Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
H. 6 Rabi' II 1447 | Na: 1447 / 02 |
M. Jumapili, 28 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Katika Ziara ya Amerika: Yote yako Pamoja – Kufedheheshwa, Kusihi, Uhalali, Makubaliano, na Majukumu Mapya!
(Imetafsiriwa)
Ziara ya Rais Erdoğan wa Uturuki nchini Marekani kushiriki katika mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ilikuwa mandhari ya kufedhehesha, sio kwake tu bali kwa viongozi wote wa dola pia. Rais mwenye kiburi wa Marekani Donald Trump alitoa hotuba mbele ya Baraza Kuu ambapo alitangaza kwamba “Marekani imebarikiwa kuwa na uchumi imara zaidi, mipaka yenye nguvu zaidi, jeshi lenye nguvu zaidi...” na kwamba ndani ya miezi minane ya utawala wake aliitoza dunia kodi ya ziada ya kiasi cha dolari trilioni 17, na kwamba Marekani iko katika nafasi nzuri huku nchi zengine “zinaenda kuzimu.” Alisema kuwa maamuzi ya Umoja wa Mataifa hayana maana, na kudai kwamba alimaliza vita saba ndani ya miezi saba. Aliitaja tarehe saba ya Oktoba 2023 kama “unyama wa magaidi wa Hamas,” akizingatia kuwa suluhisho liko katika kuachiliwa huru mara moja kwa wafungwa, na kuongeza kuwa dini inayonyanyaswa zaidi duniani ni Ukristo.
Trump alielekeza matusi katika hotuba yake kwa nchi zote, kuanzia Amerika ya Kusini hadi ardhi za Kiislamu, na kutoka Ulaya hadi Urusi, akionyesha kiburi cha Marekani kwa sauti ya juu, huku wawakilishi wa nchi zilizokuwa ukumbini wakijibu kauli hizo kwa kupiga makofi!
Kisha ikaja zamu ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ambaye alizungumza kwa uwazi kuhusu Uturuki, akisema kwamba viongozi wanaokwenda kukutana na Trump wanaiomba Marekani kutatua suala la Gaza, na kwamba wanasema chochote wanachotaka nje ya Ikulu ya White House, lakini mwishowe wanakimbilia kwake. Aliongeza kuwa Erdoğan pia atakuja Ikulu ya White House, na kwamba viongozi wote wanaomba kupata dakika tano za kukutana na kupeana mkono na Trump. Kuhusu balozi wa Marekani nchini Uturuki, Tom Barrack, alisema kuwa Trump amechoshwa na Erdoğan, lakini atampatia uhalali anaohitaji, akiashiria kwamba suala sio ndege aina ya S-400 au F-16, bali “uhalali” kwanza.
Mkutano wa Trump-Erdoğan ulifanyika katika mazingira haya ya kudhalilisha. Kabla ya ziara hiyo, vyombo vya habari vilizungumza kuhusu mkutano wa siri kati ya mtoto wa Trump na Erdoğan jijini Istanbul, ambapo ilikubaliwa kununua ndege 300 za Boeing kwa badali ya kupanga tarehe ya mkutano huo. Huku viongozi wengine wakiomba muda wa dakika tano, mkutano kati ya Trump na Erdoğan ulidumu kwa masaa mawili kamili.
Wakati wa mkutano huu, Trump hakutamka hata neno moja katika kauli zake kuhusu umbile la Kiyahudi na Gaza, wala hakumkumbusha kuhusu suala la Mchungaji Brunson, wala matamshi yake kuhusu uchaguzi ulioibiwa. Badala yake, mkutano huo ulishughulikia faili tata na za gharama kubwa, ikiwemo Syria, Ukraine, uuzaji wa ndege za F-16 na F-35 na silaha za kijeshi, vikwazo vilivyowekwa juu ya dola adui chini ya Sheria ya Kupambana na Wapinzani wa Amerika, ununuzi wa Uturuki wa gesi yenye thamani ya dolari bilioni 45 kutoka upande mwengine wa dunia kwa miaka 20, licha ya eneo lake la kijiografia kusheheni gesi, nishati ya nyuklia, suala la Halkbank, na Shule ya Monasteri huko Heybeliada.
Maelezo ya mikutano hii bado hayajafichuliwa, huku Trump akisema: “Mutafurahishwa na kile kilichotokea kwa Erdogan.” Ilikuwa la kustaajabisha kwamba Trump binafsi alimpokea Erdoğan mlangoni, akachomoa kiti chake, akammiminia sifa, akafanya mkutano mrefu naye, kisha akamuaga akiuelezea mkutano huo kuwa “mzuri,” katika mandhari inayoonyesha ukubwa wa makubaliano yaliyovuliwa na dori iliyolazimishwa.
Ni jambo lisilokubalika kabisa kwa dola ambayo watu wake ni Waislamu kushirikiana na Marekani, ambayo imetangazwa kuwa adui wa Uislamu na Waislamu, mshirika katika ukatili wote unaofanyika katika ardhi za Kiislamu, inayohusika katika mauaji ya halaiki ya Gaza, na muungaji mkono kamili wa umbile la Kiyahudi. Zaidi ya hayo, kumchukulia Rais Trump wa Marekani mwenye kiburi – ambaye anautukana ulimwengu na kuukandamiza – kama “rafiki,” na kufanya makubaliano haya yote kwa ajili ya mkutano, ni jambo lisilokubalika kabisa.
Zaidi ya hayo, ukweli kwamba Idara ya Mawasiliano ilifafanua kauli za Erdoğan kwenye Fox News, badala ya kumjibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rubio, ni jambo la fedheha sana. Udhalilifu huu ambao ulifanyika kwa ajili ya mkutano na Trump unajumuisha kuweka rehani mustakabali wetu na nchi yetu, na usaliti kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Gaza, dhahiri na hadharani.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: http://www.hizb-turkiye.org |
E-Mail: bilgi@hizb-turkiye.org |