Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 23 Jumada II 1447 | Na: HTS 1447 / 66 |
| M. Jumapili, 14 Disemba 2025 |
Ripoti ya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Wamzuru Sheikh wa Twarika ya Sammaniyah katika Mji wa Wad Madani
(Imetafsiriwa)
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ulitembelea Sheikh wa Twarika ya Sammaniyah katika Jimbo la Al-Jazirah jana, Jumamosi, 13/12/2025. Ujumbe huo uliongozwa na Ustadh Mahdi Muhajir, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, akifuatana na Ustadh Abdulaziz Ibrahim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na mhandisi Walid Kamil.
Ujumbe huo ulielezea madhumuni ya ziara hiyo, ukisema kwamba inakuja ndani ya muundo wa kampeni ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ili kuzuia mpango wa Amerika wa kutenganisha Darfur.
Sheikh Al-Fatih Abdulrahman Shatout alikaribisha ujumbe huo na ziara hiyo, akisema kwamba anajua mengi kuhusu Hizb, na kwamba Hizb ut Tahrir ndiyo pekee inayotoa masuluhisho yaliyo wazi. Kisha akasema kwamba anathamini kujitolea kwa kusimamisha Khilafah, na kwamba yuko tayari kwa kazi yoyote inayofanywa na Hizb kwa ajili ya kuzuia kukatwa kwa Darfur, na kwamba misikiti yao inawakaribisha Mashababu wa Hizb wakati wowote.
Mwishoni mwa ziara hiyo, ujumbe ulimshukuru Sheikh Al-Fatih kwa mapokezi ya dhati na ukarimu.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |