Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 22 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: H 1446 / 125 |
M. Jumatano, 18 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Majibu ya Aibu ya Tawala katika Nchi za Waislamu kwa Uvamizi wa Umbile la Kiyahudi dhidi ya Iran!
(Imetafsiriwa)
Yeyote anayetazama miitikio ya tawala zilizopo katika ardhi za Waislamu kwa mashambulizi ya umbile la Kiyahudi dhidi ya Iran atahisi huzuni kubwa na masikitiko kwa hali ya sasa ya Waislamu. Wengine wamelaani na kushutumu pekee; wengine wameonyesha hofu ya machafuko katika eneo hilo kutokana na mashambulizi haya. Baadhi walieleza kuwa ni ongezeko la hatari; wengine walielezea wasiwasi wao juu ya athari zake kwa kadhia ya Palestina. Wengine hata walitangaza kuwa tayari kufanya upatanishi kati ya Iran na umbile la Kiyahudi. Walio bora zaidi walionyesha nia ya kuiunga mkono Iran katika majukwaa ya kimataifa, huku baadhi ya nchi hizo hizo zikifungua anga zao kwa ndege za umbile la Kiyahudi kuruka juu, kuipiga Iran kwa mabomu, kuua na kuharibu, na kisha kuregea bila hata risasi moja kufyatuliwa kwao! Wengine walinasa makombora na droni za Iran zilizolenga kushambulia umbile la Kiyahudi, na hivyo kuwaepusha na kupigwa!
Hivi kweli yamefikia hapa enyi Waislamu?! Badala ya kushuhudia nchi za Waislamu zikikimbia kupeleka ndege, makombora, vifaru, mizinga na wapiganaji ili kuzuia uvamizi wa umbile haramu la Kiyahudi dhidi ya nchi mwenzetu ya Kiislamu, tunaona kulaaniwa kwa uoga na fedheha! Tunaona kujitoleo kwa usuluhishi wa kijasiri, kana kwamba mpatanishi ni upande usiofungamana na upande wowote usio husiana na Uislamu na Waislamu, kana kwamba yeye si mtawala wa mojawapo ya nchi kubwa za Kiislamu, ambayo hapo zamani ilikuwa mji mkuu wa Khilafah kwa karne tano! Hata baya zaidi ni tawala katika nchi zilizoko kati ya Palestina na Iran, zile ambazo anga zake ndege za umbile la Kiyahudi zilipitia na tawala zilizotungua makombora ya Iran. Msiba mkubwa zaidi uko katika tawala zilizowapokea raia wa umbile la Kiyahudi kwenye viwanja vyao vya ndege waliporegea Palestina baada ya viwanja vya ndege vya umbile hilo kufungwa kutokana na mashambulizi ya Iran!
Tunafahamu vyema shauku ya Waislamu kwa ajili ya jihad na kupigana na Mayahudi. Tuliona furaha ya watu wakitazama makombora na droni za Iran zikiruka juu ya vichwa vyao ili kushambulia umbile la Kiyahudi. Tuliona sherehe katika nchi nyingi za Kiislamu ziliposhuhudia makombora hayo na droni zikisababisha vifo, majeraha na uharibifu ndani ya umbile la Kiyahudi. Hatimaye walionja sehemu ya yale waliyowafanyia Waislamu mjini Gaza, Palestina, Lebanon, Syria na Yemen. Siku moja ilifika ambapo walijikuta wakihesabu maiti zao, majeruhi, na waliopotea kutokana na makombora na droni, kama tulivyofanya huko Gaza, na wanaendelea kufanya hivyo, kutokana na uhalifu wa umbile la Kiyahudi na kampeni zake za mauwaji ya watu wengi.
Enyi Waislamu: Mnasoma maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ]
“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini, Na aondoe hasira ya nyoyo zao.” [Surat At-Tawba:14-5].
Nyinyi mnaitamani siku ambayo Mwenyezi Mungu atakupeni ushindi juu ya Mayahudi, na kuziponya nyoyo zenu, na kukuondoleeni hasira zenu. Mnaposoma katika maneno ya Mwenyezi Mungu, hili linakuja kupitia kupigana nao, kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu. Haliepukiki. Ni sehemu ya Aqidah (itikadi) yenu katika yakini ya ushindi. Amri na matokeo yake katika Aya tukufu ni kama sharti na majibu yake. Maana yake ni: Piganeni nao, na pindi mkipigana nao, Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa mikono yenu, na atawafedhehesha, na atakupeni ushindi juu yao, na ataziridhisha nyoyo zenu, na ataondoa hasira zenu.
Mnaweza kusema: “Watawala wetu wanatuzuia kupigana na Mayahudi. Hiyo ni kweli na hii inalazimu kuunganisha juhudi za kuwaondoa hawa Ruwaibidha (watawala duni) wanaowatumikia Mayahudi na makafiri nyuma yao. Sisi katika Hizb ut Tahrir uongozi wa ikhlasi ambao kamwe hauwasaliti watu wake, na mbebaji mradi wa Khilafah kwa njia ya Utume, tunakuombeni mufanye kazi nasi na mutuunge mkono kuwaondoa watawala hawa na kusimamisha Khilafah Rashida. Ili Mwenyezi Mungu Mtukufu aone kutoka kwetu na nyinyi yale anayoyapenda: kuwapiga vita Mayahudi na makafiri wakoloni, na kuliondoa umbile haramu la Kiyahudi kutoka uwepo, bila kusaza alama yoyote, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
[وَلَيَنصُرَنَّ اللهُ مَن يَنصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ]
“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Surat Al-Hajj:40]
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |