Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

“Kujitawala Wenyewe” kwa Mujibu wa Matakwa ya Wakoloni!
(Imetafsiriwa)

Ushawishi wa Wakoloni makafiri wa Kimagharibi ulishuka kwenye ardhi za Waislamu, na kuzigawanya na kuzichana vipande vipande. Uliziacha zikiwa zimevunjika, zimechanika, kipande hapa na chngine kule. Yaliyotokea nchini Iraq katika upande wa muungano wa kikabila na mgawanyiko, kutenganishwa kwa Pakistan ya Mashariki na Magharibi, kutenganishwa kwa Timor Mashariki kutoka Indonesia, na kutenganishwa kwa Sudan Kusini kutoka Kaskazini, yote yanaonyesha jinsi ardhi za Waislamu zilizogawanyika zinavyoendelea kutembea kwenye njia ya mgawanyiko zaidi na kusambaratika.

Ardhi zetu za Kiislamu zimekuwa jukwaa la kupigania mali na ushawishi kati ya Marekani na Ulaya. Cha kusikitisha ni kwamba, zana za mapambano haya ni baadhi ya wana wa Ummah, iwe katika serikali au vuguvugu la waasi, kama inavyotokea leo nchini Sudan, wakati wanaoshindwa pekee katika vita hivi ni watu wasio na hatia, wasio na nguvu.

Ili kufikia malengo yake ya mgawanyiko nchini Sudan, nchi kafiri za Magharibi zilitumia mbinu mbalimbali ovu na kutekeleza mpango mmoja baada ya mwingine. Zilichochea mivutano ya kijamii, kijiografia, na kikabila na kukuza wazo la “haki ya kujitawala,” ibara ya kusisitiza kujitenga na mgawanyiko katika lugha ya siasa za kimataifa.

Msururu wa migawanyiko ulianza kwa ukaliaji kimabavu wa Misri wa Uingereza mwaka 1882, baada ya hapo ilifanya kazi ya kuigawanya, kufuatia mpango wake uliowekwa kwa ajili ya nchi za Kiislamu. Marekani na Uingereza kisha zilifanya kazi kutayarisha rai jumla ya umma kukubali wazo la kujitenga kwa kutia saini makubaliano mwaka 1953 ambayo yaliainisha kile walichokiita “haki ya kujitawala” kwa watu wa Sudan na kufanyika kwa kura ya maoni maarufu chini ya usimamizi wa kimataifa. Makubaliano haya yalifungua njia ya kujitenga kwa Sudan kutoka Misri na kutangazwa kwa Jamhuri ya Sudan mnamo 1956.

Ujanja wa Uingereza haukuishia hapo; ilikwenda mbali zaidi, ikifanya kazi ya kuigawanya Sudan katika dola mbili, moja Kaskazini na nyingine Kusini. Ilianza kutekeleza mpango huu baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia mnamo 1922, ikitabanni sera ya kuitenga Kusini kutoka Kaskazini. Iliweka vikwazo vikali juu ya kuenea kwa Uislamu katika maeneo ya kusini (Equatoria, Bahr al-Ghazal, na Upper Nile), ilipiga marufuku mila na desturi za kaskazini, na kuwahimiza watu wa kusini kuwatazama watu wa kaskazini kwa shaka. Mnamo 1930, Uingereza ilitoa uamuzi kuwatangaza watu wa kusini kama watu tofauti na watu wa kaskazini. Iliunga mkono wamishonari na wajumbe wa wamishonari kusaidia waasi, majasusi, kuchochea uasi, kueneza uasi, na kupigia debe mawazo ya kiadui na nia mbaya dhidi ya Waislamu. Kabla ya kuondoka Sudan, Uingereza ilichukua hatua nyingi za kuongeza mgawanyiko kati ya watu wa kaskazini na kusini moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia vibaraka wake katika makoloni jirani.

Wakati ushawishi ulipohama kutoka Uingereza hadi Amerika, Amerika ilitabanni fikra ya mgawanyiko kwa kutumia mbinu zake. Licha ya kutofautiana kwa maslahi ya Marekani na Uingereza nchini Sudan, kutokana na fahamu ya matumizi iliyowekwa na mfumo wao wa kibepari, wote wawili walikubaliana juu ya fikra msingi: kutenganisha Kusini na Kaskazini na kuigawanya Sudan. Makubaliano kama hayo hutokea baina yao katika baadhi ya masuala ya kimataifa, hasa katika nchi za Kiislamu.

Mojawapo ya mbinu hatari zilizotumiwa na mataifa ya makafiri, Marekani na Uingereza kwa ajili ya kuitenganisha Sudan Kusini na Kaskazini ilikuwa ni kulifanya suala hilo kuwa la kimataifa, kuliondoa mikononi mwa Wasudan na kuliweka chini ya udhibiti wa dola kubwa ili kulitatua kwa matakwa na maslahi yao. Hiki ndicho kilichotokea kwa Sudan Kusini, ambayo, kutokana na pande nyingi za kimataifa zilizohusika, ilionekana si la Wasudan tena – au hata la Kiislamu! Kusini ilifunguliwa kwa ajili ya shughuli za kimishonari na misheni 35 tofauti tofauto, pamoja na mashirika yanayojifanya kuchukua hatua kwa misingi ya kibinadamu na haki za binadamu, yote yakitoa misaada ya kifedha ili kuhalalisha uwepo wao na kufanya hujuma chini ya kivuli hiki. Lakini Sudan, kwa hakika, ni nchi tajiri, iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa maliasili nyingi mno, kinyume na dhana iliyozoeleka kwamba ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani!

Makubaliano yalitiwa saini kati ya waasi na serikali, na suala hilo liliwekwa kama mzozo uliokita mizizi kati ya Wakristo wa Kiafrika Kusini na Waislamu wa Kiarabu Kaskazini. Kisha waliidhinisha kile walichokiita “Tangazo la Kanuni,” ambalo lilijumuisha kile kinachoitwa “haki ya kujitawala wenyewe” kwa watu wa Kusini, na kufufua wazo hili kama mojawapo ya chaguzi zinazowezekana baada ya kura ya maoni maarufu.

Hiki ndicho hasa kilichotokea. Mnamo 9 Julai 2011, Sudan Kusini ilitangaza rasmi kujitenga na kuwa dola. Kwa hivyo, Uingereza na Amerika zilifikia lengo lao la muda mrefu. Urais wa Sudan na baraza la mawaziri lilikubali rasmi matokeo ya kura ya maoni (iliyoamuliwa kabla) ya kujitawala wenyewe, ambapo asilimia 98.83% walipiga kura ya kujitenga na kuanzishwa kwa dola ya Sudan Kusini ndoto ya nchi kafiri za Magharibi. Wakati huo, Rais Obama wa Marekani aliwapongeza wale wanaojiita watu wa Sudan Kusini kwa matokeo hayo, ambayo yalipangwa kwa ujanja na kutekelezwa kipumbavu na watawala na wanasiasa wa Sudan!

Leo, Sudan Kusini iko kwenye ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, kwani imeshuhudia mivutano ya kijeshi na kisiasa inayoendelea kwa miezi kadhaa kati ya washirika wawili wanaotawala: Rais Salva Kiir Mayardit na Makamu wake wa Rais wa Kwanza Riek Machar. Mzozo huo, unaoendelea kwa miaka mingi ni uhasama kati ya makabila ya Dinka na Nuer, na kusababisha makabiliano mengi ya kijeshi, ikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano kuanzia 2013 hadi 2018, ambavyo viliua takriban watu 400,000 na kumalizika kwa makubaliano dhaifu ya amani mnamo 2018.

Hii ndiyo hatima ya dola zilizojengwa kwa makubaliano ya kikabila, au kikanda. Na hivyo, msururu wa mgawanyiko wa Sudan unaendelea hadi saa hii katikati ya mzozo wa sasa. Dalili zimejitokeza zinazoashiria uwezekano wa kujitenga kwa jimbo la Darfur kutoka Sudan, kufuatia Vikosi vya Msaada wa Haraka kuzuia mauzo ya bidhaa zinazoelekea Misri kutoka katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao huko Darfur. Mshauri wa kamanda wa Kikosi cha Msaada wa Haraka, Al-Basha Mohamed Tabeek, alisema kuwa vikosi hivyo vinahitaji kuunda serikali katika maeneo wanayodhibiti kama jambo la lazima na kwamba hatua hii inapaswa kutambuliwa mara moja na kukaribishwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ili kudumisha umoja wa Sudan.

Zaidi ya hayo, matukio yanayoendelea kwa kasi nchini Sudan yanaelekea upande mmoja kuregesha udhibiti wa jeshi katika maeneo mengi ya Sudan na kuliacha eneo la magharibi, hasa Darfur, kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka. Mwelekeo huu ukikamilika, nchi itaelekea kwenye mgawanyo halisi.

Inaonekana pia kwamba nia ya Amerika katika kutenganisha Darfur kama ilivyokuwa kwa Kusini, inaongezeka kwa kasi. Hapo awali, ilifumbia macho masuluhisho ya kisiasa ya Darfur, bila kutaka kushughulikia masuala ya kusini na Darfur kwa wakati mmoja, na kuacha faili la Darfur likiwaka moto. Iliangazia tu mafaili ya kibinadamu na usalama na suala la watu waliokimbia makaazi yao, bila juhudi za kweli za kuyatatua, kila mara ikijaribu kutuliza mivutano iliyochochewa na Ulaya, ikiihakikishia jumuiya ya kimataifa utulivu huku ikijua wazi kwamba hali ya Darfur inazidi kupamba moto.

Kama inavyojulikana vyema, mzozo wa Darfur awali ulihusisha migogoro midogo ya kimila kati ya makabila kuhusu ardhi ya kilimo, unyunyiziaji maji, malisho na maeneo ya kukusanya maji ambayo yalitatuliwa haraka na viongozi wa makabila. Masuala kama haya ni ya kawaida katika maeneo yote ya kikabila na ni sehemu ya mizozo ya kimaumbile inayotokea katika jamii za kikabila zinazohama hama. Lakini Ulaya, hasa Uingereza na Ufaransa, zilizokasirishwa na udhibiti pekee wa Marekani juu ya Sudan Kusini na kutengwa kwao, ziliwasha moto wa fitina huko Darfur kati ya makabila ya Waarabu na Waafrika, ambao wote ni Waislamu. Ulaya wakati huo ililipa nguvu za kijeshi, kuliingiza siasa, na vyombo vya habari kulikuza suala la Darfur ili kuaibisha Amerika na kuvuruga serikali ya Bashir, mshirika wa Amerika wakati huo, ili kuzuia Marekani kufurahia zawadi yake iliyoikamata Kusini na kupata nafasi ya kutia mguu wake nchini Sudan.

Sasa, wakati umefika wa kuchukua udhibiti wa faili, na Amerika inafanya hivyo. Sudan imekuwa kitu cha kuchezea mikononi mwa Amerika, anachokitumia apendavyo. Suluhisho la Marekani kwa mzozo unaoendelea wa Sudan na suala la Darfur litaakisi matukio yale yale iliyotumia kutenganisha Kusini, na hivyo kufikia lengo lake la kuikata Sudan, lakini kupitia mikono ya watoto wake yenyewe: washiriki, watekelezaji, washirika, au kimya!

Msimamo ambao watu wa Sudan wanapaswa kuchukua dhidi ya njama na mizozo hii, na kukomesha kuporomoka kwa majimbo ya Sudan, ni kujiepusha na kuendelea na batili na kutokana na kuendelea na sera ya utiifu na kukubali kuwa vipande vya chess vilivyowekwa na maadui zetu katika mtaro wowote wanaouchagua. Hatupaswi kutegemea Amerika mhalifu kushughulikia maswala ya nchi. Hatupaswi kuigeuza nchi yetu kuwa uwanja wa vita kwa maadui wa Ummah. Hili ni jambo ambalo Uislamu haulikubali, kwani linapelekea kwenye maafa makubwa: fedheha, udhaifu, mgawanyiko, mfarakano, uharibifu, na khiyana kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na waumini. Makafiri wanaua, wanapora mali, wananyakua haki, na wanazurura kwa uhuru ndani ardhi za Kiislamu kwao; hakuna tofauti kati ya Palestina na Iraq, wala kati ya Indonesia, Afghanistan, Sudan, au nchi nyingine za Kiislamu.

Basi ni lini Ummah utaamka na kuwatambua maadui zake? Je, ni lini utatenda kulingana na ufahamu huu, utabainisha zana zao, na kuzikataa moja kwa moja? Je, ni lini utafanya kazi kwa ajili ya heshima na adhama yake kwa kuutabanni Uislamu peke yake kama njia ya mwamko na wokovu, kutawala kwa sheria ya Mwenyezi Mungu na kufuata mwongozo wa Mtume Muhammad (saw) katika nyanja zote za maisha, kisiasa na nyenginevyo, kubwa pamoja na dogo? Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[فَلا وَرَبِّكَ لا يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لا يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجاً مِمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيماً]

“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.” [Surat An-Nisa:65] Na Asema:

[فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللهِ وَالرَّسُولِ إِنْ كُنْتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآَخِرِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلا]

“Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.” [Surat An-Nisa:59] Hakika huko ndiko kufuzu kukubwa:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surat Al-Anfal:24]

Kwa hivyo, je mutaitikia?

#أزمة_السودان

#SudanCrisis

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Rana Mustafa

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.