Afisi ya Habari
Denmark
H. 23 Muharram 1447 | Na: 02 / 1447 H |
M. Ijumaa, 18 Julai 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kupigwa Marufuku kwa Hizb ut Tahrir? – Kufilisika kwa Demokrasia
(Imetafsiriwa)
Kufuatia kampeni ya uzushi ya kibinafsi dhidi ya mmoja wa wanachama wetu iliyofanywa na vyombo vya habari na wanasiasa—kutokana tu na matamshi na maadili yake ya Kiislamu—pande zote tatu za serikali ya Denmark sasa zimejadidisha wito wao wa kisiasa wa kupiga marufuku Hizb ut Tahrir nchini Denmark. Hii ni mbali na wanasiasa wa mara ya kwanza wa Denmark kucheza “karata ya upigaji marufuku” kutokana na kutapatapa kifikra. Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, kwa nyakati tatu tofauti, amegundua kwamba hakuna msingi wa kikatiba wa upigaji marufuku wa aina hiyo.
Hizb ut Tahrir inajulikana duniani kote kwa kutotumia vurugu, lakini badala yake inafanya kazi kwa njia za kisiasa na kifikra. Ukweli huo haubadilishwi na maamuzi yaliyochochewa kisiasa dhidi ya wanachama wetu kadhaa kwa kulingania kwa uwazi ukombozi wa Palestina. Kinyume chake! Kila mara hamu ya kisiasa ya kutupiga marufuku inapoibuliwa, huleta serikali mtawalia za Denmark karibu na marafiki na washirika wao katika serikali za mateso, ambapo wapinzani wa kisiasa na watu wenye maadili tofauti wanateswa kwa ajili ya imani na kauli zao.
Ni tawala dhalimu kama hizo katika ulimwengu wa Kiislamu ambazo Hizb ut Tahrir inataka kuzipindua ili kusimamisha dola ya Kiislamu na utaratibu wa kijamii—Khilafah—sambamba na imani na historia ya idadi ya Waislamu – tena, katika ardhi za Kiislamu.
Uongo kwamba tunafanya kazi ya kupindua jamii ya Denmark umekanushwa mara nyingi, na makanusho haya yanahitaji juhudi ndogo kuyapata na kuyathibitisha. Ufafanuzi pekee unaowezekana ni kwamba wanasiasa hao, dhidi ya elimu yao bora, kwa makusudi wanachochea chuki na uoga ili kuwakandamiza Waislamu wanaojihusisha na jamii wanaokataa kuipigia magoti mimbari ya kisekula, kupitia njia ya marufuku na kulazimishwa.
Hili linafichua unafiki wa kutisha wa watendaji hao hao wa kisiasa ambao, kwa vizazi vingi, wamewahutubia Waislamu kwamba lazima wavumilie kila namna ya uchokozi na sheria za kibaguzi kwa jina la “uhuru wa kujieleza.” Wakati huo huo, inasisitiza utupu na udhaifu wa kina wa “maadili” ya kisekula ya Magharibi ambayo hayawezi kustahamili kupingwa na maoni na fikra za Kiislamu. Katiba, mgawanyo wa madaraka, na kanuni ya uhuru wa kujieleza vyote vinaonekana kuwa vikwazo visivyoendana na wanasiasa hawa ambao hawana majibu kwa maadili ya Uislamu isipokuwa majaribio ya vitisho.
Kwa njia hii, demokrasia ya kiliberali ya kisekula inatia saini tangazo lake lenyewe la kufilisika. Si nguvu kamili ya mamlaka ya serikali wala propaganda na uwongo wa vyombo vya habari vitakavyoweza kuwashawishi Waislamu kwamba wanapaswa kuachana na maadili yao kwa ajili ya yale yanayokuuzwa na watawala katika Christianborg na chombo cha habari cha Berlingske.
Lakini hilo halipaswi kushangaza. Ni mtu gani mwenye heshima angetamani kushikamana na maadili ambayo yanahalalisha mauaji ya kikabila, uwekaji njaa jumla raia na mauaji ya halaiki?!
Hatutatiishwa na adhabu au kupigwa marufuku – sio na mtu yeyote – na kwa yakini si na wanafiki wasio na thamani, wanaounga mkono mauaji ya halaiki. Kazi yetu inaendelea kwa mafanikio, kwa neema ya Mwenyezi Mungu.
Elias Lamrabet
Mwailishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Denmark
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Denmark |
Address & Website Tel: |