Jumatatu, 20 Jumada al-awwal 1447 | 2025/11/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  15 Jumada I 1447 Na: H 1447 / 026
M.  Alhamisi, 06 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 Ukumbusho kwa Waislamu kuhusu Utakatifu wa Muislamu: Damu Yake, Mali Yake, na Heshima Yake
(Imetafsiriwa)

Vyombo vya habari vilisambaza habari za uhalifu wa kutisha uliotokea katika mji wa Al-Fashir nchini Sudan, wa mauaji, ubakaji, na uhamishaji uliosababisha maelfu ya familia kuhama.

Na swali linalojitokeza ni: je, inawezaje kuwa rahisi kwa Muislamu anayeshuhudia kwamba hakuna mola wa haki ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na anaamini Siku ya Mwisho—inawezaje kuwa rahisi kwake damu ya ndugu yake Muislamu, mali yake, na heshima yake?! Inawezaje kuwa rahisi kwake kumtisha; na Mtume (saw) amesema:

«لَا يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يُرَوِّعَ مُسْلِمًا»

“Si halali kwa Muislamu kumtisha Muislamu.”

Na kwa hakika jambo kama hilo lilitokea hapo awali katika nchi kadhaa za Waislamu kama vile Syria, Misri, Yemen, Libya, Iraq, na zengine, je, umetoweka kwa Waislamu utakatifu wa damu ya baadhi yao juu ya wengine?!

Hakika, inajulikana kutoka kwa Dini kimsingi uharamu wa kumuua Muislamu kwa makusudi kwa maandiko ya kukatikiwa ya Qur'an. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِناً مُّتَعَمِّداً فَجَزَآؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِداً فِيهَا وَغَضِبَ اللّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَاباً عَظِيماً]

Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” [Surat An-Nisā’:93].

Je, kuna uchungu zaidi kuliko huu katika adhabu ya muuaji wa kukusudia? Na Mtume (saw) asema: «كُلُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ حَرَامٌ؛ دَمُهُ وَمَالُهُ وَعِرْضُهُ» “Kila Muislamu ni haramu kwa Muislamu mwengine: damu yake, mali yake, na heshima yake.”

Na ilikuwa kutoka kwa mambo ya mwisho ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alishauri katika Hotuba ya Kuaga, uharamu wa Muislamu: damu yake, mali yake, na heshima yake kwa Muislamu mwengine. Na maandiko ya Sharia ni mingi katika ufaradhi wa kuhifadhi utakatifu wa Muislamu, na Sharia ilizidisha tishio kali kwa yeyote anayekiuka kitu kati ya matukufu haya.

Mna nini, Enyi Waislamu? Je, inawezekana kwamba Muislamu akiuke utakatifu wa ndugu zake miongoni mwa Waislamu kwa sababu tu anamiliki silaha? Kwa urahisi huo, je, makafiri wakoloni wanaweza kuwadhibiti baadhi ya Waislamu na kuwapa nguvu na silaha na kuwafanya wavunje matakatifu ya ndugu zao miongoni mwa Waislamu? Polisi au askari katika majeshi ya Waislamu anawezaje kuinua silaha dhidi ya wakaazi salama? Je, anafikiri hili linamnufaisha mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kusema kwamba yeye ni mtumishi aliyeamrishwa?

Enyi Waislamu:

Ni lazima mtambue hatari ya jambo hili na ukubwa wake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani muuaji wa Muislamu anastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, anastahili laana Yake, na kufukuzwa Kwake kutoka kwenye rehema Zake, na anastahili milele Motoni. Kwani kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyosema: «لَا يَزَالُ الْعَبْدُ فِي فَسْحَةٍ مِنْ دِينِهِ مَا لَمْ يُصِبْ دَمًا حَرَامًا» “Muumini daima anabakia ndani upeo wa dini yake maadamu hamwagi damu kwa haramu.”

Hivyo madhambi yoyote anayoyafanya pasi na kuua kwa kukusudia, humbakisha ndani ya boma katika dini yake; lakini kwa kuua kwa kukusudia hupoteza nafasi hiyo, hupoteza mafanikio, na hupigwa na hasira ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hakuna udhuru wowote unaomnufaisha—hata kama ndugu yake Muislamu alimkabili kwa silaha. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «إِذَا الْتَقَى الْمُسْلِمَانِ بِسَيْفَيْهِمَا فَالْقَاتِلُ وَالْمَقْتُولُ فِي النَّارِ. قِيلَ: هَذَا الْقَاتِلُ فَمَا بَالُ الْمَقْتُولِ؟ قَالَ: إِنَّهُ كَانَ حَرِيصًا عَلَى قَتْلِ صَاحِبِهِ» “Wanapogombana Waislamu wawili wao kwa wao kwa panga zao, basi muuaji na aliyeuawa watakuwa Motoni. Ikasemwa: “Hii ni kwa muuaji, lakini ni vipi kesi ya aliyeuawa?” Akasema: “Alikuwa na hamu ya kumuua mwenzake.”

Na iwapo muulizaji atauliza afanye nini katika hali kama hiyo, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) anajibu swali hili kuhusiana na kutokea kwa fitna. Imepokewa kutoka kwa Abu Musa al-Ash’ari kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «إِنَّ بَيْنَ يَدَيْ السَّاعَةِ فِتَنًا كَقِطَعِ اللَّيْلِ الْمُظْلِمِ، يُصْبِحُ الرَّجُلُ فِيهَا مُؤْمِنًا وَيُمْسِي كَافِرًا، وَيُمْسِي مُؤْمِنًا وَيُصْبِحُ كَافِرًا، الْقَاعِدُ فِيهَا خَيْرٌ مِنْ الْقَائِمِ، وَالْمَاشِي فِيهَا خَيْرٌ مِنْ السَّاعِي، فَكَسِّرُوا قِسِيَّكُمْ، وَقَطِّعُوا أَوْتَارَكُمْ، وَاضْرِبُوا سُيُوفَكُمْ بِالْحِجَارَةِ، فَإِنْ دُخِلَ - يَعْنِي عَلَى أَحَدٍ مِنْكُمْ - فَلْيَكُنْ كَخَيْرِ ابْنَيْ آدَمَ» “Kabla ya Kiyama kutakuwa na fitna mithili ya usiku wa giza; mtu atakuwa muumini asubuhi na kafiri jioni, au muumini jioni na kafiri asubuhi. Yule aliyekaa wakati huo ni bora kuliko yule aliyesimama; na yule anayetembea ni bora kuliko yule anayekimbia. Kwa hivyo vunjeni pinde zenu, na kateni kamba zenu za upinde, na piga panga zenu kwenye mawe. Na ikiwa mtu atamshambulia mmoja wenu (kumuua), basi na awe kama bora wa wana wawili wa Adamu.”

Kwa kila Muislamu, kwa kila afisa, mwanajeshi, na polisi, kwa kila mtu mwenye kumiliki silaha:

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alitupa sababu ya kufikiria kwayo, na alitulazimisha kuitumia ipasavyo. Mtu hapaswi kutenda, kufanya chochote, au kusema neno lolote kabla ya kujua hukmu yake ya kisheria. Na kujua hukmu ya kisheria kunahitaji kuelewa uhalisia ambao hukmu hiyo inapaswa kutumika. Kwa hivyo, Muislamu lazima awe na ufahamu wa kisiasa, aone mambo jinsi yalivyo kweli, na asiburutwe nyuma ya mipango ya makafiri wakoloni ambao hawatutakii mema wala Uislamu, na ambao wanajitahidi kwa nguvu zote, udanganyifu, na ujanja kututenganisha, kudhibiti ardhi zetu, na kupora uwezo na rasilimali zetu. Kwa hivyo Muislamu anawezaje kukubali kuwa chombo mikononi mwa makafiri hao wakoloni, au mtekelezaji wa amri za vibaraka wao?! Je, anatamani sehemu ndogo ya mali za kidunia zinazomalizika na hivyo kupoteza Akhera yake, akiwa miongoni mwa watu wa Motoni milele humo, aliyelaaniwa na kufukuzwa kutoka kwa rehema ya Mwenyezi Mungu? Je, Muislamu anakubali kumridhisha yeyote kati ya wanadamu dhaifu aliyeumbwa huku akimkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, Ambaye mkononi mwake mna mamlaka ya dunia hii na Akhera? Someni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na muamue msimamo wenu:

[وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيراً مِّنَ الْجِنِّ وَالإِنسِ لَهُمْ قُلُوبٌ لاَّ يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لاَّ يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لاَّ يَسْمَعُونَ بِهَا أُوْلَـئِكَ كَالأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ أُوْلَـئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ]

Na tumeiumbia Jahannamu majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika.” [Al-A‘rāf:179].

Je, mnakubali kuwa kama ng'ombe, bali wenye kupotea zaidi kuliko wao—ili msinufaike na macho yenu, wala masikio yenu, wala akili zenu, na mkawa miongoni mwa watu wa Motoni?!

Enyi Waislamu:

Hakika Hizb ut Tahrir inamwonya kila Muislamu dhidi ya kuchukua chochote kutoka kwa Muislamu, damu yake, mali yake, au heshima yake na inawaonya kuhusu ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na adhabu yake kali. Wallahi, jambo hilo ni zito na si mzaha. Kwa hivyo msiwe miongoni mwa walioghafilika ambao hawaamki isipokuwa wakati wa kifo, pindi hakuna wakati wa majuto, na wakati imani ya nafsi haitainufaisha ikiwa haikuamini hapo awali au kupata mema kupitia imani yake. Wala msidanganyike na starehe ndogo ya dunia, kwani itatoweka pasi na budi, na kwa hakika kifo kiko karibu zaidi na mmoja wenu kuliko kamba ya kiatu chake. Kwa hivyo yeyote kati yenu asijiruhusu kuchukua chochote kutoka kwa ndugu yake bila haki.

Na kwa hakika Hizb ut Tahrir inakulinganieni ili kunyanyua kiwango chenu cha ufahamu wa kisiasa, kushikamana na hukmu za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kufanya kazi pamoja nayo ili kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, ili mikono ya makafiri wakoloni na vibaraka wao iondolewe kutoka kwenu, na njama zao katika ardhi zetu zitibuliwe.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ * وَاتَّقُواْ فِتْنَةً لاَّ تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنكُمْ خَآصَّةً وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa. Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Al-Anfāl:24-5]

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-uttahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-uttahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu