Hizb ut Tahrir / Amerika: Jibu kwa Kongamano la Suluhisho la Dola Mbili!
- Imepeperushwa katika Amerika
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Jibu kwa Kongamano la Suluhisho la Dola Mbili!
Jibu kwa Kongamano la Suluhisho la Dola Mbili!
Palestina ni ardhi ya Kiislamu; Umar al-Faruq (ra) aliifungua, Salahudin Al-Ayubi akaikomboa, na Khalifa Abdul Hamiid II akailinda. Haiuzwi, na haikubali kugawanyika baina ya watu wake, na aliyeikalia kimabavu, akiwatoa watu wake humo. Suluhisho lake sio dola mbili. Badala yake, utatuzi wake ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Al-Aziz, Al-Jabbar, na kauli yake (swt) ndiyo suluhisho la kweli, “Na wauweni katika vita popote mtakapowakuta, na watoeni popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah: 191].
Hizb ut Tahrir/Denmark iliandaa kikao, mbele ya ubalozi wa Misri katika mji mkuu wa Copenhagen cha kuwanusuru na kuwaombea nusra watu wetu mjini Gaza na Palestina yote inayokaliwa kwa mabavu, kutoka mto wake hadi bahari yake. Ustadh Abdul Rahman Muhammad, mwanachama wa Hizb ut Tahrir nchini Denmark, alitoa kalima kwa waliohudhuria.
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik (ra) kuwa amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): “Hajaamini yule ambaye analala tumbo lake likiwa limeshiba na hali ya kuwa jirani yake ana njaa na yeye anajua.” Basi vipi kuhusu mji wa Gaza ambao watu wake wanakufa njaa, huku pambizoni mwake kuna ardhi zilizo jaa neema na kheri nyingi, chini ya utawala wa watawala walioisaliti, na kula njama dhidi yake pamoja na maadui zake, wakafunga mipaka na kuziba midomo ya wale walioomba msaada na nusra. Hawakuridhika na kuisaliti tu, walizuia nusra yake na wakajitahidi kuizingira, wakiinyima chakula na dawa.
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kimezindua kampeni ya kimataifa kuangazia maafa yanayozidi kuwa mabaya ya kibinadamu yanayowakabili Waislamu wa Sudan. Kampeni hii pia itashughulikia: siasa na ajenda zilizofichwa nyuma ya mzozo huu.
Mgogoro wa kikatili nchini Sudan kati ya Wanajeshi wa Sudan (SAF) wanaoongozwa na mtawala mkuu wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti), ambaye hapo awali alikuwa naibu wa al-Burhan katika Baraza Kuu, sasa umeingia mwaka wake wa tatu, na kusababisha vifo vya maelfu ya raia. Baadhi ya makadirio yanaweka idadi ya waliofariki katika vita hivi vya kipumbavu kufikia 150,000, huku kukiwa na ukatili wa kutisha uliofanywa na pande zote mbili, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kinyama, mateso, ubakaji mkubwa na uhalifu mwingine wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana. Mauaji ya kikabila pia yameripotiwa, huku jamii nzima zikiteketezwa kwa moto na kuangamizwa, na mauaji ya halaiki katika miji mbalimbali, vijiji na kambi za watu waliokimbia makaazi yao.
Unapomteua mtu wa kutekeleza jukumu ambalo asili yake ulikabidhiwa, hii ina maana kwamba ni wajibu wako wa Shariah kumfuatilia na kumhisabu ikiwa ameghafilika, anafanya makosa, au anadhulumu, na kadhalika. Ni jambo la kawaida kwa Ummah kuendelea kuwa macho juu ya mtawala. Haya ni faradhi yake ya Shariah na Shariah yake kwa wakati mmoja. Maana ya faradhi yake ya Shariah ni kuwa Ummah utakuwa ni wenye dhambi ukilipuuza hili. Haki yake Shariah ni kwamba mtawala atatenda dhambi ikiwa atauzuia kutekeleza wajibu wa kuhisabu, ufuatiliaji, na ushauri, na kadhalika.
Hii ni hotuba kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa Waislamu kuhusiana na faradhi ya Shariah ya kuwanusuru Waislamu walio chini ya mamlaka ya dola za kikafiri na makafiri ambao hawajahamia kwenye Nyumba ya Uislamu (Dar ul Islam), iwe kwa kuwazuia utekelezaji wa ibada zao za kidini au kwa kuwadhulumu.
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi 21, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa na kupotezwa kwa zaidi ya wanaume na wanawake 200,000 Waislamu hadi sasa. Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa matembezi makubwa ya halaiki kote nchini Uturuki licha ya serikali ya Uturuki kuyapiga marufuku.
Axios iliripoti kwamba mkutano wa ngazi ya juu ulifanyika jijini Paris kati ya Waziri wa Mambo ya Kimikakati wa ‘Israel’ Ron Dermer na Waziri wa Mambo ya Nje Asaad Al-Shibani, uliopatanishwa na mjumbe maalum wa Marekani nchini Syria, Thomas Barak, mnamo 25/7/2025. Siku chache zilizopita tangu tarehe 12/7/2025 zimeshuhudia kuongezeka kwa machafuko katika Jimbo la Al-Suwayda [Sweida] kusini mwa Syria, ambalo wengi wa wakaazi wake ni Druze. Umbile la Kiyahudi limetangaza kuingilia kati masuala yao sambamba na kuendeleza uvamizi na mashambulizi yake nchini Syria. Lilishambulia pambizoni mwa kasri la rais, na kuishambulia Wizara ya Ulinzi na Majeshi jijini Damascus.