Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
| H. 10 Jumada II 1447 | Na: 1447 / 06 |
| M. Jumatatu, 01 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Udhalimu wa Watawala Wakandamizaji Unaweza Kukomeshwa Tu Kupitia Mabadiliko Msingi
(Imetafsiriwa)
Tangu Jumamosi iliyopita, mkoa wa Erbil umekuwa ukishuhudia mvutano wa kiusalama kufuatia maandamano ya makabila ya Herki katika wilaya ya Khabat, yakikituhumu Chama cha Kidemokrasia kwa kukaidi ahadi zake za kuwapa viti vitatu bungeni kwa badali ya kabila hilo kuwapa kura zao katika uchaguzi. Maandamano hayo kisha yakageuka kuwa mapigano kati ya makabila ya Herki na vikosi vya usalama, na kusababisha vifo na majeraha. Katika tukio muhimu, kabila hilo lilitangaza uhamasishaji wa jumla huko Erbil, na waandamanaji wakachoma makao makuu ya Chama cha Kidemokrasia cha Kurdistan katika wilaya hiyo leo, Jumatatu.
Kwa fikra hiyo hiyo ya dola ya kipolisi, Chama cha Kidemokrasia kiliamiliana na maandamano ya wakaazi wa kijiji cha Lajan, ambao walidai huduma na fursa za kazi kwa vijana wasio na ajira, wakitangaza kwamba mazingira katika eneo hilo yamechafuliwa kwa sababu ya Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Lanaz kinachomilikiwa na Chama cha Kidemokrasia, na kukituhumu kwa kudhibiti utajiri wa mafuta bila kutoa manufaa yoyote kwa watu wa eneo hilo. Waandamanaji walifungia barabara malori ya usafirishaji mafuta, ambayo yalisababisha mapigano na vikosi vya Zeravani ambavyo Chama cha Kidemokrasia kilivileta ili kukandamiza maandamano hayo.
Maandamano haya yanaonyesha kuzorota kwa hali katika eneo hilo, na hali bado ni tete kwani waandamanaji kadhaa wamekamatwa na wakaazi wa kijiji hicho wameombwa kuhama kwa kisingizio cha kufanya upekuzi wa silaha.
Tukio hili linaloendelea Erbil ni tukio lile lile linalojirudia nchini Iraq na katika ardhi zote za Waislamu. Tangu mamlaka yalipotekwa nyara na dola kupoteza tabia yake ya malezi, wale wanaoshikilia madaraka na utawala wamegeuka kuwa papa wa ufisadi wasiotosheka, mapanga yakining'inia shingoni mwa Ummah, na madaraja ya mipango ya makafiri wa Magharibi katika nchi za Waislamu. Wao ni kama alivyowaeleza Mtume (saw):
«أَلَا إِنَّهُ سَيَكُونُ عَلَيْكُمْ أُمَرَاءُ يَقْضُونَ لِأَنْفُسِهِمْ مَا لَا يَقْضُونَ لَكُمْ، إِنْ عَصَيْتُمُوهُمْ قَتَلُوكُمْ، وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ أَضَلُّوكُمْ»
“Watakuwapo watawala juu yenu ambao watajiruzuku wasiyokuruzukuni. Mkiwaasi wanakuuweni, na mkiwatii wanakupotosheni.”
Udhalilishaji huu, fedheha, na dhulma ambayo Waislamu wanaishi chini yake si kitu chengine ila ni dalili za ugonjwa mmoja: kutokuwepo kwa Khilafah. Hakuna tiba na hakuna marekebisho isipokuwa kwa kurudi kwake; kutia kiraka nguo iliyoraruka hakutasaidia.
Enyi Waislamu: Je, hamjatosheka na kafara mlizotoa kwa miongo kadhaa, mkizunguka katika duara lisilo na matunda bila ufahamu, mkitafuta maisha ya starehe lakini yenye kudhalilisha, huku nyinyi ni taifa ambalo hapo awali lilikuwa likiwaongoza wanadamu kwa nuru na uongofu?
Hizb ut Tahrir inawalingania kwenye kazi nzito na mwelekeo sahihi wa kuregesha izza na heshima yenu kupitia mabadiliko msingi na kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Kwa hivyo kuweni pamoja na wafanyikazi wenye ikhlasi kwa ajili ya faradhi hii kubwa.
[وَاللَّهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ] “Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu.” [Muhammad: 35].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Iraq |
Address & Website Tel: |
E-Mail: hutiraq@yahoo.com |



