Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  3 Safar 1447 Na: HTS 1447 / 08
M.  Jumatatu, 28 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Muungano Msingi ni Hatua ya Juu katika Kuharakisha Mpango wa Amerika wa Kutenganisha Darfur
(Imetafsiriwa)

Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), kupitia muungano wao unaoitwa Muungano Msingi wa Sudan "Ta'sis," ulitangaza mnamo Jumamosi, 26/7/2025, uteuzi wa Rais na Makamu wa Rais wa Baraza la Rais, na Waziri Mkuu, ambayo ina maanisha kuundwa kwa serikali sambamba katika mamlaka inayoendeshwa na jeshi kutoka mji wa Port Sudan, mashariki mwa nchi.

Muungano huo unajumuisha mashirika ya kijeshi, kisiasa, na kikabila, hasa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Sudan (SPLM) – Kaskazini, ambako katiba yake ya msingi ilitiwa saini Februari mwaka jana katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan daima tumefichua mpango wa Marekani na kuwaonya watu wa Sudan kwamba vita vya Sudan vina ajenda za kikoloni za kuigawanya Sudan, ambayo nyuma yake anasimama mkuu wa uovu, Amerika, kupitia vibaraka wake kutoka kwa viongozi wa jeshi na viongozi wa RSF. Kama vile serikali ya al-Bashir ilivyotenganisha Sudan Kusini kwa ushirikiano na SPLM iliyoongozwa na John Garang aliyefariki, leo serikali ya al-Burhan, pamoja na RSF, wanaendelea na suala la Darfur katika mpango huo huo, kupitia kujiondoa kwenye shaka na kukabidhi kambi za jeshi na miji kwa RSF, na kushindwa kupeleka majeshi au ndege ili kukomesha uasi wao! Wakati jeshi la Sudan linao uwezo wa kumaliza vita na kuikomboa nchi na watu, ikiwa tu hatamu zingeachiliwa kutoka mikononi mwa wanaozizuia.

Al-Bashir nyuma alikiri kwamba alipitisha kujitenga kwa Kusini kwa shinikizo la Marekani, akisema: “Kujitenga kwa Kusini kulikuwa chini ya shinikizo la Marekani, na mpango wa Marekani ni kuigawanya Sudan katika nchi tano.” (Tovuti ya Urusi ya Sputnik).

Baada ya hapo, maungamo ya nguzo za utawala wake na mawaziri wa mambo ya nje yalifuata, ambapo ina maanisha kwamba walikuwa wana ufahamu wa mpango huo na walikuwa wakiutekeleza. Leo, hali hiyo hiyo inarudiwa huko Darfur, ikipanga kujitenga kwake kupitia RSF, ambao waliimarishwa chini ya usimamizi wa kiongozi wa jeshi al-Burhan.

Inatia uchungu sana kwamba mkuu wa uovu, mkoloni wa kafiri Marekani, anaweza kuendesha vita vinavyovuna uhai nchini Sudan kupitia vibaraka wake—ambao wanatekeleza mpango huo kwa uwazi, sio kwa siri, hadharani, sio kwa faragha—kwa kusaidiwa na vyombo vya habari vya upotoshaji na wanasiasa mamluki ambao hamu yao pekee ni viti vilivyochakaa wanavyokalia, huku mkoloni kafiri akiwadhibiti.

Kugawanywa kwa ardhi za Waislamu ni uhalifu mkubwa, na kila anayeshiriki katika hilo anabeba dhambi. Amesema Mtume (saw) kama ilivyosimuliwa na ‘Arfajah ibn As’ad:

«مَن أتاكُمْ وأَمْرُكُمْ جَمِيعٌ علَى رَجُلٍ واحِدٍ، يُرِيدُ أنْ يَشُقَّ عَصاكُمْ، أوْ يُفَرِّقَ جَماعَتَكُمْ، فاقْتُلُوهُ»

Iwapo mtu atakujieni na hali mambo yenu yameshikamana chini ya mtu mmoja na kutaka kuigawanya jamii yenu au kuuvunja umoja wenu, muueni. Imepokelewa na Muslim. Na Muslim pia amepokea kutoka kwa Abu Said Al-Khudri kwamba Mtume (saw) amesema:

«إذا بُويِعَ لِخَلِيفَتَيْنِ، فاقْتُلُوا الآخِرَ مِنْهُمَا»

“Ikiwa makhalifa wawili watapewa kiapo cha utiifu, muueni wa huyo wa pili.”

Hili linathibitisha wajibu wa kuhifadhi umoja wa Ummah na kutoruhusu kugawanyika kwake.

Kwa msingi huu, sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan tunawataka wenye ikhlasi miongoni mwa maafisa wa jeshi na watu wenye mamlaka na ulinzi kuacha uhalifu huu wa kinyama na waizuie Marekani na dola zote za kikoloni na ala zao kutekeleza mipango yao ya maafa katika nchi yetu, na kunusuru mradi mtukufu wa Ummah kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kwa Khilafah pekee ndio kimbilio na wokovu.

Mtume (saw) amesema: «فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلَافاً كَثِيراً، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ، فَتَمَسَّكُوا بِهَا وَعَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ» Kwani atakaye ishi miongoni mwenu ataona ikhtilafu (tofauti) nyingi. Basi shikamaneni na Sunnah yangu na Sunnah ya makhalifa waongofu. Zikamateni kwa majego yenu.”

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.