Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 511
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Maadamu serikali itatawala kwa mujibu wa mifumo, nidhamu na sheria zilizorithiwa kutoka kwa wakoloni, uhuru wa kweli utabakia kuwa ndoto. Kwa hakika wale walioko madarakani wanaotawala kwa kufuata mifumo hii ya kikoloni, kimsingi, ni wasaliti wa kweli wa nchi na Ummah, kwani wameshindwa kuisimamia amana waliyopewa na Mwenyezi Mungu (swt), ambayo ni kutabikisha Shariah yote kwa jumla yake.
Enyi majeshi, msichana mdogo Rahaf Ziyad Abu Sweireh (umri wa miaka 4), ambaye anatoka katika kambi ya Nuseirat huko Gaza, Hashem, aliuawa kishahidi baada ya moyo wake kusimama kwa hofu kutokana na ukali wa sauti ya mashambulizi ya mara kwa mara ya umbile nyakuzi la Kiyahudi.
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwasilisha kwa wafuasi wake na wageni wa kurasa za Afisi Kuu ya Habari silsila ya video yenye kichwa, “Kauli za Wanazuoni kuhusu Khilafah” iliyotolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Pakistan.
Filamu ya Hali Halisi “Kutoka Moyoni mwa Gaza!”
Uongozi wa kijeshi na kisiasa, na mirengo yake yote, inategemea uwepo wao kwa dola za kikoloni za Magharibi!
Katikati ya utakaso wa sasa na kuwekwa kando maafisa ambao wanampinga mkuu wa sasa wa jeshi la Pakistan, ilijiri kutajwa kwa Hizb ut Tahrir. Gazeti maarufu la Kiurdu la “Daily Jang,” liliripoti mnamo tarehe 13 Agosti 2024, katika toleo lake kwa jiji la jeshi la Rawalpindi kwamba, “(2011) Brigedia Ali Khan alifikishwa mahakama ya kijeshi kwa kuwa na uhusiano na shirika lenye itikadi kali la Hizb ut Tahrir. Pia alituhumiwa kwa kueneza uasi ndani ya Jeshi la Pakistan.”
Enyi maafisa wa Jeshi la Pakistan! Vibaraka wa Marekani chini ya uongozi wenu ndio waliomuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, rehema na amani zimshukie!