Jumanne, 24 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  18 Rabi' I 1447 Na: H 1447 / 009
M.  Jumatano, 10 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Umbile la Kiyahudi ndilo Tatizo Kubwa zaidi katika Nchi za Kiislamu
Na Waungaji Mkono wake ndio Tatizo Kubwa Zaidi Duniani Ewe Trump!
(Imetafsiriwa)

Vyombo vya habari viliripoti taarifa ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Gaza, ambapo alisema, “Gaza ni tatizo kubwa kwa Israel na Mashariki ya Kati.” Hatujamsikia hata mmoja wa watawala wajinga wasio na maana (ruwaibidha) katika nchi za Kiislamu akimjibu, akimwambia kwamba umbile nyakuzi la Kiyahudi ndilo tatizo kubwa katika nchi za Kiislamu, na kwamba nyinyi ndio mnaliruzuku zana za kijeshi na msaada wa kisiasa na kiuchumi. Nyinyi ndio tatizo kubwa katika ulimwengu wote. Mfumo wenu wa kibepari ndiyo sababu ya masaibu ya dunia, na nyinyi ndio sababu ya kugawanyika kwa nchi za Kiislamu katika dola dhaifu na maumbo hafifi tiifu kwenu.

Rais huyu mwenye kiburi asingetoa kauli kama hiyo lau angempata mtu mmoja miongoni mwa watawala wa Waislamu ambaye angejibu kauli yake, akakusanya majeshi ili kulitokomeza umbile vamizi la Kiyahudi, na kumletea kipofu huyu ukweli kwenye hisia zake na akili timamu; kwamba umbile la Kiyahudi ndilo ambalo limenyakua ardhi iliyobarikiwa, na kwamba ni umbile hilo ndilo linalowaweka watu wake kwenye mateso mabaya zaidi, na kwamba kiburi chake kimefikia hata nchi jirani na za mbali.

Tatizo la nchi za Kiislamu lilianza kwa kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah mwaka 1924, na kugawanyika kwake kuwa dola ndogo ndogo, dhaifu, zinazodhibitiwa na makafiri wakoloni. Haya yalifuatiwa na unyakuzi wa Palestina na kuasisiwa kwa umbile vamizi la Kiyahudi huko, kwa msaada wa Uingereza, kisha ufadhili wa Amerika, na khiyana ya watawala wa Kiislamu, ambao walianzisha umbile la Kiyahudi, kisha wakalilinda na kuwazuia Waislamu kuikomboa Palestina. Hii ndiyo hali ya watawala Ruwaibidha katika nchi zetu; baadhi yao wanalilinda umbile la Kiyahudi, baadhi yao wanafanya makubaliano nalo waziwazi na kubadilishana nalo mahusiano ya kidiplomasia, baadhi yao wanaanzisha mahusiano nalo nyuma ya pazia, baadhi yao wanalalamikia Baraza la Usalama pindi ndege zake zinaposhambulia ardhi na ubwana wao, baadhi yao wanalaani upinzani wa Waislamu kwao huko Palestina, baadhi yao wanashiriki nao katika kuwazingira watu wa Gaza, baadhi yao wakaingia katika Makubaliano ya Abraham, na wote wanayafungia majeshi kwenye kambi zao na kuwazuia kuikomboa Palestina, na wanawazuia watu wao hata kueleza kupinga kwao mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza. Ni maovu kiasi gani wanayoyafanya!

Sisi, katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, tunamfikishia Trump na viongozi wa umbile katili la Kiyahudi habari njema kwamba hali hii haitadumu. Mumeona mabadiliko katika rai jumla ya umma ya kimataifa kuhusu uhalifu wa umbile la Kiyahudi mjini Gaza. Umma wa Kiislamu umetambua njia yake na unasonga mbele kwa kasi kuelekea kusimamisha dola yake, dola ya Khilafah ambayo inazijaza nyoyo zenu uoga na hofu. Wakati huo, hamtasikia jibu kutoka kwa Khalifa wa Waislamu; bali, mutaona majeshi makubwa, ambayo wa kwanza wao yuko kwenu na wa mwisho wao yuko kwake. Hizb ut Tahrir inaongoza Ummah kwa hatua za haraka za kufikia lengo hili, basi jitayarisheni kwa yale yatakayokuudhini, kwani kesho iko karibu kwa wale wanaoiona.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu