Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  17 Rabi' I 1447 Na: HTS 1447 / 28
M.  Jumanne, 09 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan
Wakutana na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Wanazuoni katika Jimbo la White Nile
(Imetafsiriwa)

Jana, Jumatatu, tarehe 8/9/2025, huko Rabak, mji mkuu wa Jimbo la White Nile, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ulikutana na Sheikh Abdullah Al-Nur Tutu, Imam na Khatib wa Msikiti Mkuu wa Asalaya na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Wanazuoni wa Sudan, Tawi la White Nile, nyumbani kwake katika kitongoji cha Asalaya. Ujumbe huo uliongozwa na wafuatao Dkt. Ahmad Mohammad, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, akifuatana na Ustadh Faisal Madani, Abdul Majeed Osman Abu Hajar, na Al-Zein Abdul Rahman, wanachama wa Hizb ut Tahrir. Mkutano huo ulikuwa sehemu ya kampeni ya Hizb ut Tahrir ya kuzuia kujitenga kwa Darfur.

Mkuu wa ujumbe huo, Dkt. Ahmad, alizungumzia jinsi ziara hiyo inavyoingia ndani ya muundo wa kampeni iliyoanzishwa na Hizb kuzuia kujitenga kwa Darfur, akielezea mpango wa Marekani wa kutenganisha Darfur, kupitia mpango wa mipaka ya damu, kwa kuchana kile kilichosambaratika, na jinsi mpango huo unavyoelekea utengaji, kama ilivyotenganisha eneo la kusini. Alieleza kuwa muumini hang’atwi kutoka kwenye shimo moja mara mbili, hivyo hatutaruhusu kujitenga kwa Darfur, kama vile kusini ilivyojitenga, kutokana na haki ya kujitawala. Mkuu wa ujumbe alisisitiza umuhimu wa umoja wa Ummah, ambalo ni suala nyeti, na kwamba Umma hauwezi kuzuia miradi ya makafiri isipokuwa kwa kusimamisha Khilafah unayouunganisha.

Baada ya kuishukuru hizb, sheikh alieleza kwa ufasaha, “Ziara kuhusiana na jambo hili linalohusiana na Umma wa Kiislamu na umoja wake katika masaa haya (machache) haitoshi.” Akasema, “Magharibi wanapanga njama dhidi ya Ummah na wanapanga njama mchana na usiku.” Aliuliza kwa uwazi, “Ni nini hasa kinachohitajika kwangu?” Tukamwambia, “Fanya kazi ya kuwaelimisha watu ili kutibua mpango wa kutenganisha Darfur, na kwamba watu lazima wajue kwamba hakuna njia isipokuwa kwa umoja wa Ummah kwa kusimamisha Khilafah Rashida.”

Sheikh huyo alihitimisha hotuba yake kwa kuwashukuru wanachama wa hizb na kusema, “Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukutana na wanachama wa Hizb ut Tahrir wakati wa ziara kwake. Hata hivyo, alikuwa amesoma habari zao na aliwahi kutembelea maonyesho ya vitabu mwaka 2012.” Aliahidi kwamba maisha yake yote yaliyosalia atajitolea kwa ajili ya kuutumikia mradi wa umoja wa Umma, Mwenyezi Mungu akipenda, na akasema, “Agano liko kwa Mwenyezi Mungu.”

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.