uislamu.
Uislamu unaitaka serikali kuwa mlinzi wa maslahi ya taifa, na sio kuwabebesha mzigo wa ushawishi wa kigeni. Inahitaji dola kujenga upya miradi yake kwa msingi wa “ubwan ni kwa Sharia na mamlaka ni kwa Ummah,” sio maagizo ya nchi wafadhili. Hili linaweza tu kufikiwa kupitia mfumo ambao unatawala kikweli kwa mujibu wa Uislamu, unaounganisha upya siasa kwa maadili, na kufanya utunzaji wa mambo ya watu kuwa lengo lake kuu, si kauli mbiu tu ya matumizi ya vyombo vya habari.
Ewe Mwenyezi Mungu, turudishie dola ya Kiislamu, mamlaka yake na sheria yake, ili tufurahie tena kivuli chake; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُواْ وَاتَّقَواْ لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاء وَالأَرْضِ وَلَـكِن كَذَّبُواْ فَأَخَذْنَاهُم بِمَا كَانُواْ يَكْسِبُونَ]
“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.” [Al-A’raf 7:96]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |