Jumanne, 18 Safar 1447 | 2025/08/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wamisri Wawili Wapotezwa Kwa Nguvu Baada ya Kuwataka Maafisa wa Usalama Kupinga Mzingiro wa Gaza

(Imetafsiriwa)

Habari:

Vijana wawili wametoweka baada ya video yao kusambaa mitandaoni inayoonyesha wakivamia kituo cha polisi katika makao makuu ya Usalama wa Dola katika kituo cha polisi cha Ma’asara huko Helwan kusini mwa Cairo, ambapo waliwaweka wanausalama kwenye seli ya gereza. Kusudio la hatua hii ilikuwa kupinga utepetevu wa maafisa kwa watu wa Gaza. (MEE)

Maoni:

Katika video hiyo ambayo wanaume hao walikuwa wameisambaza kwenye Telegram, vijana hao wawili walioitwa Mohsen Mustafa (umri wa miaka 27) na binamu yake Ahmed Sherif Ahmed Abdel Wahab (umri wa miaka 23) walivamia kituo cha polisi na kuwafungia askari wa usalama kwenye seli ya gereza. Katika video hiyo, wanaume hao walikuwa wakiwaambia maafisa hao kwamba ikiwa maafisa hao wangeambiwa wawakamate waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa ajili ya ndugu na dada zetu huko Gaza, wangewakamata, wakisema “Wao [watawala] wanakutumieni kwa sababu hamukatai amri. Kamwe hamukatai amri! Hamutumii akili zenu.” Aliendelea na kulaani kwake kwa kusema, “Ndugu na dada zetu wako Gaza, na sisi tunataka kufungua kivuko. (X)

Ushujaa huu, wa kuikabili serikali, moja kwa moja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) ni ushujaa wa kweli kweli! Kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«انْصُرْ أَخَاكَ ظَالِمًا أَوْ مَظْلُومًا» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ هَذَا نَنْصُرُهُ مَظْلُومًا، فَكَيْفَ نَنْصُرُهُ ظَالِمًا؟ قَالَ: «تَأْخُذُ فَوْقَ يَدَيْهِ»‏‏

“Mnusuru ndugu yako, ikiwa ni dhalimu au ni mwenye kudhulumiwa.” Watu wakauliza, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)! Ni sawa kumnusuru akidhulumiwa, lakini tutamnusuru vipi akiwa dhalimu?” Mtume (saw) akasema: “Kwa kumzuia kuwadhulumu wengine.”

Walisimama kwa ajili ya kaka na dada zao, ambao wanadhulumiwa mchana na usiku. Pia walikuwa wamejitahidi kadiri wawezavyo kuwazuia maafisa wa utawala huu kushiriki katika ukandamizaji huo. Waliwahoji na kuwafanya wasikilize kile ambacho kilitakiwa kusemwa, wakitohofia kupata matokeo yoyote kwa matendo yao. Walisimama, wakijua utawala wanaoukabili unajulikana kwa kuwatesa na kuwaua wale wanaotoka nje ya mstari. Lakini hilo halikuwazuia kufanya yote ambayo walijua wangeweza kufanya kwa ajili ya ndugu na dada zetu. Mwenyezi Mungu (swt) azikubali amali zao na awape subira familia zao. Na tunawaombea waupate msimamo huu kuwa ni chanzo cha Nur (mwangaza) siku watakaposimama mashahidi.

Enyi maafisa wanyoofu katika Kinana! Tunajua kwamba wako maafisa waaminifu miongoni mwenu, ambao waliingia katika jeshi au vikosi vya usalama ili kutimiza wajibu wenu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Tunajua kwamba hamtaki kuwa madhalimu! Kwa hivyo chukueni maneno ya Mohsen na Ahmed na mutafakari juu yake! MUNATUMIWA kuendeleza ajenda. Kwao, nyinyi si chochote ila ni chombo, kinachotumiwa na Makafiri na tawala za khiyana za nchi za Kiislamu ili kutekeleza zaidi ajenda ya Wamagharibi! Tumieni akili zenu! Fikirini na jiulizeni, inapofika siku na mashahidi wote wakasimama kutoa ushahidi mbele ya Mwenyezi Mungu A’za Wajal, ni upi msimamo wenu? Mutajibu nini kwa Muumba wenu mukiulizwa mumewafanyia nini kaka na dada zenu, walioko ng'ambo ya pili tu ya mpaka bandia, ambao wanakufa kwa NJAA! Wakati sio tu munaweza kuleta misaada, lakini pia munaweza kuikomboa Gaza na Palestina yote! Simameni dhidi ya tawala hizi, msichukue amri kutoka kwao, bali kutoka kwa yule ambaye atatabikisha hukmu za Mwenyezi Mungu (swt), Khalifa.

Enyi Maafisa Wanyoofu! Semeni imetosha... fanyeni Jihad yenye heshima zaidi na musimame dhidi tawala! Mtume (saw) amesema:

‏«أَفْضَلُ الْجِهَادِ كَلِمَةُ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ»

“Jihad bora ni (kuzungumza) neno la haki mbele ya mtawala jeuri.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Khadijah Hafidh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu