Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  26 Safar 1447 Na: 1447 / 01
M.  Jumatano, 20 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Mubashir Ahmad Atakuwa Mwathirika Mwengine wa Utawala wa Uzbekistan?
(Imetafsiriwa)

Mnamo Agosti 19 mwaka huu, mashtaka yalianza katika kesi ya jinai dhidi ya Alisher Tursunov, anayejulikana kwa jina lake bandia Mubashir Ahmad. Anatuhumiwa kwa kuchapisha machapisho yanayopigia debe mawazo ya kidini yenye msimamo mkali na ushupavu kupitia vyombo vya habari. Hapo awali alishtakiwa kwa kuandaa, kuhifadhi, au kusambaza nyezo za kidini kinyume cha sheria, na Wizara ya Mambo ya Ndani ilimweka kwenye orodha ya watu wanaotafutwa kimataifa! Uturuki ilimregesha Mubashir Ahmad hadi Uzbekistan kwa ombi lake mwezi Mei mwaka huu.

Tovuti ya Mubashir Ahmad ya Azon Global ilianza shughuli zake mnamo Novemba 2023 kwa lugha nne: Kiuzbeki, Kirusi, Kiingereza, na Kituruki. Inatoa nyenzo kuhusu Uislamu na Waislamu na habari za ulimwengu, ambapo msisitizo mkubwa unawekwa kwenye jinai zinazofanywa na umbile lililolaaniwa la Kiyahudi katika Palestina iliyobarikiwa, pamoja na sera ya kikatili ya ukandamizaji inayofuatwa na China dhidi ya Waislamu wa Uyghur. Inaonekana kwamba shughuli ya tovuti hii hailingani na maelekezo waziwazi yaliyowekwa na serikali ya Uzbekistan kuhusiana na maudhui ya Kiislamu. Walakini, ni muhimu sana kusisitiza kwamba tovuti hii kuhalisia haifanyi shughuli za uadui dhidi ya serikali ya Uzbekistan. Kwa kuongeza, inafanya kazi kabisa nje ya Uzbekistan, yaani, katika eneo ambalo sheria zake hazitumiki. Kwa hakika, si jambo geni kwamba utawala wa Uzbekistan unazikanyaga sheria zake yenyewe zilizobuniwa na kumwadhibu mtu yeyote isiyempenda.

Twamuomba Mwenyezi Mungu kwamba Ndugu yetu Mubashir Ahmad aachiliwe na aharakishe ukombozi wake kutoka katika mikono ya utawala dhalimu.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يَخْذُلُهُ وَلَا يَحْقِرُهُ» “Muislamu ni ndugu ya Muislamu, hamdhulumu wala hamtelekezi wala hamchukii.” [Sahih Muslim]

Kazi ya Mubashir Ahmad inaweza kuchukuliwa kama ishara kwa wanaharakati wote nchini mwetu na nje ya nchi. Yaani lengo ni kuonesha kuwa adhabu haiepukiki hata kama mtu anapotoka kidogo kutoka katika mwelekeo wa kisiasa usio wa Kiislamu uliowekwa na utawala wa Uzbekistan, au hata kufanya makosa madogo au mapungufu!

Lakini tunaamini kwamba wanaharakati wote ndani ya nchi yetu na nje ya nchi lazima wajifunze kutokana na kisa cha Mubashir Ahmad, kwa sababu utawala huu unatekeleza matakwa ya dola za kikoloni kama vile Urusi, Amerika na China katika kuupiga vita Uislamu na Waislamu bila kuchelewa. Kwa sababu hii, utaendelea kukuwekeeni marufuku baada ya marufuku hadi kila chembe ya dini yenu iangamiziwe.

Wakati umefika sasa wa kukoma kujisalimisha kwa utawala wa Uzbekistan na dola ovu zilizo nyuma yake, na kufanya kazi kwa ikhlasi kwa ajili ya maslahi ya kimsingi ya Uislamu na Waislamu, kwa kutafuta tu radhi za Mwenyezi Mungu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.