Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 22 Safar 1447 | Na: 05 / 1447 |
M. Jumamosi, 16 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ukosoaji wa Trump wa India ... Maslahi ya Amerika, Sio Urafiki na Pakistan
(Imetafsiriwa)
Mnamo 30 Julai 2025, Rais wa Marekani, Donald Trump alitangaza msururu wa ushuru wa kulipiza kisasi dhidi ya India, akiikosoa kwa kuwa na “vizuizi vizito na visivyo vumilika vya biashara visivyo vya ushuru” na kutoza ushuru wa forodha wa 25% pamoja na faini. Huku Trump alkikiri “urafiki” na India, aliikosoa vikali kwa kununua vifaa vya kijeshi vya Urusi na mafuta ya bei nafuu wakati Marekani ilikuwa ikiishinikiza Urusi kumaliza vita nchini Ukraine. Katika karipio la hadharani lisilo la kawaida, Trump aliusifu uchumi wa Urusi na India kuwa “umekufa” na akamuonya Rais wa zamani wa Urusi Medvedev “kuchunga mdomo wake.”
Misimamo hii inayoonekana kugongana ya rais wa Marekani kwa hakika inathibitisha kwamba Marekani—iwe chini ya Trump au mtu mwengine yeyote—haina rafiki wa kweli isipokuwa maslahi yake yenyewe. Ikifanya urafiki na mtu, ni tu kutumikia na kuendeleza maslahi yake binafsi, sio kutokana na mapenzi kwa upande mwingine. Katika muktadha huu, ni wazi kuwa Trump anatenda kulingana na uhalisia huu – lakini kwa njia ya jambazi na mnyanyasaji wa kimataifa, anayedai usalimishaji kamili kutoka kwa vibaraka wake na dola zilizo chini yake, kama vile India na nyenginezo. Anatoa sifa za maneno kwa wale wanaombembeleza na kusujudia matakwa yake, na hasiti kuwadhalilisha na kuwatukana wengine wanaojaribu kumpinga au kuchelewesha kuonyesha utiifu na kunyenyekea kwa sababu ya shinikizo la ndani. Sera ya Trump si chochote ila sura halisi ya Marekani, kama kiongozi wa kimataifa wa ubepari huria wa kisekula. Mfumo huu ndio umemsukuma Trump katika muda wa miezi sita na nusu iliyopita kutafuta “mpango bora” ambao unatumikia tu maslahi ya kiuchumi na siasa za kijiografia za Marekani.
Kwa muda mrefu Marekani imekuwa ikichukulia China na Urusi kuwa wapinzani wake wakuu. Kwa hivyo, inafanya kazi kwa kutumia zana zote za shinikizo na vibaraka ili kukabiliana na kuvuruga sera na matamanio ya kambi za kimataifa zinazoongozwa na China na Urusi, kama vile BRICS, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), Jumuiya ya Uchumi ya Eurasian (EAEU), Jumuiya ya Mkataba wa Usalama wa Pamoja (CSTO), na nyenginezo. Kwa sababu hii, Amerika imewekeza pakubwa katika uhusiano wake na India tangu mwishoni mwa miaka ya 1990, ikiitumia kuidhibiti China. Ushirikiano huu wa kimkakati unaendelea hadi leo, huku serikali mtawalia za Republican na Democrat zikiipa India teknolojia ya hali ya juu ya kijeshi, makubaliano ya nyuklia ya kiraia, na ufikiaji wa taasisi za kiuchumi za Magharibi. Hii si kutokana na upendo wowote kwa India, bali ni kunenepesha na kuitumia katika kukabiliana na mahasimu wake wa kikanda – China na Urusi.
Utawala wa Trump hautabadilisha mwelekeo wa kimkakati wa ushirikiano wa Marekani-India unaolenga kuidhibiti China. Badala yake, Amerika inaamiliana na India kupitia njia ya karoti-na-fimbo. Kutozwa kwa ushuru, faini, kauli kali, na uonevu wa Marekani kuelekea India ni fimbo ambayo Trump hutumia dhidi ya “mtumishi” wake India ili kuilazimisha kufanya juhudi kubwa zaidi katika huduma yake na kufungua zaidi soko lake la ndani ili kuunda fursa kwa makampuni ya Marekani. Katika mchakato huu, Trump pia anaitumia Pakistan kuishinikiza India. Hii ndiyo sababu anajifanya “kuegemea” kuelekea Pakistan na kumtishia Modi kuyumbisha serikali yake ili kukidhi matakwa ya Marekani juu ya ratiba ya kasi zaidi.
Enyi maafisa wanyoofu katika jeshi la Pakistan! Msidanganywe na ukosoaji wa hadharani wa Amerika kwa serikali ya Modi au sifa za Trump kwa Pakistan.
"مِلَّةُ الكُفْرِ وَاحِدَةٌ" “Mila ya ukafiri ni mmoja”; kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyothibitisha katika kauli yake:
[وَالَّذِينَ كَفَرُوا بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ إِلَّا تَفْعَلُوهُ تَكُنْ فِتْنَةٌ فِي الْأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيرٌ]
“Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipo fanya hivi itakuwako fitna katika nchi na fisadi kubwa.” [Surah Al-Anfaal 8:73].
Uhalisia ni kwamba ushirikiano wa kistratejia kati ya Marekani na India bado ungali imara na unalenga dhidi ya Pakistan na Waislamu wa eneo hilo. Tusisahau jinsi utawala wa Trump ulivyohadaa utawala wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia ili kuandaa njia ya mashambulizi ya kijeshi ya Kiyahudi kwenye vituo vya nyuklia. Trump amesema katika mahojiano mingi na vyombo vya habari nyuma kuhusu mtazamo wake kuhusu silaha za nyuklia za Pakistan kama tishio, hasa kutokana na maumbile yao ya Kiislamu. Aliyekuwa Naibu Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jon Finer alitangaza katika taasisi kuu utafiti ya Amerika mnamo Oktoba 2024 kwamba mfumo wa makombora wa masafa marefu wa Pakistan unaleta tishio kwa Marekani.
Kutokana na hayo, taasisi za Marekani na mashirika ya kijasusi yanaendelea kuiona Pakistan kama tishio. Tumeona jinsi utawala wa Trump ulivyotoa msaada wa kidiplomasia kwa shambulizi la India dhidi ya Pakistan mnamo Mei 2025 na kushinikiza watawala watiifu wa Pakistan kujizuia mbele ya uchokozi wa Modi. Lau si kwa ujasiri wa simba wetu na mwewe katika vikosi vya jeshi – ambao walimlazimisha Modi na Trump kushindwa – matokeo yangekuwa mabaya.
Enyi maafisa katika jeshi la Pakistan! Ulimwengu wa Kiislamu unapita katika hatua muhimu ya mabadiliko siku hizi. Hali ya joto katika barabara ya Waislamu imefikia kilele chake kutokana na mauaji ya halaiki ya Kiyahudi yanayoungwa mkono na Marekani mjini Gaza, na kufanya kuwa ni lazima kuunganisha ardhi za Waislamu chini ya Khilafah Rashida. Kikwazo pekee kwa hili ni kusita kwenu kuangusha viti vya watawala vibaraka wa Trump na kutoa nusrah kwa Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah. Leo fursa ya kusimamisha Khilafah iko mikononi mwenu—musiiache ikaponyoka, musije mukajuta kuikosa na mukapoteza heshima ya dunia hii na neema ya Akhera:
[اسْتَجِيبُوا لِرَبِّكُمْ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَ يَوْمٌ لَا مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللَّهِ مَا لَكُمْ مِنْ مَلْجَإٍ يَوْمَئِذٍ وَمَا لَكُمْ مِنْ نَكِيرٍ]
“Muitikieni Mola wenu Mlezi kabla haijafika siku isiyo epukika itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo hamtakuwa pa kukimbilia wala hamtakuwa na cha kukingia.” [Surah Ash-Shuraa 42:47].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |