Jumatatu, 21 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  14 Rabi' II 1447 Na: H 1447 / 014
M.  Jumatatu, 06 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Machozi ya Furaha kwa Maadui wa Mwenyezi Mungu, Kushindwa na Kukata Tamaa kwa Waislamu nchini Cyprus

(Imetafsiriwa)

Aprili iliyopita, Baraza la Mawaziri la Cyprus Kaskazini lilitoa “amri ya kiserikali” ambayo inaruhusu wanafunzi kuvaa hijabu za Kiislamu katika shule za sekondari. Hata hivyo, Muungano wa Walimu wa Sekondari wa Cyprus na Uturuki (KTOEOS), ulianza migomo, ukakataa kufundisha watoto waliofika shuleni wakiwa wamevalia mavazi ya kidini, na hatimaye wakaiomba Mahakama Upeo. Wiki iliyopita (mwisho wa Septemba), Mahakama ya Upeo ya Cyprus Kaskazini ilibatilisha “amri ya kiserikali”, ikiamua kuwa ilikuwa kinyume na katiba. Viongozi wa Muungano huo wa Walimu, ambao waliomba kubatilishwa kwa amri hiyo, walisherehekea kuregea kwa marufuku ya hijabu kama “ushindi kwa usekula” kwa kububujika “machozi ya furaha”. Wakati huo huo serikali imetangaza kuanza mara moja “kufanyia kazi sheria mpya”.

Enyi Waislamu wa Cyprus! Je, kamwe inawezekana kwa bunge la demokrasia la kisekula, ambalo husherehekea pombe, na kuhalalisha mahusiano nje ya ndoa, na kamari, zaidi ya hayo hupigia debe haya kama chanzo cha mapato kwa nchi, kuzingatia ulinzi wa maisha, mali na hadhi ya Waumini kama wajibu wake mkuu? Sheria ya mavazi ya Kiislamu kwa wanawake na wasichana wa Kiislamu ni hukmu isiyopingika iliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (swt)... Tofauti na mapendekezo ya Mahakama ya Upeo na ya wanasiasa wenu, hili si suala la uhuru, la usawa, wala la “kutokuwa na upendeleo”, kwani Waislamu wamefungwa na hukmu za Mwenyezi Mungu pekee.

Vivyo hivyo Mahakama ya Upeo ya mfumo huu wa kisekula wa kidemokrasia ilibatilisha “amri ya kiserikali” ya Baraza la Mawaziri lililoondoa marufuku ya hijabu, kesho itaanzisha marufuku mpya kwa visingizio vyembamba na kucheza na maneno.

Kwa hiyo, badala ya kutarajia Mawaziri wenu kuondoa marufuku ya hijabu kwa binti zenu katika bunge la kidemokrasia, munahitaji kudai kutoka kwao kutawala kwa mujibu wa hukmu za Mwenyezi Mungu (swt). Ili waweze kuwa na uwezo wa kufanya hivyo, munahitaji kuwalingania kufanya kazi ambayo ni muhimu ili kuwa sehemu jumla ya Ummah wote wa Kiislamu na kuungana na nchi zengine za Kiislamu na kukataa ukamilifu wa mifumo, sheria, machaguo na mapendeleo yote yasiyo ya Kiislamu. Ni dola ya Khilafah pekee ndiyo itakayoziunganisha nyoyo, mali na majeshi ya Waislamu duniani kote juu ya Qur’an na kwa mujibu wa njia ya Rasulallah (saw), hivyo kukukingeni na mashambulizi yoyote, udhalilifu na ukandamizaji kutoka kwa makafiri! Na itafanya hivyo mara moja, bila masharti, bila kusita kwa kuhamasisha kila njia iliyopo.

Enyi Waislamu kote Ulimwenguni! Msiwaache ndugu na dada zenu Waislamu nchini Cyprus peke yao! Ili kuzuia makafiri wasirudie tena jinai zao dhidi yao, ili kuizuia isiwe Gaza ya pili... jikingeni kwa Mwenyezi Mungu (swt) na katika hukmu zake! Na linganieni dola, ambayo haitumii wakoloni wa Magharibi kama mlingoti wake mkuu bali ni uchaMungu (taqwa), na ambayo uwepo wake ni muhimu mno kwa uwepo wenu. Linganieni Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume! Hapo inakusubirini ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume (saw) ya kukukomboeni, kuikomboa Cyprus, na kuikomboa Palestina!

[وَعَدَ اللّٰهُ الَّذ۪ينَ اٰمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْاَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذ۪ينَ مِنْ قَبْلِهِمْۖ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ د۪ينَهُمُ الَّذِي ارْتَضٰى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ اَمْنًاۜ يَعْبُدُونَن۪ي لَا يُشْرِكُونَ ب۪ي شَيْـًٔاۜ وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذٰلِكَ فَاُو۬لٰٓئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur 55]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu