Afisi ya Habari	
				
				Wilayah Sudan
			
| H. 6 Jumada I 1447 | Na: HTS 1447 / 46 | 
| M. Jumanne, 28 Oktoba 2025 | 
Mwaliko wa Kuhudhuria na Kushiriki katika Kikao cha Masuala ya Ummah
 (Imetafsiriwa)
Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, tuna furaha kuwaalika ndugu zetu wanahabari, wanasiasa, na wale wenye hamu na masuala ya umma kuhudhuria na kushiriki katika kikao cha kila mwezi cha masuala ya Umma, ambacho mwezi huu kitakuwa kwa kichwa:
El Fasher: Kituo Kilicho na Vurugu Zaidi katika Mzozo wa Kimataifa wa Sudan
Wazungumzaji katika kikao:
1- Ustadh Muhammad Jami’ (Abu Ayman) – Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan
2- Ustadh Ibrahim Mushrif – Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan
3- Afisa wa Kikao: Ust. Dawood Abdullah – Mwanachama wa Hizb ut Tahrir
Wakati: 10 Jumada al-Awwal 1447 H, sawia na 01 Novemba 2025 M saa 13:00 Mchana
Mahali: Afisi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, Port Sudan – Wilaya ya Al-Azma – Mashariki mwa Uga wa Port Sudan
Uwepo wenu ni heshima kwetu, unaakisi kujali kwenu masuala ya Umma wenu.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
 Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
 katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan | Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ | E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com | 
 
			



