Alhamisi, 11 Dhu al-Hijjah 1447 | 2026/05/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  5 Dhu al-Hijjah 1447 Na: 1447 / 12
M.  Ijumaa, 22 Mei 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kama Hujui, Hilo Ni Janga;

Lakini Kama Unajua, Basi Janga Ni Kubwa Zaidi!

(Imetafsiriwa)

Wakati wanasiasa wa Iraq na kambi zao wakigombea nyadhifa, matukio yanajitokeza ambayo yanathibitisha tena kwamba nchi hii si tu kwamba haina ubwana, bali pia kwamba maamuzi yake, ardhi, na anga zake vinakiukwa waziwazi na mtu yeyote na kila mtu. Amri za Marekani zinatolewa waziwazi na bila kuficha kuhusu uundaji wa serikali. Uingiliaji kati wa Iran kupitia kamanda wa Kikosi cha Quds cha Iran na ziara zake za mara kwa mara pia ni uko hadharani na haujafichika. Suala jengine lilikuwa ni ufichuzi wa ‘New York Times’ wa kuwepo kwa kambi mbili za kijeshi za umbile la Kiyahudi wakati wa vita vya Marekani dhidi ya Iran: moja katika Jangwa la Al-Nukhaib na nyingine katika jangwa la magharibi.

Sio siri kwamba kuanzisha kambi za kiwango hiki hakuwezi kukamilika kwa muda mfupi; badala yake, ni matokeo ya mipango mirefu na ya kina. Zaidi ya hayo, ugunduzi wake haukuwa matokeo ya juhudi za kijasusi, bali ni suala la bahati. Baada ya ugunduzi wake, hatukuona na kusikia hatua yoyote inayolingana na uzito wa hali hiyo; badala yake, tulishuhudia uhalalishaji, shaka, na majaribio ya kupunguza uzito wa suala hilo!

Hii inaonyesha kwamba Iraq haistahili kuitwa dola, na kwamba makundi na vyama vyote vinavyohusika katika mchakato wa kisiasa havistahili kuitwa wanasiasa. Hawa si chochote zaidi ya wezi mamluki wanaojali maslahi yao na maslahi ya mabwana zao pekee.

Enyi Waislamu, Enyi wana wa Umma bora: Hali imekuwa mbaya, ufisadi umeenea bara na baharini, na mnaishi katika shida. Yote haya ni kutokana na kuipa mgongo kwenu Shariah ya Mwenyezi Mungu, kutokuwepo kwa mamlaka yenu, na kugawanyika kwa dola yenu. Adui yenu amepata nguvu juu yenu, akiwaletea mateso mabaya zaidi kupitia mauaji, uhamishaji, na ukiukaji wa kile kilicho kitakatifu.

Ni wajibu juu ya wana wa Umma ambao mababu zao waliongoza ulimwengu na kutoa mashahidi kueneza nuru na mwongozo kwa wanadamu ili warudi kwenye Dini yao na chanzo cha izza yao kwa kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume—dola ya heshima na ubwana, nuru na mwongozo—ili waweze kuwa warithi bora wa watangulizi bora.

Kwa ajili ya wajibu huu mkubwa na heshima kubwa, Hizb ut Tahrir inakulinganieni. Kuweni answari wa Mwenyezi Mungu kama Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) walivyokuwa, waliosilimu kwa nyoyo na viungo vyao, na kuweka mfano bora wa kutoa, muhanga, na kujitolea, ili mpate kupata furaha katika ulimwengu hhu na akhera na radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu