Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Takbira “Allahu Akbar na Sheria ni ya Mwenyezi Mungu Pekee”
- Imepeperushwa katika Tunisia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya swala ya Ijumaa mnamo tarehe 5 Dhul-Hijjah 1447 H, matembezi ya Takbira (Allahu Akbar) yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia yalianza kutoka Msikiti wa Al-Fath katika mji mkuu, Tunis. Umati mkubwa wa Watunisia ulishiriki, wakipiga Takbir na Tahleel (Allahu Akbar na La Ilaha illa Allah), na kuandamana kupitia barabara kuu za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra (Mapinduzi). Mabango yaliinuliwa, ikiwa ni pamoja na moja lililoandikwa, “Allahu Akbar, na sheria ni ya Mwenyezi Mungu pekee,” jengine liliandikwa, “Allahu Akbar: Uislamu ndio kitambulisho chetu na Khilafah ndio Dola yetu,” na la tatu liliandikwa, “Allahu Akbar, Uislamu ni dini yetu na njia yetu ya maisha, Khilafah ni dola yetu, na Jihad ni njia yetu.”



