Jumanne, 09 Dhu al-Hijjah 1447 | 2026/05/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Pakistan yenye Nyuklia Ni Sehemu Isiyofutika ya Ummah wa Kiislamu, Yenye Uwezo wa Matokeo Katika Kiwango cha Kimataifa, Baada ya Kusimamishwa Khilafah Rashida

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kitengo cha vyombo vya habari cha vikosi vya jeshi vya Pakistan, Inter-Services Public Relations (ISPR), kilitoa taarifa kwa vyombo vya habari mnamo tarehe 17 Mei 2026, kikijibu kuwepo tishio kutoka kwa kamanda wa jeshi la Mabaniani, ambalo lilisema, “COAS ya India ilitoa taarifa ya uchochezi wakati wa mahojiano ya hivi karibuni kwamba ‘Pakistan inapaswa kuamua kama inataka kuwa sehemu ya jiografia na historia’... Kinyume na mfumo wa imani ya kirongo na ya kindoto na licha ya matamanio mabaya yaliyopo kila mahali nchini India inayoongozwa na Hindutva, Pakistan tayari ni nchi yenye matokeo katika ngazi ya kimataifa, dola ya nyuklia iliyotangazwa na sehemu isiyofutika ya jiografia na historia ya Asia Kusini.” (Chanzo: ISPR)

Maoni:

Maono finyo ya kitaifa na kikanda ya uongozi nchini Pakistan bado yanawanyima Waislamu wa Pakistan uwezo wao kamili. Uongozi huo unachukulia matokeo katika ngazi ya kimataifa kuwa tarishi wa Trump, anapojitahidi kuepuka matope ya mgogoro na Iran. Zaidi ya hayo, ingawa Pakistan ni sehemu ya jiografia na historia ya Asia Kusini, ina uzito mkubwa zaidi, kama sehemu isiyofutika ya Umma wa Kiislamu wa bilioni mbili, unaodhibiti njia muhimu zaidi za nishati duniani, pamoja na kumiliki sehemu yake kubwa ya rasilimali za nishati.

Huku uongozi wa sasa ukibaki madarakani, Pakistan itaendelea kuwa mwathirika wa njama za Dola ya Kibaniani, iwe ni vitisho vinavyoendelea kwa usambazaji wa maji au kuchochea migogoro kati ya Waislamu, iwe ndani ya Baluchistan au na Afghanistan. Kuhusu bwana wa utawala huo, Trump, yuko bize katika kujenga Mashariki yake Mpya ya Kati, ambapo mrithi wake Magharibi, umbile la Kiyahudi, na mrithi wake Mashariki, Dola ya Kibaniani, watawatawala Waislamu. Ama kuhusu Waislamu, dori yao katika Mashariki ya Kati Mpya ya Trump ni kupigana wao kwa wao chini ya mabango ya kupambana na ugaidi na utengano. Haya ni matunda uchungu ya moja kwa moja ya uongozi ambao hauoni zaidi ya utaifa na ukanda.

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Mko kimya vipi mbele ya utaifa wa uongozi wa Pakistan? Utaifa ni fahari ovu na ubaguzi wa rangi unaoangamiza, ambao Dini yenu tukufu imeuharamisha. Mtume (saw) amesema, «إِذَا الرَّجُلُ تَعَزَّى بِعَزَاءِ الْجَاهِلِيَّةِ فَأَعِضُّوهُ بِهَنِ أَبِيهِ وَلَا تَكْنُوا» “Anayelingania fahari ya kijahiliya, ni kana kwamba ameuma sehemu za siri za baba yake, na msione aibu kusema hivi.” Mtume (saw) amesema kuhusu upotovu wa ujinga (جاهلية jahilliyah), «دَعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ» “Uwacheni kwani huo ni uvundo. Imepokewa katika Sahih Muslim kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«وَمَنْ قَاتَلَ تَحْتَ رَايَةٍ عِمِّيَّةٍ يَغْضَبُ لِعَصَبَةٍ أَوْ يَدْعُو إِلَى عَصَبَةٍ أَوْ يَنْصُرُ عَصَبَةً فَقُتِلَ فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ» “Mwenye kupigana chini ya bendera ya upofu, akaghadhibika na kabila lake, au akalingania kabila, au akaunga mkono kabila, kisha akauawa kwa sababu hiyo, basi atakufa kifo cha kijahiliya.

Pindi dola za kikafiri zilipoeneza utaifa miongoni mwa Waislamu, zilivunja umoja wa Waislamu kuwa watu na rangi tofauti. Pindi utaifa wa Kituruki, Kiarabu, Kikurdi na Kifursi ulipochochewa miongoni mwa Waislamu, safu za Umma wa Kiislamu ziligawanyika. Hii ilisababisha mgawanyiko wa Waislamu, kuvunjika kwa dola yao moja, na eneo lao moja kutenganishwa na jengine. Hatari yake ilikuwa maangamivu kwa Umma wa Kiislamu na kwa dola ya Kiislamu, na athari zake mbaya zinabaki nasi hadi sasa.

Enyi Waislamu wa Pakistan, kwa kweli, tumedhoofishwa na uongozi wa kitaifa, wakati Pakistan ina uwezo wa kusimamisha Khilafah Rashida imara ambayo itaunganisha haraka Ulimwengu wa Kiislamu kama dola moja yenye nguvu. Tunatamani hukmu kwa yale yote  aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt), kama vile Waislamu kutoka Indonesia hadi Morocco wanavyotamani. Swali pekee ni, ni nani miongoni mwa Waislamu atakuwa wa kwanza kujitahidi, kujitolea mhanga na kustahili nasr ya Mwenyezi Mungu (swt).

Enyi Waislamu wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan!

Je, ruwaza ya Trump na vibaraka wake katika uongozi wenu wa kijeshi ni ipi, akiwemo mkuu wake wa kijeshi anayempenda, Asim Munir, kwenu? Ni vita vya kudumu vya Waislamu, juu ya dhana ya kikoloni ya Mzozo wa Kiwango cha Chini (LIC) kwa majeshi ya Waislamu, ambayo imeundwa kudhoofisha uwezo wetu na kutuzuia kupigana na maadui kutoka miongoni mwa Mayahudi, Mabaniani na makruseda. Watu wa Trump katika uongozi wenu wanajivunia uwezo wao katika diplomasia na mazungumzo linapokuja suala la kuiokoa Amerika kutokana na ghadhabu ya Waislamu wa Iran, lakini hawana maono kama hayo kwa Waislamu wa Afghanistan, ambao hivi karibuni walipigana bega kwa bega na nyinyi dhidi ya Urusi ya Kisovieti. Uongozi wenu wa kitaifa kamwe hautakuongozeni kutoa nusrah (نصرة usaidizi wa kijeshi) kwa ajili ya kusimamishwa Khilafah, kuunganisha Ulimwengu mzima wa Kiislamu, kulazimisha Marekani kurudi nyuma kutoka ardhi zetu na kuikomboa Kashmir na Al-Masjid Al-Aqsa.

Kama hamjaelewa tayari, kila wiki na mwezi unaopita, inazidi kuwa wazi kwenu kwamba munahitaji uongozi mpya, ambao umejengwa juu ya kulinda maslahi ya Uislamu na Ummah wake. Tunahitaji uongozi wa Kiislamu ambao utasuluhisha mizozo miongoni mwa Waislamu, kuwalazimisha maadui kurudi nyuma na kuwaongoza wanadamu wote kwa msingi wa uadilifu na mwongozo wa Uislamu. Uongozi huo ni Hizb ut Tahrir (حزب التحرير Chama cha Ukombozi) ambao hutembea ndani yenu, kati yenu na karibu yenu, ulio rahisi kuufikia, kwa hivyo itikieni, Enyi waja wa Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu