Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
| H. 1 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: BN/S 1447 / 23 |
| M. Jumatatu, 18 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kilio cha Wafungwa Kinasikika Nyoyoni mwa Waislamu Baada ya Uamuzi wa Umbile la Kiyahudi wa Kutekeleza Taratibu za Unyongaji
(Imetafsiriwa)
Waziri wa Vita na anayeitwa Waziri wa Usalama wa Kitaifa katika umbile la Kiyahudi walitangaza kuanza kwa utekelezaji wa sheria ya adhabu ya kifo kwa wafungwa wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji. Hili lilikuja “baada ya kamanda wa Kamandi Kuu katika jeshi la uvamizi, Avi Bluth, kusaini marekebisho ya amri ya kijeshi inayohusiana na Ukingo wa Magharibi” (Raya Network). Idhini ya Knesset ya uamuzi huo haikutosha kutumia sheria hiyo kwa Ukingo wa Magharibi, ambayo haiko chini ya sheria za kiraia moja kwa moja. Marekebisho haya, yaliyotolewa chini ya amri ya kijeshi, yanaruhusu sheria hiyo kutumika ndani ya mahakama za kijeshi zinazofanya kazi katika Ukingo wa Magharibi.
Taratibu hizi zinajumuisha matumizi ya kivitendo ya sheria iliyopitishwa na umbile hilo kuwaua wafungwa wa Kipalestina. Hii inatumika kama onyo la mwisho, ikipaza sauti za wafungwa tena, ikitumai kufikia masikio ya Ummah ili kuwagusa na kuwaokoa, ikiongozwa na huruma na hisia ya heshima na wivu wa kulinda damu ya Waislamu na wafungwa wao.
Kilio hiki hakielekezwi kwa mamlaka inayoshikilia Makubaliano ya khiyana ya Oslo, hata kama Palestina yote itapotea, watu wake kuangamizwa, na wakalazimika kukimbia!
Kilio hiki hakielekezwi kwa serikali ambazo zimeliunga mkono umbile nyakuzi tangu siku lilipoteka Ardhi Iliyobarikiwa hadi leo, serikali ambazo zimepigana vita na yeyote anayepinga au hata anayefikiria kulidhuru. Hizi ni serikali zinazowaua Waislamu majumbani mwao, kuwaua, na kuwakandamiza bila sababu nyengine yoyote isipokuwa kwamba wanabeba Dini ya Mwenyezi Mungu katika nafsi zao, nyoyoni mwao, na vitendo vyao. Hawa ni watawala ambao wamewashinda Mayahudi katika uadui wao kwa waumini.
Kilio hiki hakitarajii milango ya Umoja wa Mataifa, jumuiya ya kimataifa, au dola za Magharibi na Mashariki zilizounda umbile hili, zilizotengeneza njia ya kuwepo kwake, na kuendelea kuliunga mkono, na kulipatia njia zote za ukandamizaji na mauaji zinazowapata watu wa Palestina, kufunguka kwa ajili yake.
Hiki ni kilio masikioni, hapana, bali ni kilio kilicho nyoyoni mwa Umma mmoja unaoiona Masra (eneo la Safari ya Usiku ya Mtume Muhammad (saw)) na ardhi inayolizunguka kuwa ardhi iliyobarikiwa kabisa, ya Kiislamu inayomilikiwa na Waislamu, ambapo damu ya watu wa Palestina ni sawa na damu ya watu wa Baghdad, Cairo, Ankara, Islamabad, Makka, na Madina.
Ni kilio nyoyoni mwa Umma unaoogopa adhabu na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iwapo utachelewa kuikomboa Al-Quds, mateka wake, na watu wake kutoka kwenye makucha ya ukafiri, na kujitahidi kulipia fidia kwa miongo kadhaa ya kutochukua hatua, ukitumai kwamba Mwenyezi Mungu atakubali toba ya wale miongoni mwao ambao wameshindwa!
Ni kilio kwa ari ya majeshi na wale ambao wana uwezo wa kutenda lakini wanabaki bila kuchukua hatua, wakitumai kwamba damu itachemka kwenye mishipa yao wanaposhuhudia mti wa kunyongea uliowekwa tayari kwa ajili ya ndugu zao.
Hiki ni kilio ambacho hakikubali utiifu kwa mtawala ambaye amemuasi Mwenyezi Mungu huko Palestina na katika mambo yote yanayomhusu Mwenyezi Mungu (swt). Hakikubali hofu ya ukandamizaji wa madhalimu, kuzigandama mali za kidunia zinazopita, na maslahi yaliyopitwa na wakati.
Ni kilio cha imani na Uislamu, kilio kutoka kwa Umma ambao amani yake ni moja, ambao vita vyao ni vimoja, ambao damu yao ni moja, na wafungwa wao ni wamoja. Ni Umma ambao neno lake lazima liunganishwe juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake (saw), na ambao lazima wavikanyage viti vya utawala vilivyoufunga kwa miongo kadhaa kutokana na vita vya ushindi, nusra, na ukombozi wa wafungwa na Masra. Je, kilio hiki kitawafikia watu wake stahiki?
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ * وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa * Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Al-Anfal: 24-25]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Ardhi ya Baraka-Palestina |
Address & Website Tel: 0598819100 www.pal-tahrir.info |
E-Mail: info@pal-tahrir.info |