Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  11 Safar 1447 Na: 03 / 1447
M.  Jumanne, 05 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kashmir Haiwezi Kukombolewa Bila Kubadilisha Uongozi Unaopoteza Fursa ya Dhahabu ya Kuikomboa Kashmir, kwa ajili ya Kumfurahisha Trump

(Imetafsiriwa)

Leo, tarehe 5 Agosti 2025, miaka sita imepita tangu kuunganishwa kwa lazima kwa Kashmir Inayokaliwa kimabavu na Raja Dahir wa zama hizi, Modi. Kulingana na makubaliano yaliyofikiwa nchini Marekani, kuisalimisha Kashmir ilikuwa ni usaliti wa wazi wa uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan wa wakati huo, serikali ya Bajwa-Imran. Miezi michache tu baadaye, Jenerali Bajwa aliendeleza usaliti huu kwa kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano, na Dola ya Kibaniani kuhusiana na Kashmir. Hata hivyo, usaliti huu dhidi ya Waislamu wanaodhulumiwa na wanyonge wa Kashmir uliendelea hata zaidi ya hapo.

Mnamo tarehe 6 Mei 2025, katika kukabiliana na vita vilivyo lazimishwa na Dola ya Kibaniani nchini Pakistan, mwewe wa Jeshi la Anga la Pakistan waliidhalilisha India. Sio tu kwamba waliangusha karibu nusu dazeni ya ndege za kisasa za kivita za Dola ya Kibaniani, pia walipata udhibiti kamili wa anga dhidi ya Mabaniani waoga. Matokeo yake, baada ya kungoja kwa muda mrefu, fursa ya dhahabu iliibuka ya kuirudisha Kashmir, chini ya kifuniko cha anga cha Jeshi la Anga la Pakistan, ili uunganishaji wa Modi wa upande mmoja uzikwe huko Srinagar. Walakini, badala ya kuchukua fursa hii kama waumini wa kweli, uongozi wa kijeshi na kisiasa wa Pakistan ulitoa umuhimu zaidi katika kumfurahisha Trump na, kwa maagizo yake, waliamua kusitisha mapigano. Hivyo, kama walivyowatelekeza Waislamu wa Gaza, pia waliwaacha Waislamu wanaodhulumiwa wa Kashmir peke yao wakabiliane na uvamizi na udhalimu wa Kibaniani.

Ingawa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يُسْلِمُهُ» “Muislamu ni ndugu ya Muislamu mwengine, hamdhulumu wala hamkabidhi (kwa adui).” [Bukhari na Muslim]. Hata kurudi kwa mito sita kutoka Dola ya Kibanainai, au kuregeshwa kwa Mkataba wa Maji wa Indus hayakuhakikishwa. Badala yake, mapatano yale yale ya khiyana ya kusitisha mapigano yalidumishwa, ambayo sasa yanaonekana kuwa doa kwenye nyuso za watawala hawa!

Enyi Maafisa Wanyoofu na Wanajeshi katika Vikosi vya Wanajeshi vya Pakistan! Uongozi wenu wa kijeshi na kisiasa umeifanya furaha ya Trump kuwa lengo lao la maisha, lakini hawako tayari kukuhamasisheni kuwasaidia Waislamu. Wanashughulika kumteua Trump kwa Tuzo la Nobel, na kumpa Nishan-e-Imtiaz kamanda wa CENTCOM, Jenerali Kurilla, mpangaji wa kijeshi wa vita dhidi ya Gaza. Uongozi wenu ulichukua sifa kwa ushujaa wa mwewe wa Jeshi la Anga la Pakistan na kujipandisha vyeo, hadi kufikia cheo cha Field Marshal. Hata hivyo, hakuna medali na vyeo hivi vilivyowanufaisha Waislamu wa Gaza au Kashmir. Kwa uhalisia, juhudi zao zote zinafanana na kazi ya mjumbe wa kutumainiwa wa Trump, aliye kwenda nchi hadi nchi kufungua njia ya suluhisho la Kizayuni la dola mbili.

Kashmir kamwe haitakombolewa chini ya uongozi huu kwa sababu hawana ujasiri wa kuvuka laini zilizochorwa na mfumo wa kimataifa na Trump. Kashmir kamwe haitakombolewa na chochote kando na Jihad na Vikosi vya Wanajeshi vya Pakistan. Kashmir itaachiliwa huru tu na uongozi ambao, huku ukiinua bendera ya Tawhid, unawaachilia askari wenye nyoyo za simba wa Jeshi la Pakistan, na, badala ya kumwamini Trump, wanaweka imani kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kuvunja minyororo ya mfumo huu wa kimataifa.

Hizb ut Tahrir inakulinganieni kwenye kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itang'oa uvamizi usizo halali wa Mayahudi na Mabaniani juu ya Gaza na Kashmir. Kwa hiyo, jitokezeni na mumpe Ba’yah ya Nusrah (msaada wa kijeshi) Amiri wa Hizb ut Tahrir na mtawala wa kimataifa, Aalim mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa ajili ya kusimamisha Khilafah, na timizeni faradhi ya Shariah uliyowekwa juu yenu na Mwenyezi Mungu (swt).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.