Alhamisi, 14 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  2 Jumada II 1447 Na: HTS 1447 / 58
M.  Jumapili, 23 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wanamgambo ni Tishio la Usalama kwa Umbo la Serikali, na Uwepo Wao ni Ukiukaji wa Sharia
(Imetafsiriwa)

Mapigano ya silaha yalitokea katika mji wa Dongola, mji mkuu wa Jimbo la Kaskazini, jioni ya Ijumaa, 21/11/2025, kati ya vikosi vya jeshi la Sudan na kikundi chenye silaha kinachojulikana kama Awlad Gamri, kaskazini mwa kituo cha usafiri wa miji. Kulingana na kile kilichoripotiwa katika habari, kiongozi wa kikundi hicho, anayeitwa Al-Tom Gamri, alijeruhiwa na kupelekwa hospitalini, na kuna habari za kuuawa kwa mlinzi wake binafsi.

Mapigano haya yalitokea licha ya ukweli kwamba wanamgambo hawa awali walikuwa miongoni mwa makundi yanayopigana pamoja na jeshi la Sudan, na hii inathibitisha hatari ya kutegemea wanamgambo, kwani hakuna dola yenye heshima inayoruhusu kuwepo kwa vikosi vyengine vya kijeshi kando yake, zaidi ya vikosi vyake rasmi vya jeshi. La kusikitisha, Sudan imekuwa nchi ya wanamgambo bora, wanamgambo wa aina mbalimbali na majina tofauti tofauti; kuna wanamgambo wa kikanda, wanamgambo wa ndani, na hata wanamgambo wa kikabila, na wengine ambao ni wa kifamilia, hadi maeneo yote ya Sudan yamekuwa jukwaa la wanamgambo!!

Na machafuko haya ya wanamgambo ni onyo la kusambaratika kwa nchi; kwa sababu wanamgambo walio nje ya mamlaka ya dola wanaweza kuingiliwa kwa urahisi na dola za kikoloni, kama sio zenyewe zilizowaunda na kuwapa silaha, kama ilivyotokea kwa harakati za Darfur, ambazo zilibeba silaha dhidi ya serikali kwa miaka mingi, na baadhi yao sasa wanapigana na jeshi la kawaida, lakini si chini ya bendera yake, badala yake chini ya viongozi tofauti na bendera zao!! Kwa hivyo ni nini kinachowazuia wanamgambo hawa siku moja kugeuka dhidi ya dola kama walivyofanya hapo awali?! Na inatosha kama mfano kile kilichotokea kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka, ambavyo serikali ya Bashir ilivitegemea katika kupigana na waasi, na walipopata nguvu, walielekeza silaha zao dhidi ya jeshi na dhidi ya serikali, wakiisaidia Amerika katika mpango wake wa kuitenga Darfur kutoka kwa mwili wa Sudan.

Ni muhimu kwamba dola isiruhusu kuwepo kwa vikosi vyovyote vya kijeshi nje ya wigo wa vikosi vyake vya jeshi na nje ya mamlaka ya dola, kwa sababu kuwepo kwa wanamgambo hawa nje ya udhibiti wa dola ni tishio kwa umoja wake na onyo la kugawanyika kwa umbo lake. Badala yake, kuwepo kwao ni ukiukaji wa Shariah, kwani katika Uislamu machafuko kama hayo hayaruhusiwi.

Imekuja katika Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah iliyotayarishwa na Hizb ut Tahrir, na ambayo itarudi hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, katika Kifungu cha 66: “Jeshi lote linapaswa kufanywa jeshi moja lililowekwa katika kambi maalum, lakini baadhi ya kambi hizi lazima ziwekwe katika mikoa mbalimbali, na baadhi yake katika maeneo ya kimkakati. Baadhi yake zitafanywa kuwa kambi zinazohama za kudumu ambazo huunda vikosi vya mashambulizi. Kambi hizi zimepangwa katika makundi mengi, ambayo kila moja huitwa jeshi na kupewa nambari, kwa hivyo itasememwa Jeshi la Kwanza, Jeshi la Tatu kwa mfano, au kumepewa jina la mkoa katika mikoa au wilaya katika wilaya.”

Ni lazima tufanye kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo inashikamana na Sharia, na haitaruhusu kuwepo kwa vikosi vyovyote isipokuwa jeshi la dola, ambalo hulinda mipaka na kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb Ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu