- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Kongamano la kila Mwaka la Khilafah: “Kufeli kwa Serikali ya Kisasa na Kutoepukika kwa Dola ya Khilafah”
Hizb ut Tahrir/Wilayat Tunisia ilifanya kongamano lake la kila mwaka la Khilafah mnamo siku ya Jumamosi, 26 Aprili 2025, katika ukumbi wa mikutano kwenye makao makuu ya Hizb katika makutano ya barabara ya Sakra katika mji mkuu, Tunis, chini ya kichwa:
“Kufeli kwa Serikali ya Kisasa na Kutoepukika kwa Dola ya Khilafah”
Kumbi mbili zilizotengwa kwa ajili ya wageni zilijaa idadi kubwa ya wanaume na wanawake waliofika kwenye kongamano hilo kutoka pande zote za ardhi ya kijani ya Tunisia. Shughuli za kongamano hilo zilianza kwa kusomwa baadhi ya aya za Qur'an Tukufu, zilizosomwa kwa waliohudhuria na Ustadh Muhammad Ali Al-Aouni, na kufuatiwa na hotuba za kongamano.
Hotuba ya kwanza ilitolewa na Ustadh Mohamed Bouaziz chini ya kichwa “Kufeli kwa Dola ya Kisasa... Tunisia ni Mfano.” Kisha Ustadh Taher Nasr alizungumza chini ya kichwa “Sifa Muhimu Zaidi za Mfumo wa Utawala katika Uislamu.” Baada yake, Ustadh Ibrahim Al-Shater alitoa hotuba yenye kichwa “Sera ya Elimu katika Dola ya Khilafah.” Hii ilifuatiwa na hotuba ya Ustadh Tariq Rafi ambapo alieleza “Sifa za Mfumo wa Kiuchumi katika Uislamu.” Hotuba ya mwisho ilikuwa ya Ustadh Omar Al-Arabi ambayo alieleza “Sera ya Kigeni katika Dola ya Khilafah.”
Kongamano lilihitimishwa kwa barua iliyotumwa na Ustadh Najmuddin Shuaibin kwenda kwa Netanyahu kujibu kauli zake za kupinga Khilafah. Kauli mbiu ziliimbwa wakati wa hotuba hizo, zikiwemo “Netanyahu, sikiliza, sikiliza, Khilafah yetu itaregea,” na “Khilafah, Khilafah, Khilafah,” na kauli mbiu nyinginezo.
Hivyo basi, Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia inaendelea na kazi yake isiyochoka ya kufichua kufeli kwa dola ya kisasa na sheria zake mbovu na zisizo za haki, na wakati huo huo ikiwasilisha mradi wa Dola ya Khilafah Rashida katika maelezo yake yote kwa watu wa nchi hii. Kongamano hilo lilisambazwa sana hasa kwenye mitandao ya kijamii na kuwa gumzo nchini Tunisia. Kama kawaida, mashini za wale wanaojiita wanausasa ilihamasishwa kujaribu kuipaka tope Hizb na mradi wake wa hadhara, lakini kama kawaida, wanatweet nje ya hatua ili kuwafurahisha mabwana zao, tofauti na watu wengi wa nchi ambao waliingiliana vyema na kile ambacho Hizb ut Tahrir inachopendekeza na mradi wake wa hadhara, ambao unathibitisha kwamba watu wa Tunisia ni waaminifu kwa itikadi yao, itikadi tukufu ya Uislamu.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia
Jumamosi, 28 Shawwal 1446 H sawia na 26 Aprili 2025 M
Matangazo ya Moja kwa Moja ya Amali za Kongamano la kila Mwaka la Khilafah
Sehemu ya Amali za Kongamano la kila Mwaka la Khilafah
https://www.hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/4637.html?print=1&tmpl=component#sigProId38430b2064
- Mwaliko wa Kongamano la Khilafah la kila Mwaka -
Mwaliko 1
Mwaliko 2
- Alama Ishara za Amali -
#أقيموا_الخلافة
#كيف_تقام_الخلافة
ReturnTheKhilafah#
#YenidenHilafet
#خلافت_کو_قائم_کرو
#TurudisheniKhilafah
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir