Jumatano, 15 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  8 Dhu al-Hijjah 1446 Na: HTS 1446 / 67
M.  Jumatano, 04 Juni 2025

Pongezi kutoka Hizb ut Tahrir/ Wilayah ya Sudan

Kwa Mnasaba wa Idd Al-Adha 1446 H

(Imetafsiriwa)

Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, tunafuraha kuwapongeza watu wetu nchini Sudan na Umma wote wa Kiislamu kwa mnasaba wa Idd Al-Adha. Mwenyezi Mungu airudishe kwetu, tukiwa Ummah ulioungana chini ya bendera ya Al-Uqab, bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Tunakupongezeni, wakati nchi yetu ya Sudan, bado inateseka chini ya janga la vita, ambalo limeingia mwezi wake wa tatu wa mwaka wake wa tatu, licha ya mauaji, ukiukwaji wa utukufu, uporaji wa pesa, uharibifu wa mali, na kuhamishwa kwa salama, hadi watu wengi wa nchi hiyo wamekuwa wakimbizi wasiokubalika katika nchi jirani, au wakimbizi wachochole wa ndani. Droni bado zinaendelea kushambulia vituo muhimu katika miji ya mashariki, magharibi na kaskazini, na mwanadamu katika nchi yetu bado hana thamani, hakuna uangalizi au jukumu, bali wahalifu wakubwa wanashindania mamlaka na mali, hadi magonjwa na maumivu yameikumba nchi, ambayo ya hivi karibuni yalikuwa ni kipindupindu, ambacho kiliua mamia, hata maelfu, kwa kukosekana kwa huduma za afya na maji safi. Mateso yote haya yalitakiwa kuwa kichocheo kwa wale waliokuwa madarakani kuregea kwenye fahamu zao na kutubia kwa Mola wao kwa kutekeleza sheria yake. Lakini badala ya hayo, bado wanaendelea na upofu katika upotofu wao, na kufuata upotofu wa makafiri, kwa kutekeleza usekula na kutenganisha Dini na maisha, mpaka wakaingia nao kwenye shimo la mjusi, ambalo Mtume (saw) alitahadharisha nalo. Imepokewa kutoka kwa Abu Said, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume (saw) amesema: «لَتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ مَنْ قَبْلَكُم شِبْراً بشبْر، وذراعاً بذراع، حتَّى لو سَلَكُوا جُحْر ضَبٍّ لَسَلَكْتُمُوهُ؛ قلنا: يا رسول الله؛ اليهودُ والنَّصارى؟ قال النَّبيُّ ﷺ فَمَن؟» "Mtafuata njia mbaya, za watangulizi wenu, shubiri kwa shubiri, na dhiraa kwa dhiraa, mpaka ikiwa wataingia kwenye shimo la mjusi, nyinyi pia mutaenda humo." Tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mayahudi na Manaswara? Akajibu, "Nani mwingine?" (Maana yake, bila shaka, Mayahudi na Wakristo.) [Imepokewa na Mashekhe wawili]

Je, mateso yataondolewa vipi ikiwa hatuzipi uzito hukmu za Shariah katika sheria zetu na katika mifumo ya maisha yetu?!

Isipokuwa tukijitahidi kwa dhati kwa ajili ya hukmu ya Shariah, kwa kuuleta Uislamu safi kwenye kiti cha utawala, kupitia kusimamisha dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume, tutaendelea kuteseka katika maisha haya magumu hadi tutakaporegea kwa Mola wetu, tukiwa tumeongoka. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ]

“Je! Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki.” [At-Tawbah: 126]

Idd Mubarak.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah of Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu