Jumatano, 26 Safar 1447 | 2025/08/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  21 Safar 1447 Na: H 1447 / 08
M.  Ijumaa, 15 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Watu! Je, bado mungali na matumaini kwa Watawala na Wanasiasa Watepetevu (Ruwaibidha) wa Sasa?!

(Imetafsiriwa)

Mbio za kuomba-omba mlangoni mwa dola ya kikoloni ya kilimwengu Marekani kati ya matabaka ya kisiasa ya kidemokrasia yenye uchu wa madaraka hazijawahi kutokea.

«إِذَا لَمْ تَسْتَحْيِ فَاصْنَعْ مَا شِئْتَ»

“Ikiwa huna haya, basi fanya chochote unachotaka” (Sahih Bukhari); hadith hii ya Mtume (saw) inaakisiwa katika serikali ya mpito ya sasa na matabaka ya kisiasa ya kidemokrasia, ambayo bila kujali matarajio ya watu, yameonyesha mfano usio na haya katika uchu wa madaraka baina yao na ushindani wa utiiifu kwa mkoloni kafiri Marekani. Watu wamechoshwa na sarakasi hii ya kisiasa na wakati huo huo wana wasiwasi sana. Kwa sababu, watu waliokuwa wameasi sera ya ufisadi-utawala mbaya, utumwa kwa Marekani-Uingereza-India na vita dhidi ya Uislamu vya dhalimu Hasina kwa muda wa miaka kumi na tano na nusu na kuuangusha utawala wa chama kikuu cha kisekula-Awami League katika maasi ya Julai iliyopita, sasa wanashuhudia kurudi kwa siasa hizo hizo. Azimio la Julai ni kudumisha mwendelezo wa mfumo wa kisekula wa kibepari uliofeli ambao umekuwepo kwa watu kwa miongo mingi; na Mkataba wa Julai unaopendekezwa ni kudumisha udhibiti wa Wamarekani kwa kudumisha utatuzi wa kisiasa wa kugawanya madaraka kati ya vyama vya kisiasa na vibaraka. Je, watu wanaweza kuwa na matarajio gani kutoka kwa watawala hawa wasio na haya na matabaka ya kisiasa?

Baada ya kuanguka kwa dhalimu Hasina, watu walitarajia Profesa Yunus achukue hatua madhubuti za kukabiliana na udhibiti wa Marekani-Uingereza-India kwa kutumia ushawishi wake wa kimataifa. Angeweza kuunda mjadala huo na mazingira ya kisiasa nchini humo ambayo kwayo watu wangeweza kuunda suluhisho jipya la kisiasa ili kulinda maslahi ya Uislamu, maslahi ya watu na ubwana wa nchi katika Bangladesh mpya. Ijapokuwa idadi kubwa ya wakaazi wa nchi hii ni Waislamu, serikali ya mpito, kuuondoa Uislamu katika masuluhisho ya kisiasa, haijaondoa marufuku iliyowekwa na dhalimu Hasina kwa chama cha kisiasa cha Hizb ut Tahrir kwa kujisalimisha kwa Marekani-India. Pamoja na hayo, kupitia makongamano ya mtandaoni Hizb ut Tahrir imewasilisha muundo wa dola ya Kiislamu, njia ya kuasisi uchumi unaojitegemea na kuwa na jeshi thabiti kwa ajili ya kulinda ubwana wa nchi hii kwa kuzingatia katiba ya Kiislamu ili kutekeleza matumaini na matarajio ya wananchi wa Bangladesh mpya. Kwa kuongezea, makongamano haya, kama lile lenye mada “Vipi Mapinduzi yanashindwa?”, limeunda mwamko wa kisiasa. Badala ya kukubali mapendekezo haya ya kulinda Uislamu, maslahi ya watu na ubwana wa nchi, serikali ya mpito haijaacha kuwakandamiza watu wanaopenda Uislamu wa nchi hii na Hizb ut Tahrir.

Inawezekana kuwaunganisha watu wa nchi hii kwa misingi ya itikadi ya Kiislamu pekee, hata hivyo chama kimoja cha Kiislamu pamoja na kimojawapo cha vyama vya kisiasa vya kisekula - BNP, vimeiahidi Marekani kukabiliana na kuibuka kwa mfumo wa Kiislamu-Khilafah. Kwa hakika kupitia haya wameungana katika siasa za utumwa wa Wamarekani na kukata uhusiano wao na watu wanaopenda Uislamu wa nchi hii. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitutahadharisha kuhusu watawala na wanasiasa hawa: : «سَيَأْتِي عَلَى النَّاسِ سَنَوَاتٌ خَدَّاعَةٌ، يُصَدَّقُ فِيهَا الْكَاذِبُ، وَيُكَذَّبُ فِيهَا الصَّادِقُ، وَيُؤْتَمَنُ فِيهَا الْخَائِنُ، وَيُخَوَّنُ فِيهَا الْأَمِينُ، وَيَنْطِقُ فِيهَا الرُّوَيْبِضَةُ» قِيلَ: وَمَا الرُّوَيْبِضَةُ؟ قَالَ: «الرَّجُلُ التَّافِهُ يَتَكَلَّمُ فِي أَمْرِ الْعَامَّةِ» “Itawajia watu miaka ya khiyana, muongo atasadikishwa na mkweli atakadhibishwa, khaini ataaminiwa na mwaminifu atafanywa kuwa khaini na Ruwaibidha watatoa maamuzi ya mambo.” Akaulizwa (saw): ‘Ni nani Ruwaibidha?’ Akajibu ﷺ: “Watu watepetevu na wajinga wanaosimamia mambo ya watu” (Hadith: Sunan Ibn Majah). Kwa hiyo, ni wajibu wa wananchi kuachana na watawala na wanasiasa hao wajinga na watepetevu. Wanapenda sana kulinda maslahi ya Wamarekani lakini ni wanazembea sana katika kuchunga mambo ya watu.

Enyi Watu, imetosha! Sasa munapaswa kuwa wachangamfu. Mwenyezi Mungu ﷻ asema,

[إِنَّ اللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ]

“…Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Surah Ar-Ra’d: 11]. Lazima mukatae siasa za utumwa kwa Marekani na kuungana kwa msingi wa Uislamu. Kimbilio lenu la mwisho ni wana wenu waaminifu wanaotumikia jeshi. Lazima mudai wazi wazi kutoka kwao kwamba wakabidhi madaraka kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “…kisha utakuwa mwisho wa utawala wa kidhalimu, kisha itakuweko Khilafah kwa njia ya Utume.” (Hadith: Musnad Ahmad). Vitu viwili viko wazi katika hadith hii; cha kwanza, bishara njema ya kurudi Khilafah kwa njia ya Utume na cha pili, kumalizika kwa utawala wa sasa wa kidhalimu kupitia kusimamisha Khilafah iliyokaribia.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Surah Muhammad: 7].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu