Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Sudan: Giza la Muundo wa Makubaliano au Nuru ya Katiba Inayotokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake?
(Imetafsiriwa)

Haishangazi kwa mtu yeyote anayefuatilia hali ya kisiasa nchini Sudan kujua kwamba vita hivi viliratibiwa na kusimamiwa na Marekani chafu na yenye nia mbaya ili kufanikisha ajenda yake na kuvunja nguvu za washindani wake wa Ulaya, hasa raia wanaoshirikiana na Uingereza. Vita hivi vinafadhiliwa na Amerika, ni mchezo wao uliolaaniwa. Ushahidi wa wazi zaidi ni kwamba taarifa kuhusu kurefusha vita ilitoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Blinken. Kurefushwa kwa vita hivi si kwa ajili ya utatuzi au kuhifadhi damu au kukomesha uharibifu ambao umeharibu nchi na watu wake; badala yake, ni mapambano ya nyuma na mbele na jaribio la kuweka maono ya kisiasa ambayo yanahakikisha na kuhifadhi maslahi ya Marekani nchini.

Taarifa za hivi karibuni za Marekani za kutaka amani na kukomesha vita sio kulinda maisha, kukomesha umwagaji damu, au kwa kujali Sudan na utu na heshima ya watu wake, hili ndilo jambo la mwisho analofikiria mkoloni. Badala yake, ni juu ya kutekeleza amani kupitia mamlaka ili kufikia mambo mawili: Kwanza, kulazimisha udhibiti wa Amerika na kujitangaza yenyewe kama dola inayoongoza ulimwenguni, kusimamisha vita wakati inaporidhika na kuruhusu viendelee wakati inapotaka. Pili, kuhifadhi maslahi ya Amerika duniani kote, ikiwemo Sudan. Vita ilivyovianzisha ili kuondoa ushawishi wa Ulaya vitasimamishwa mara tu maslahi hayo yatakapopatikana kupitia maono ya kisiasa inayolazimisha. Katika hali zote, matokeo yake ni uharibifu kwa Sudan, kuteseka kwa watu wake, umwagaji damu, ukiukwaji wa utu, na uporaji wa mali.

Uhalisia huu sio wa ajabu wala wa kushangaza, bali ni kawaida chini ya mfumo wa kibepari. Katika ulimwengu wa leo chini ya mfumo huu potovu, ni serikali gani inayowapa watu wake maisha yenye ufanisi? Ni nchi gani inayotoa maisha ya utu, usalama kwa raia wake, mali zao, heshima yao, dini yao, na haki zao, bila ya kuporwa rasilimali zake na Amerika au wengineo, bila kuteseka kiuchumi? Lakini kinaya kilicho uchungu zaidi ni kwamba serikali inayotekeleza sera za Marekani inakuja chini ya jina la “Serikali ya Matumaini,” yenye waziri mkuu ambaye alikuwa afisa wa zamani wa Umoja wa Mataifa!

Je, kuna matumaini gani, wakati serikali hii, ambayo dhamira yake ni “kufanikisha usalama, ufanisi, na ustawi wa watu” inakusudia kutimiza malengo haya kupitia mfumo ule ule wa kidemokrasia wa kisekula ambao umekuwepo tangu kuingia kwa majeshi ya mkoloni Kitchener nchini Sudan mwaka 1898 hadi leo? Umefeli kabisa, haukuleta usalama, wala ufanisi, wala ustawi. Badala yake, ni matabaka juu ya matabaka ya giza: kuanzia kujitenga kwa Kusini na vita vya umwagaji damu vilivyodumu kwa miaka chini ya al-Bashir, hadi vita kati ya al-Burhan na Hemetti, hadi majaribio ya kuitenga Darfur, yote yakisababisha makumi ya maelfu ya watu waliokandamizwa, uporaji wa mali ya taifa, na uharibifu wa miundombinu.

Taarifa za kisiasa kati ya pande zinazozozana zinahusu hisa katika serikali ya mseto, ya kitaalamu au vyenginevyo, nyadhifa au viti katika serikali ambayo haifanyi lolote ila kutekeleza maagizo ya Amerika. Mizozo inazungunga pambizoni mwa haki za makundi yaliyotengwa au ustahili wa nyadhifa za mawaziri... Kauli mbiu zisizohesabika, kelele nyingi, lakini hakuna hatua halisi. Mawaziri wote hawa na watu wanaotaka kuwa viongozi wa kisiasa walioundwa na Amerika wanatafuta tu matamanio ya kibinafsi na hadhi ya kidunia. Wanawasilisha kwa watu wanaoteseka kauli mbiu zinazovutia kuhusu matumaini na ufanisi, ilhali hakuna hata mmoja wao aliye na mpango wazi au mradi wa kina wa kuiinua Sudan, kuijenga upya, na kuhifadhi damu na heshima ya watu wake.

Miongoni mwa vyama vya kisiasa, hakuna kama Hizb ut Tahrir, mkweli kwa watu wake ambayo ina mradi wa kina na wa wazi unaotokana na itikadi ya watu wa umma huu wa kheri.

Mradi wenye uwezo wa kumaliza mizozo ya umwagaji damu na kuiokoa Sudan kutokana na mapambano ya kisiasa ya dola zenye ulafi, kwa sababu Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho lengo lake ni kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Inawasilisha kwa uwazi fikra na mradi wake kwa umma na inahutubia Ummah na majeshi yake changamfu ili kuutabanni na kuuunga mkono ili uweze kutabikishwa, na kuleta fahari kwa Uislamu na watu wake.

Mradi huu unawasilishwa kwa Ummah na wabebaji wake ni wale wanaobeba Uislamu kama fikra na twarika (njia). Unajulikana sana, sio jambo lisiloeleweka, na iko wazi kwa ajili ya mjadala kupitia ushahidi na dalili za Kiislamu. Hizb inauhakikishia Ummah kwamba kwa kuutekeleza mradi huu, uliotokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Wake, mateso yake yatakwisha, na utaachwa huru kutokana na udhalimu wa Marekani, Ulaya na nyenginezo. Ina wanaume wanaojali juu ya kuinuka kwa Ummah wao, sio kupata vyeo. Wanajua kwamba jukumu lao kwa Ummah na kutabikishaji Sharia ya Mwenyezi Mungu ni faradhi ambayo kwayo watahisabiwa mbele ya Mwenyezi Mungu, sio kiti cha fahari katika Umoja wa Mataifa au Baraza la Usalama.

Tofauti kati ya “Serikali ya Matumaini” na Mradi wa Muundo wa Makubaliano au mpango mwengine wowote ambao Amerika inautayarisha kwa ajili ya Sudan, na kati ya mradi wa kikatiba uliotayarishwa na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya Ummah, ni kama tofauti kati ya giza na nuru.

Watu wa Sudan wanataka serikali itakayotatua matatizo yao na kuinua maisha yao hadi kufikia kiwango cha utu, kwa kudhamini mahitaji ya kimsingi ya kila mtu (chakula, mavazi, makaazi), na kuhakikisha mahitaji ya msingi ya pamoja (usalama, elimu, huduma za afya), pamoja na maji safi, umeme, miundombinu (mitandao ya mawasiliano, barabara, madaraja, nk.), na kukomesha uporaji wa mali zao zote za umma, kurudisha mali za umma kwa wamiliki wake halali, ambayo yote yanahitaji kung'oa ushawishi wa kafiri mkoloni kutoka katika ardhi zetu. Hili ndilo linaloleta matumaini ya kweli kwa watu wa Sudan, jambo ambalo serikali ya Kamal Idris haiwezi kufanikiwa, kwa sababu tu inatekeleza usekula, ambao umethibitisha kufeli kwake duniani kote katika ngazi zote. Mfumo huu unatabanni itikadi ya kutenganisha dini na maisha, kunyima haki ya Muumba kutunga sheria, na kuifanya raha ya mtu binafsi na matamanio lengo kuu na njia ya kufikia furaha. Unapigia debe dhana ya mwenye nguvu mpishe, ambapo mafanikio yanapimwa kwa faida ya kibinafsi kwa gharama yoyote, hata ikiwa inadhuru wengine “sheria haiwalindi wapumbavu.” Unakusanya mali mikononi mwa kipote kidogo kinachochukuliwa kuwa wanaostahili kutokana na akili zao na uwezo wa kupata, bila kujali wanyonge au wasio na bahati. Hamu ya serikali ni kudumisha uzalishaji wa hali ya juu na udhibiti wa kiuchumi ili kulinda maslahi yake. Ni mfumo ambao watu binafsi hawana thamani isipokuwa katika kutumikia tabaka la juu. Unaruhusu ukiukwaji wa matukufu ya watu na ufujaji wa mali zao, na kuhalalisha jinai hizi kwa jina la haki za binadamu na uenezaji uhuru!

Mifumo ya kidemokrasia huzalisha wahalifu, kulea uhalifu, na kufadhili ufisadi kutokana na adhabu zake dhaifu. Wanadhani wao wana huruma zaidi kuliko Muumba wao, na baada ya ukafiri hakuna dhambi jengine kubwa zaidi.

Matumaini ya kweli kwa Sudan yapo chini ya Uislamu pekee, imani na mfumo kamili wa maisha unaokumbatiwa na watu wa Sudan hadi Siku ya Kiyama.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإسلام دِيناً]

“Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.” [Al-Ma’idah: 3].

Uislamu huu ndio haki, na matumaini yanaweza tu kuzaliwa chini ya haki. Pindi mfumo wa Khilafah unapoanzishwa, matumaini ya maisha yenye hadhi chini ya Uislamu huzaliwa, kwa sababu zifuatazo:

1. Khalifa atabatilisha mara moja katiba iliyotungwa na mwanadamu na kuanza kutabikishaji wa katiba ya Kiislamu inayotokana na Qur’an na Sunnah, na hivyo kuukata mkono wa kafiri Magharibi na kukataa uingiliaji wote wa kigeni.

2. Khalifah atateua haraka manaibu na magavana na kuanza kutatua matatizo ya watu bila ya kugawanya sehemu yoyote, kwa sababu mamlaka, kwa mujibu wa Sharia, ni ya Ummah, si ya wale wanaobeba silaha au wanaoshirikiana na dola za kigeni. Ataleta karibu watu wenye elimu, uchamungu, na uongofu, na hivyo kuleta kitambulisho cha kweli cha Umma.

3. Khilafah itasitisha makubaliano yote batili ya kisiasa au kiuchumi na dola za kigeni, na kukomesha uporaji wa utajiri wa Sudan na nchi za Magharibi. Itajengwa juu ya rasilimali za kifikra na nyenzo za kimada za umma ili kuinuka tena kama dola inayoongoza ulimwenguni, kama ilivyokuwa hapo awali.

4. Khilafah itaondoa mapango yote ya ujasusi wa kigeni. Dori ya afisi za balozi na misheni za balozi za kidiplomasia zitakuwa tu katika kufikisha ujumbe kati ya Khalifa na dola za kigeni sio kuingilia siasa au kuzurura nchi kupora rasilimali zake. Pia itahakikisha haki za raia wasio Waislamu (dhimmi), bila kujali dini zao au kabila, kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, kukomesha suala la makundi yaliyotengwa, ubaguzi wa rangi na madhehebu. Uislamu unamdhamini kila mtu haki zake.

5. Khalifa ataunganisha majeshi yote chini ya uongozi wake, na kusitisha ghasia za wanamgambo wapya wanaochipuka kila uchao na baya zaidi, wengine wanapewa mafunzo nje ya nchi! Je, tunawezaje kutafuta matumaini na maisha yenye staha chini ya makundi hayo yenye silaha yalivyovunjika vunjika?

6. Khilafah itatumia uwezo wake wote wa vyombo vya habari kueneza ujumbe wa Uislamu, uadilifu wake na ukweli wake, kwa ulimwengu. Itakuuza thaqafa ya Kiislamu, kuunga mkono sayansi na wanazuoni, na kujitahidi kuondoa fikra au dhihirisho lolote la kithaqafa lisilomridhisha Mwenyezi Mungu. Jamii itakuwa yenye udugu, huruma, na ushirikiano katika uongofu na uchamungu. Sambamba na hayo, itahakikisha utoaji wa mahitaji ya kimsingi kwa watu binafsi na jamii, kurudisha umiliki wa umma na serikali katika maeneo yao stahiki, na kutumia mali pale Mwenyezi Mungu alipoagiza, pamoja na utekelezaji wa adhabu za Kiislamu ili kudhamini usalama wa jamii ambayo watu wanaishi kwa usalama, wakiangazia ufanisi, maendeleo ya kifikra na kisiasa, na kubeba Uislamu, sio kuuwana wao kwa wao na kueneza ufisadi na ghasia.

Hili ni tone tu kutoka katika bahari ya hukmu za Kiislamu. Tunapoziwasilisha kama mradi kwa Ummah, wanaweza kweli kufufua matumaini ya maisha yenye staha. Na siku zitakapotabikishwa, maisha yetu yatabadilika, na matumaini yatageuka kuwa vitendo, vyenye kutuinua tena kwenye vilele vya izza kama hapo awali. Na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].

 أزمة_السودان #         #SudanCrisis

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bayan Jamal

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.