Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
H. 20 Rabi' I 1447 | Na: H.T.L 1447 / 06 |
M. Ijumaa, 12 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ziara ya Ujumbe wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon kwa Mufti wa Sidon na Wilaya zake
(Imetafsiriwa)
Katika muktadha wa mawasiliano na wanasiasa, wanajamii wa Kiislamu huko Sidon, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Wilayah Lebanon ukiongozwa na Hajj Ali Aslan, Mwanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, Mhandisi Bilal Zaidan, Mwanachama wa Kamati ya Shughuli na Hajj Hassan Nahlas, Mkuu wa Kituo cha Sidon, walimtembelea Mheshimiwa Mufti wa Sidon na wilayah zake, Sheikh Salim Sosan.
Ziara hiyo ilihusu mada kadhaa, ikiwemo jaribio la kubadilisha kitambulisho cha Kiislamu cha mji wa Sidon, suala la wafungwa wa Kiislamu, suala la jinsia, na dini ya Ibrahim.
Katika ziara hiyo, mjadala wa kina ulifanyika kuhusiana na masuala haya, ambapo maoni yalibadilishwa kuhusu athari za mambo haya kwa jamii ya wenyeji ya mji wa Sidon.
Makubaliano yalifikiwa juu ya ulazima wa kuhifadhi kitambulisho cha Kiislamu cha Sidon, kuunga mkono suala la wafungwa wa Kiislamu, na mkazo uliwekwa juu ya umuhimu wa kukabiliana na mipango kama vile jinsia na dini ya Ibrahim, ambayo yanaathiri maadili ya kijamii na familia.
Ziara hii inajiri ndani ya mundo wa juhudi za Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon kuhifadhi maadili ya Kiislamu katika jamii na kuimarisha mawasiliano na watu wa Sidon.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |