Ijumaa, 03 Muharram 1447 | 2025/06/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ziara ya Usaliti

(Imetafsiriwa)

Habari:

Trump aikumbatia Pakistan: ‘mapenzi ya mbinu’ au ‘duara la ndani’ jipya?

Trump amkaribisha mkuu wa jeshi la Pakistan Asim Munir kwa chakula cha mchana cha White House ambapo haijawahi kushuhudiwa, huku Marekani na Pakistan zikirekebisha mafungano. (https://www.aljazeera.com/)

Maoni:

Katika wakati ambapo ulimwengu wa Kiislamu unavuja damu—kuanzia Gaza hadi Kashmir, hadi barabara za Tehran—ziara ya Jenerali Asim Munir kwa Rais wa Marekani Donald Trump si tu kwamba ni uziwi bali ni usaliti wa kiasi kikubwa. Mkutano huo, uliofanyika katika Ikulu ya White House na uliandaliwa na Trump kama ishara ya kushukuru dori ya Munir katika kutuliza hali iliyokaribia vita na India, inasifiwa na sehemu za utawala wa Pakistan kama hatua ya kimkakati ya kidiplomasia.

Kwa kweli, inaashiria sura nyingine katika urithi wa kudhalilisha wa kipote cha jeshi la Pakistan wanaosujudu mbele ya dola za Magharibi-hata kama dola hizo hizo ndizo zinazoupa silaha na kuulinda utawala wa Kizayuni katika wimbi la hivi karibuni la uvamizi wa kikatili katika Mashariki ya Kati.

Trump kumkaribisha Munir kunakuja kufuatia mashambulizi ya 'Israel' yanayoungwa mkono na Marekani ndani ya Iran, ambayo yamesababisha vifo vya mamia. Badala ya kupinga ushiriki wa Marekani katika umwagaji damu huu, Munir alinyoosha mkono kwa Trump yuleyule ambaye anafadhili na kulipa silaha umbile la Kizayuni, aliidhinisha mashambulizi ya droni katika ardhi za Waislamu, na wakati mmoja aliita Pakistan taifa la "uongo na udanganyifu." Kuwepo kwa jenerali huyo jijini Washington kunaonyesha ni kwa kiwango gani uongozi wa Pakistan umekuwa mshiriki katika mfumo wa kimataifa wa utawala wa wakoloni.

Ziara hii inaakisi miongo kadhaa ya sera ambapo viongozi wa kijeshi wa Pakistan wametanguliza kipaumbele kudumisha upendeleo kwa Washington juu ya kusimama na Umma. Trump mwenyewe aliweka wazi kwamba utawala wake unaithamini Pakistan kimsingi kwa uimarishaji wake wa kimkakati dhidi ya Iran na kwa kusaidia kudhibiti mzozo na India - maslahi ambayo yanatumikia utawala wa Marekani, sio Umma wa Kiislamu.

Kinachofanya usaliti huu kuwa mchungu zaidi ni kukatika fungamano kati ya kujitolea na mapenzi ya kina kwa Uislamu miongoni mwa watu wa Pakistan na matendo ya uongozi wake. Kuna usaliti wa waziwazi na kupuuza waziwazi wajibu wa kujisalimisha kwa amri za Mwenyezi Mungu, kuwachukulia maadui wa Ummah kama maadui, kutetea ardhi za Waislamu, na kulipizia kisasi mashahidi wao. Wajibu huo, hapa, umeachwa bila aibu.

Kwa Waislamu wa Pakistan na kwa upanuzi wao ndani ya jamii yetu: tunawakumbusha kwamba uongozi wa kweli haupigi magoti mbele ya maadui wa Uislamu, wala hauketi kimya huku Palestina na Kashmir zikiungua, na sasa Iran inavuja damu. Njia ya kusonga mbele iko katika kujitoa kamilifu kisiasa na kifikra kutoka kwa maagizo ya Amerika. Ni kwa kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume pekee ndipo nguvu za kijeshi za Pakistan zinaweza kutumika kukomboa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, kulinda matukufu, na kuregesha uadilifu kwa Umma. Hadi wakati huo, kila makubaliano na mhalifu wa kivita kama Trump yatabaki kuwa ukumbusho mchungu wa jinsi uongozi wa Pakistan umepotoka kutoka kwa wajibu wake wa Kiislamu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاء بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [5:51]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Haitham Ibn Thbait
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu