Jumatatu, 21 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kupokea Sifa kutoka kwa Rais Trump wa Marekani, Mkuu wa Ukafiri, ni Aibu na Fedheha!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais Trump wa Marekani alisema kuwa rais Erdoğan anafanya juhudi kubwa kwa ajili ya makubaliano mjini Gaza; “Ni mtu wa ajabu. Kiongozi imara sana. Hamas inamheshimu sana.”

Maoni:

Mara tu baada ya Trump, kiongozi mkuu wa ukafiri kutangaza kwa umma makubaliano ya kusitisha mapigano yenye nukta ishirini, na kuashiria kwamba nchi zote za Kiarabu na Kiislamu zinaunga mkono makubaliano hayo na kwamba ulimwengu unaonyesha nia katika mwelekeo huu, Rais Erdoğan alisema kuwa makubaliano haya ni hatua muhimu kuelekea kupatikana kwa amani ya kudumu.

Kadhalika, Erdoğan, ambaye alimtuma Mkurugenzi wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi (MİT) İbrahim Kalın kwenda Qatar ili kuishawishi Hamas, alisema katika ujumbe wake aliousambaza kwenye akaunti yake ya X baada ya majibu chanya ya Hamas kwamba jibu la Hamas kwa mpango wa kuanzishwa kwa usitishaji vita huko Gaza ni hatua ya nzuri na muhimu katika kufikia amani ya kudumu. Aliendelea kwa kusisitiza kwamba kinachotakiwa kufanywa hivi sasa ni kusitisha mara moja mashambulizi yote ya umbile la Kiyahudi na kuzingatia mpango wa kusitisha mapigano, kuchukua hatua zote bila kuchelewa kufikisha misaada ya kibinadamu Gaza na kuhakikisha amani ya kudumu, na kukomesha mauaji haya ya halaiki na picha hii ya aibu, ambayo inaumiza sana dhamiri ya kimataifa.

Rais Erdoğan pia aliahidi kutumia njia zote kupigania utekelezwaji wa mpango wa “Suluhisho la Dola Mbili”, ambao asili yake ni Marekani na anatazamia kuwa dola wakilishi ya Palestina katika sehemu ndogo ya ardhi ambayo imesalia baada ya asilimia 80 kukaliwa kwa mabavu.

Kauli hizi za Erdoğan ni uthibitisho wa wazi kwamba anazunguka kwenye mzunguko wa kisiasa wa Marekani, anatumikia maslahi yake, na anasaliti kadhia ya Palestina na Hamas. Juhudi zote za Erdoğan ni kuifurahisha na kuiridhisha Amerika, ambayo ameitabanni kama kibla. Shukrani kwa watawala kama hao wanaofanya kazi pamoja na Amerika na Magharibi, umbile vamizi la Kiyahudi limekuwa likiendelea na uvamizi wake na mauaji tangu 1948. Limeharibu kila kitu katika njia yake, chenye uhai au kisicho uhai. Kwa hiyo, kusema, hakuacha jiwe hata moja juu ya jengine, wala kichwa juu ya bega.

Watawala hawa wanatazama tu ukatili na ushenzi huu. Kwa hiyo, je, watawala hawa—ambao wamesalia kimya na kutazama, wanaogeuza izza na heshima ya Ummah kuwa sehemu duni ya mazungumzo tu katika diplomasia, na ambao wanatenda kama ngao ya ulinzi kwa umbile la Kiyahudi—watakomesha uvamizi na uonevu huu?

Umbile la Kiyahudi halikomi kwa sababu halioni nguvu yoyote inayoweza kulizuia, kwa hivyo linaendelea na uvamizi wake na mauaji. Mgawanyiko wa ardhi za Waislamu, utepetevu wa majeshi yenye silaha zote za kiteknolojia, uoga na udhaifu wa watawala ndio msingi mkubwa wa uvamizi huu. Ndiyo maana umbile la Kiyahudi linajua hili vizuri sana: Hadi Waislamu watakapoungana na kukusanyika chini ya mamlaka moja ya kisiasa, litakuwa huru kufanya linavyotaka hivyo linaweza kuua na kufanya mauaji makubwa, na ndiyo maana umbile hili ovu halikomi.

Vivyo hivyo, leo, wakati kila sehemu ya Ummah inamkimbiza kiongozi tofauti, adui anatenda kwa mpango mmoja. Umbile la Kiyahudi linashambulia, linaua, linatekeleza mauaji ya halaiki, lakini Umma hauna kiongozi!

Amerika na dola za kikoloni za Magharibi zinakalia kimabavu ardhi za Ummah, zikipora na kunyonya mali na utajiri wao, Ummah hauna jeshi! Madhalimu wanamwaga damu hakuna kiongozi shupavu wa kisiasa wa kuwahisabu!

Hata hivyo, ni jambo la aibu na fedheha kwamba Erdoğan, ambaye aliwaacha Waislamu wa Gaza peke yao na wanyonge, alipuuza matakwa halali ya Ummah, lakini mara moja akatimiza matakwa ya Amerika, na hakuchukua hatua zozote madhubuti za kukomesha dhulma na uvamizi huko Gaza, alipokea maneno ya sifa kutoka kwa kafiri Trump, ambaye yeye ni mtumishi wake. Walakini, watawala kama hao huchukulia fedheha kama sifa, utukufu na heshima. Kwa hakika, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio hivi majuzi alisema, “Nchi zengine zote, ikiwemo Uturuki, karibu zitusihi tujihusishe na masuala haya. Watu hawa wanaweza kusema wanachotaka, lakini mwisho wa siku, wanakuja Ikulu ya White House wanapotaka kitu kishughulikiwe. Wote wanataka kuzungumza na Trump ili asuluhishe tatizo hilo. Ukweli ni kwamba hata leo tuna mikutano inayoendelea na viongozi hao kivitendo wanaomba wawe sehemu ya mikutano hii. Wanapiga simu, wakisema, ‘Tujumuisheni pia, tupeni dakika tano tu tupeane mikono’”.

[اَلَّذٖينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرٖينَ اَوْلِيَٓاءَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنٖينَۜ اَيَبْتَغُونَ عِنْدَهُمُ الْعِزَّةَ فَاِنَّ الْعِزَّةَ لِلّٰهِ جَمٖيعًا]

“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [Surah An-Nisa:139]

Awe Rais Erdoğan au watawala wengine wa Umma wa Kiislamu, wamezoea kudhalilishwa kila mara na makafiri hawa. Hali hii imekuwa tabia ndani yao. Watawala hawa wamezama kwa kina kirefu zaidi. Kwao, hakuna kikomo tena.

Kwa hiyo, umefika wakati kwa Ummah kuwaondoa watawala kama hao wanafiki.

Ni wakati sasa wa Khilafah kusimamishwa, ambapo Ummah utapata tena izza na heshima.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yılmaz Çelik

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu