Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 29 Muharram 1447 | Na: H 1447 / 05 |
M. Alhamisi, 24 Julai 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkasa wa Milestone: Watoto Wasio na Hatia na Rubani wetu Jasiri Tauqir, walikuwa Waathiriwa wa Ukatili wa Kukosekana kwa Dola yenye kujali inayowachunga Watu
(Imetafsiriwa)
Jumatatu iliyopita (21 Julai, 2025) alasiri, ndege ya kivita ya Jeshi la Anga la Bangladesh F-7 BGI iligonga jengo katika sehemu ya chini ya Shule ya Milestone na Chuo katika eneo la Uttara katika Mji Mkuu kutokana na hitilafu ya kiufundi. Hii ilisababisha hali ya kusikitisha na ya kuhuzunisha kwa matukio ya kutisha ya watoto walioungua na kukatwa viungo na vijana waliouawa na kujeruhiwa. Sisi katika Hizb ut Tahrir, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) msamaha kwa marehemu hao, na tunawaombea nafuu ya haraka waliojeruhiwa. Na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awajaalie wahasiriwa hadhi ya mashahidi Peponi kwa mujibu wa bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «...وَصَاحِبُ الْحَرِيقِ شَهِيدٌ» “Mwenye kufa katika moto ni shahidi…” (Ahmad, Abu Dawud, An-Nasa’i).
Enyi Watu, kama vile ikhlasi na ushujaa wa watu umedhihirika kupitia tukio hili la kusikitisha, unafiki na kutowajibika kwa watawala na vyama vya kisiasa vya kisekula vyenye ubinafsi pia vimefichuliwa kwa watu. Tumeona ushiriki wa ajabu wa wananchi katika shughuli za uokoaji na kuchangia damu kwa majeruhi, muhanga wa kishujaa ya mwalimu aliyejitolea maisha yake kuokoa wanafunzi wasiopungua 20. Kwa upande mwingine, serikali imeshindwa kutoa misaada na matibabu ya haraka kwa watoto walioungua vibaya, achilia mbali kuwaandalia gari la wagonjwa ili liwapeleke hospitali; ilhali wananchi wameshuhudia kwamba watawala hao na pote la kisiasa wanapougua, wanapelekwa Singapore kwa ndege ya kusafirisha wagonjwa.
Wakati taifa zima linapoomboleza tukio hili la kusikitisha, matakwa ya wanafunzi kuahirisha mtihani wa HSC yamecheleweshwa hadi saa sita usiku kwa kisingizio cha sheria, jambo ambalo limezua hasira kubwa miongoni mwa wazazi na wanafunzi wote. Wanasiasa wa kisekula wenye uchu wa madaraka walikuwa na shughuli nyingi na vipindi vya hotuba-taarifa-picha ili kupata manufaa ya kisiasa na walizua dhoruba katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya mtandao kwa kutafuta nadharia za njama bila kuihisabu serikali. Mikutano ya kugawanya madaraka ya vipote vyenye uchu wa madaraka katika Tume ya Makubaliano ya Kitaifa na ziara za nchi nzima kwa ajili ya kampeni za uchaguzi haijasitishwa. Kwa kweli, suala hili liko wazi mithili ya mchana kote duniani, mfumo wa Ubepari wa kisekula usiojali Mungu ni kiwanda cha kuunda watawala wabinafsi na wapuuzi.
Enyi Watu, suala la kutia wasiwasi ambalo limejitokeza tena kupitia tukio hili ni kusitasita na kuzembea kwa watawala wa kisekula kwa miongo kadhaa kuunda jeshi lenye nguvu lililo na silaha bora. Kwa sababu hiyo, tumepoteza askari jasiri mmoja baada ya mwengine katika ndege zetu za kujitoa uhai, si kwa kukabiliana na adui. Hii si mara ya kwanza kwa ajali hii ya ndege ya kivita kutokea nchini Bangladesh, F-7 hii imehusika katika ajali nyingi katika kipindi cha miaka kumi na moja iliyopita. F-7 iliyotengenezwa na Wachina, ikitoa mfano baada ya Mig-21 ya Urusi, inayoitwa “ndege ya kivita ya babu”, ambayo China iliiunda miaka ya 1960 na kusitisha utengezaji wake mwaka 2013.
Enyi watu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«الْإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ...»
“Mtawala juu ya watu ni mchungaji na anawajibika juu ya raia wake…” (Bukhari na Muslim). Katika historia ya Khilafah tukufu ya Umma wa Kiislamu, hili limedhihirishwa kwa karne nyingi na makhalifa Abu Bakr, Umar (ra) na watawala wengine wasiohesabika wachaMungu. Umar (ra) aliwahakikishia raia jukumu lake, akasema, "لو أن بغلة عثرت على شاطئ الفرات لخشيت أن يسألني الله عنها يوم القيامة" “Iwapo atakufa mwanakondoo aliyepotea kwenye ukingo wa Furaat, naongopa Mwenyezi Mungu ataniuliza kumhusu Siku ya Kiyama.”
Mfumo wa sasa wa kisekula usiojali Mungu, ambao hauwezi hata kuhesabu maiti za watu wake kwa miongo kadhaa, unatukumbusha leo kukosekana kwa dola yenye kujali ya Khilafah ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka mia moja na umuhimu wake. Ukosefu wa uboreshaji wa jeshi katika mfumo wa sasa usiojali Mungu unatwambia jinsi gani ubwana wetu ulivyo hatarini; uhalisia ambao unatukumbusha kukosekana kwa nguvu kubwa ya kijeshi ya Khilafah ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka mia moja na ulazima wake. Amri ya Mwenyezi Mungu (swt) imeilazimisha Dola ya Khilafah kuendelea na juhudi zake za hali ya juu za kufanya kuboresha na kuimarisha jeshi lake. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ اللَّهُ يَعْلَمُهُمْ]
“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua.” [Surah Al-Anfal: 60].
Wito wa Hizb ut Tahrir kwa watu wenye utambuzi wa nchi hii, wanasiasa wanyoofu, wasomi na maafisa wa jeshi, ni kusonga mbele katika kuregesha mfumo huo wa Khilafah wenye kujali na wenye nguvu bila kuchelewa.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |