Jumanne, 20 Shawwal 1447 | 2026/04/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Amali kwa Mnasaba wa Idd ul-Fitr Iliyobarikiwa 1447 H

Katika siku ya tatu ya Idd al-Fitr Iliyobarikiwa, sawia na Jumamosi, 12 Machi 2026 M, mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan walikusanyika katika afisi ya hizb katikati mwa jiji la Khartoum ili kupeana salamu za Idd. Mkutano huo ulijumuisha mashababu kutoka kote Khartoum, Omdurman, Jabal Awliya, Kalakila, Nile Mashariki, na maeneo mengine. Walitoa pongezi zao kwa Idd iliyobarikiwa na kuelezea furaha yao ya kuonana baada ya miaka mingi ya vita. Msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir nchini Sudan, Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), alihutubia umati mkubwa. Alianza kwa kuwaombea waliouwawa miongoni mwa wabebaji Da'wah, kisha akatuma pongezi zake kwa Amir wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Rashta, na mashababu wa hizb duniani kote, hadhira iliyokuwepo, na Waislamu wote kwa Idd hii ya furaha.

Kisha akazungumzia kuhusu mpango wa kihalifu wa Amerika wa kuigawanya Darfur, akisema kwamba ulikuwa ukifuata hali ya Libya nchini Sudan, pamoja na kuwepo kwa serikal mbili. Alisisitiza umuhimu wa kukwamisha mpango huu.

Msemaji pia alizungumzia kuhusu mageuko ambayo dunia inapitia leo, udhibiti wa Amerika na umbile la Kizayuni, na kiwango halisi cha nguvu zao katika vita dhidi ya Gaza na Iran. Alieleza kwamba nguvu hii kubwa haikuwezi kuvunja ari ya kundi dogo la Waislamu huko Gaza isipokuwa kupitia usaliti wa watawala katika nchi za Kiislamu, na vivyo hivyo kwa vita vya sasa dhidi ya Iran.

Abu Khalil alisema kwamba haya yote ni habari njema kwa Umma wa Kiislamu, ikionyesha kwamba Amerika ni dhaifu kuliko simbamarara wa karatasi, na kwamba Umma sasa unatamani umoja unaotegemea Uislamu na kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hotuba ya msemaji ilishangiliwa na miito ya “Allahu Akbar” kutoka kwa mashababu na kauli mbiu zinazotoa wito wa kuregea kwa Khilafah.

Kwa upande mwingine, baadhi ya mashababu walitoa hotuba fupi, wakiwasilisha salamu zao za Idd na pongezi kwa mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Rashta, amiri wa Hizb ut Tahrir, na kwa kaka na dada zao wanaobeba dawah ya Uislamu kote ulimwenguni.

Pia katika hafla ya Idd al-Fitr, mashababu wa Hizb ut Tahrir mjini Port Sudan walipeana salamu na pongezi siku ya tatu ya Idd al-Fitr katika afisi ya hizb katika kitongoji cha Al-Azma cha Port Sudan.

Ustadh Adel Ibrahim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alihutubia waliohudhuria, akiwapongeza wabebaji dawah na kuwatakia Idd njema. Kisha akazungumzia haja ya wanadamu kwa hukmu za Uislamu, akiwahimiza mashababu kujitahidi kadri wawezavyo katika kusambaza ujumbe huo kupitia utafiti, usambazaji, na uenezaji.

Ustadh Dawood Abdullah, pia mwanachama wa Hizb ut Tahrir, kisha akazungumza, akiorodhesha udhibiti unaotolewa na mkoloni kafiri juu ya nyanja zote za maisha katika nchi za Kiislamu na udhibiti wao juu ya sera za ndani na nje za vidola hivi. Udhibiti huu, alielezea, ni matokeo ya kutokuwepo kwa hukmu za Kiislamu kutoka kwa maisha yetu, kutokana na utiifu wa watawala wa Waislamu kwa matakwa ya mkoloni kafiri.

Pia kulikuwa na michangio ya busara kutoka kwa mashababu, na kuifanya siku hiyo kuwa siku iliyojaa kalima zinazoelezea hamu waliyonayo mashababu kwa ustawi wa Ummah.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan
Jumamosi, 03 Shawwal 1447 H – 21 Machi 2026 M

Kalima ya Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Kwa Mnasaba wa Idd ul-Fitr Al-Mubarak

Katika Afisi ya Hizb ut Tahrir Khartoum

Jumamosi, Siku ya Tatu ya Idd ul-Fitr 1447 H – 2026 M

Kwa Maelezo zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu