Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 2 Dhu al-Qi'dah 1446 | Na: 1446/32 |
M. Jumatano, 30 Aprili 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkondo wa Bahari wa Suez: Mtazamo kwa Kauli za Trump na Msimamo wa Utawala wa Misri
(Imetafsiriwa)
Katika onyesho jengine la kiburi, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kwenye jukwaa la "Ukweli wa Kijamii" kwamba meli za Kimarekani zinapaswa kupita kwenye Mikondo ya Suez na Panama bila malipo, akidai kwamba Marekani "iliunda mikondo yote miwili." Alimteua Waziri wake wa Mambo ya Nje kufuatilia makubaliano ambayo yataasisisha matakwa haya ya kikoloni.
Kauli hii ya uchochezi ilizua wimbi la hasira rasmi na vyombo vya habari nchini Misri. Mwanachama mmoja wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Kitaifa katika Baraza la Wawakilishi aliilaani kauli hiyo akiichukulia kuwa ni ukiukaji wa ubwana wa Misri. Licha ya hasira ya umma, utawala wenyewe ulijibu kwa ukimya, ukionyesha msimamo wake dhaifu mbele ya maagizo ya kimataifa, kujisalimisha na utiifu wake kwa Magharibi ya kikoloni, na kutokuwa na uwezo kamili wa kutetea ubwana, au hata sura ya msingi kabisa ya heshima ya 'kitaifa'.
Mkondo wa Suez ni mshipa muhimu kwa biashara ya kimataifa. Kulingana na data kutoka kwa Mamlaka ya Mkondo wa Suez za 2023, zaidi ya meli 26,000 zilipitia mkondo huo, na kupata mapato ya takriban $ 9.4 bilioni. Inachukua 12% ya kiasi cha biashara ya kimataifa na 30% ya usafirishaji wa makontena ya kimataifa. Hata hivyo pamoja na umuhimu wake mkubwa, udhibiti juu yake unabakia chini ya mfumo wa kimataifa wa kikoloni, ambao ulilazimisha Mkataba wa Konstantinopoli wa 1888, unaowajibisha Misri kuruhusu urambazaji huru kupitia mkondo huo kwa mataifa yote - ikiwemo dola za kikafiri za kiuadui. Hata hivyo, usimamizi na ubwana juu ya mkondo huo unabakia kwa dola ya Misri, ambayo ina haki ya kulazimisha ada za usafiri. Hata hivyo, muundo huu wa kisheria ni zao la mfumo wa kimataifa uliowekwa na dola za kikoloni katika karne ya 19, wakati ambapo Umma wa Kiislamu ulikuwa kwenye mporomoko wa kisiasa na kijeshi.
Kauli ya Trump ni kielelezo cha wazi cha itikadi ya Magharibi kuhusu ardhi za Kiislamu. Wanazitazama rasilimali zetu kama mali ya kawaida kwao wenyewe na wanatuona kama makoloni tegemezi yasiyo na ubwana wa kweli. Wanachukulia uingiliaji wao wa mambo yetu kuwa ni haki halali. Hii ni sehemu ya sera ya zamani ya kikoloni, kama ilivyoelezwa na Lord Cromer aliposema, "Hatukuikalia Misri kwa ajili ya Misri, bali kwa ajili ya maslahi yetu wenyewe." Trump sasa anafufua mantiki hiyo hiyo isiyo na aibu, chini ya tawala tiifu kwa mabwana zao wa Magharibi.
Njia za maji zinazopitia ardhi za Waislamu ni sehemu ya mali ya umma na lazima zisimamiwe kwa mujibu wa hukmu za sheria ya Kiislamu, sio kwa sheria zilizotungwa na binadamu au mikataba ya kikoloni. Katika Uislamu, milango ya bahari na njia za maji zilizomo ndani ya ardhi za Kiislamu zinasimamiwa na hukmu zifuatazo:
1. Ubwana kamili juu yake ni kwa Sharia, hukmu zake, na mamlaka ya Uislamu, inayowakilishwa na Al-Khilafah.
2. Kupitia kwao kunatakiwa kuratibiwa kwa mujibu wa kile ambacho Khilafah inakiona kuwa ni kwa maslahi ya raia wake, sio kwa makubaliano yaliyolazimishwa juu ya Ummah. 3. Kutoza ada za usafiri au kukataza kupitishwa meli kunaruhusiwa kisheria. Ama kwa dola zenye uadui, hasa zile za kikoloni, kupita kwao ni marufuku kabisa.
Mkondo wa Suez ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya ardhi ya Misri, ambayo yenyewe ni sehemu ya ulimwengu wa Kiislamu. Kwa hivyo, haipaswi kusalimishwa, kuwekewa mashirika ya kimataifa, au kulazimishwa upitaji bila masharti bila malipo. Hili haliwezi kupatikana isipokuwa kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo inaunganisha ardhi za Waislamu na kuregesha mamlaka yao juu ya rasilimali zao. Watu wa Misri ngao ya Mwenyezi Mungu Duniani, lazima wafanye kazi kwa bidii na Hizb ut Tahrir kuisimamisha.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surat Al-Anfal:24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |