Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 25 Dhu al-Qi'dah 1446 | Na: H 1446 / 45 |
M. Ijumaa, 23 Mei 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maandamano ya Kulaani yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir, Wilayah Bangladesh:
“Palestina, Kashmir, Arakan – Khilafah pekee ndiyo Suluhisho”
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, leo (23/05/2025) baada ya swala ya Ijumua, iliandaa maandamano ya kulaani katika misikiti mbalimbali ya Dhaka na Chittagong dhidi ya wimbi jipya la mashambulizi ya umbile lililolaaniwa la Kiyahudi kuchukua udhibiti wa Ukanda wote wa Gaza.
Wazungumzaji wakielezea hali ya hivi sasa ya Waislamu ni Gaza, walisema: umbile lililolaaniwa la Kiyahudi limepanga kufanya mashambulizi makubwa ili kuchukua udhibiti wa eneo lote la Ukanda wa Gaza na kuwaondoa manusura waliosalia. Wamezindua awamu ya kwanza ya mashambulizi mapya makubwa yanayoitwa ‘Gideon’s Chariots’. Wakaazi wa huko wanaonyesha matarajio yao ya mwisho na wazazi wanaandika majina mikononi mwa watoto wao ili miili yao iliyochanika ijulikane. Kisha, katika muda wa saa 36 tu, Wapalestina wasiopungua 250 waliuawa katika mashambulizi kutoka kwa umbile la Kiyahudi katika Ukanda wa Gaza, na Waislamu wasiopungua 24 wa Palestina, wakiwemo watoto, wamechomwa moto wakiwa hai katika mashambulizi ya anga dhidi ya mahema yaliyohamishwa katika eneo la Al-Mawasi la Khan Yunis. Si hivyo tu, hali ya watoto, ambao wamekuwa wakikabiliwa na mgogoro mkubwa wa chakula kutokana na kuzuiwa kwa misaada kwa muda wa wiki 11 zilizopita, ni mbaya sana kiasi kwamba mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu alionya mnamo Mei 19, 2025, kwamba watoto 14,000 mjini Gaza wanaweza kufa bila msaada katika saa 48 zijazo. Hatimaye, malori matano ya misaada yaliingia Ukanda wa Gaza Jumatatu iliyopita, mawili kati yake yakiwa yamejaa sanda. Mumeshuhudia kwamba licha ya kuenea kwa maandamano na hasira za Umma wa Kiislamu, watawala vibaraka wa ardhi za Kiislamu wanatamani sana kulinda maslahi ya Marekani inayounga mkono umbile haramu la Kiyahudi. Mfano bora zaidi ni kwamba watawala wa Kiarabu hivi karibuni walitia saini mikataba ya mabilioni ya dolari ya silaha na Amerika na kumpa Trump ndege ya kisasa ya burudani. Serikali ya mpito ya Bangladesh inatamani sana kulinda maslahi ya Amerika katika eneo hili kwa kutoa kile kinachoitwa ukanda wa kibinadamu na bandari kwa kampuni ya DP World kwa maslahi ya kieneo ya Wamarekani. Kwa sababu ya sera ya utiifu ya watawala wa Kiislamu, umbile kafiri la kishirikina la Kiyahudi linapata shajaa katika mashambulizi haya ya kinyama dhidi ya Waislamu.
Wazungumzaji pia walisema: kiwango cha kuongezeka uvamizi dhidi ya Waislamu sio tu Palestina bali pia duniani kote. Pia tunashuhudia njama za wakoloni makafiri kuhusiana na Waislamu wa Rohingya. Kuna mipango ya kutoa "njia za kibinadamu" kwa Jeshi korofi la Arakan na linapanga kuwatupa Waislamu wa Rohingya kwenye makucha ya mikono yao, ambayo imekuwa na bado inawaua na kuwafukuza Waislamu wa Rohingya. Tunashuhudia kwamba utawala wa Hindutva wa India umegeuza Kashmir kuwa moja ya magereza makubwa zaidi duniani. Tangu shambulio la Pahalgam huko Kashmir, zaidi ya Waislamu 6,000 wamezuiliwa kwa jina la uthibitisho wa uraia. Wanavunja maelfu ya nyumba na misikiti ya Waislamu katika sehemu mbalimbali za India, na Waislamu wanahamishwa kutoka kwa makaazi yao.
Wazungumzaji pia walisema: ingawa inaweza kuonekana kama udhaifu wa Waislamu kwa mtazamo wa kwanza, ukweli halisi ni kwamba Wakoloni makafiri wanafahamu wazi juu ya mwamko wa Umma wa Kiislamu; kwa hivyo, wana hofu na wanajaribu wawezavyo kuuzuia kwa nguvu zao zote. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema,
«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (Khalifa) ni ngao ambayo watu hupigana nyuma yake na kujikinga kwaye” [Sahih Muslim]. Kwa sababu hii, Umma wa Kiislamu umeungana katika kuwaondoa watawala vibaraka na kusimamisha Khilafah. Kwa sababu dhulma kwa Waislamu duniani kote si jambo geni, Waislamu wamekuwa wakikabiliana nayo tangu kuanguka kwa ngao na mlinzi wao – mfumo wa Khilafah. Wasiwasi na kufazaika kwa Mkoloni Kafiri juu ya kurudi kusikoepukika kwa Khilafah tayari kumetoka kwenye midomo ya uongozi wao. "Waislamu wanataka kuchukua utawala katika nchi mbalimbali ili kutawala chini ya mfumo wa Khilafah ya Kiislamu" - kauli ya hivi majuzi ya mkuu wa kijasusi wa Marekani Tulsi Gabbard imefichua wasiwasi wao kuhusu kuibuka kwa Khilafah katika bara dogo la India, hivyo mshirika wa kikanda wa Marekani - Hindutva India - amekuwa na hamu kubwa ya kuwakandamiza Waislamu wa eneo hili. Na pia inaonekana wazi katika kauli ya muuaji wa halaiki Netanyahu kwamba "hatutakubali kuanzishwa Khilafah yoyote katika fuo za Bahari ya Mediterania".
Hatimaye wazungumzaji waliwahutubia watu, hususan wanasiasa wanyoofu, wasomi na watu wenye nguvu: Mwenyezi Mungu (swt) asema, [كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ] “Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu” [Ali Imran: 110]. Ummah huu bora kamwe hautanyenyekeshwa na makafiri washirikina, na huu ni ukweli uliothibitishwa. Unaelekea kwenye marudio ya Khilafah kwa njia ya Utume; bishara njema hii ilitolewa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) mwenyewe,
«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “...kisha utamalizika utawala wa dhulma, kisha kutakuwepo na Khilafah kwa njia ya Utume” [Hadith: Musnad Ahmad]. Hivyo basi, lazima mujitolee katika kuendeleza mradi wa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surah al-Anfal: 24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |