- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ulaya Inaendelea Kuunga Mkono Mauaji ya Halaiki mjini Gaza
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mauaji ya halaiki sasa yamekuwa yakiendelea kwa miaka miwili.
Hata hivyo, Muungano wa Ulaya unasalia kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa umbile la Kizayuni, ikiwa na biashara inayofikia thamani euro trilioni 42.
Licha ya kauli mbiu tupu kuhusu kuitambua dola ya Palestina, Ulaya inaendelea kusafirisha silaha kwa umbile hilo la Kizayuni. Habari zilizovuja zilizopatikana na gazeti la Denmark zinafichua kuwa hivi majuzi mwezi wa Agosti, serikali ya Denmark ilituma vifaa vya silaha kwa ndege zilizotumiwa kuua watoto mjini Gaza.
Mahakama ya Upeo ya Uholanzi pia imetoa uamuzi kwamba haitaingilia shehena ya serikali ya Uholanzi ya vipuri vya ndege kwa ajili ya ndege za kivita za F-35 za Wazayuni.
Maoni:
Barakoa ambayo nchi za Magharibi zimetumia kuikoloni dunia – barakoa ya kile kinachoitwa haki za binadamu na dhana kwamba sisi ni wema na wastaarabu huku kila mtu mwengine akiwa ni muovu – imepasuka kabisa.
Nchi za Magharibi zimejitahidi sana kuhifadhi koloni lake la kisasa la walowezi nchini Palestina, kwa sababu zinajua kwamba kuanguka kwake kungeashiria mwisho wa utawala wa Magharibi juu ya ulimwengu wa Kiislamu. Ukaliaji wa kimabavu wa Kizayuni ni alama ya ushindi wa Wamagharibi dhidi ya Uislamu, na iwapo umbile hili haramu litaanguka, itaashiria kwamba ulimwengu wa Kiislamu uko njiani kuelekea kwenye mwamko.
Hili lingeupa ulimwengu wa Kiislamu hali ya kujiamini isiyoelezeka na kuupeleka umma wa Kiislamu mbele kuelekea kwenye ushindi wa mwisho dhidi ya ubeberu wa Magharibi.
Kwa hiyo hakuna gharama ambayo Wamagharibi hawako tayari kulipa ili kuubakisha uvamizi huo wa Kizayuni hai. Wametoa kafara pesa na uaminifu mdogo ambao wanaweza kuwa wamebaki nao ili kulibakisha umbile la Kizayuni lidumu kwa njia ya bandia.
Lakini halitaendelea muda mrefu. Ulimwengu mzima umetambua kwamba nchi za Magharibi si chochote ila ni zimwi, na ulimwengu wa Kiislamu kwa hakika unaanza kuamka na kuinuka dhidi ya tawala khiyana na dhalimu. Maandamano ya Morocco ni mwanzo tu na ishara tosha kwamba Umma huu haujafa, kama Wazayuni wanavyoamini.
Hapana – uko hai, na ni suala la muda tu kabla ya kuregesha heshima ya ulimwengu na kuonyesha kwamba uongozi unawezekana bila ya ujambazi, umwagaji damu, au ukoloni – bali kupitia akili na maadili ya Uislamu.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Taimullah Abu Laban