Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 10 Jumada II 1447 | Na: HTS 1447 / 61 |
| M. Jumatatu, 01 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Wakutana na Mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Bahari Nyekundu
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumatatu, 1 Disemba 2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akifuatana na Ustadh Abdullah Ismail, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, walimtembelea Dkt. Imad al-Din Muhammad Hamdallah, mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Bahari Nyekundu, afisini kwake Port Sudan.
Baada ya kutambulishana, mkuu wa ujumbe alielezea kuhusu Hizb ut Tahrir na malengo yake: “Kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ikiliona kama jambo la hatima na faradhi kwa kila Muislamu kufanya kazi kuelekea hilo.” Mwenyekiti alijibu, “Tunawaunga mkono wale wote wanaofanya kazi kwa ajili ya Uislamu,” na akaomba baadhi ya machapisho ya hizb. Ujumbe huo uliahidi kuyatoa na kisha ukampa machapisho yanayohusiana na kampeni ya Hizb ut Tahrir nchini Sudan ya kutibua mpango wa Amerika wa kutenganisha Darfur.
Ujumbe ulimshukuru nahodha kwa mapokezi ya dhati.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb Ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |



