Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  24 Dhu al-Hijjah 1446 Na: 46 / 1446
M.  Ijumaa, 20 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kati ya Usaliti wa Palestina na Kashmir na Utumwa kwa Amerika
Asim Munir Anafanya Nini Mbele ya Firauni Wa Zama Zetu, Trump?
(Imetafsiriwa)

Katika wakati ambapo Amerika inapigana vita dhidi ya jirani Muislamu, Iran, kwa kutumia mkono wake mchafu katika eneo hilo, umbile la Kiyahudi, Rais wa Marekani, Donald Trump, alimkaribisha Mkuu wa Majeshi wa Pakistan mnamo Jumatano, 18 Juni 2025, kwa chakula cha mchana katika mkutano ambao haujawahi kushuhudiwa katika Ikulu ya White House. Kinachotia shaka kuhusu mkutano huu, na muda wake, ni kwamba ni mara ya kwanza kwa rais wa Marekani kumkaribisha mkuu wa jeshi la Pakistan katika Ikulu ya White House, bila ya kuwepo kwa afisa yeyote mkuu wa kiraia wa Pakistan, kuashiria umuhimu wa mkutano huo, na unyeti wa mada yake.

Katika kuonyesha ima kutojua, au kupuuza kwa makusudi ukweli kwamba Amerika ndiyo inayoongoza vita dhidi ya Iran, maafisa na wataalamu wa Pakistan walidai kwamba Asim Munir anatarajiwa kumshinikiza Trump asiingie vitani pamoja na "Israel" dhidi ya Iran, na kushinikiza kusitishwa kwa mapigano, licha ya ukweli kwamba ubalozi wa Pakistan jijini Washington tayari ulitetea maslahi ya Iran nchini Marekani! Kwa hivyo, je, Asim Munir alienda Washington ili kukomesha vita? Je, kweli anaweza kufanya hivyo? Na je, kamwe yuko katika nafasi ambayo Trump angemruhusu kufanya ombi kama hilo?

Inasemwa katika methali ya Kiarabu, التذاكي على الأذكياء ضرب من الغباء “Kujaribu kuwapiku wenye hekima ni aina ya upumbavu.” Ukweli ni kwamba Trump anajiona kuwa Firauni wa zama hizi. Trump havumilii hata ushauri, au maombi, kutoka kwa kibaraka wake yeyote. Ama kuhusu ukweli kwamba Marekani imeyalinda maslahi yake, miongoni mwao ikihakikisha utawala wa umbile la Kiyahudi katika eneo hilo, ni wazi sana kwamba haihitaji maelezo zaidi. Haya ni maslahi ambayo Amerika inayaona kuwa "muhimu na ya kimkakati," na haikubali upatanishi, au maridhiano hata kidogo, juu yake. Kwa hivyo hakuna haja ya vinywa vya serikali nchini Pakistan kupandisha hadhi ya Asim Munir, wakimuonyesha akiwa ndani ya hadhi asiyo nayo, wala kustahili.

Ilionekana kuwa Amerika ilikuwa imepatanisha usitishaji wa mapigano ili kuzuia kutokwa na damu kwa India mwezi uliopita, baada ya kupata hasara kubwa mikononi mwa mwewe na simba wa jeshi la Pakistan, huku Trump akidai kuwa majirani hao wawili wa nyuklia huko Asia Kusini walikuwa wamekubali kusitisha mapigano, kupitia upatanishi wa Amerika. Walakini, Waziri wa Mambo ya nje wa India, Vikram Misri, alifichua ukweli, akisema kwamba Modi alimweleza Trump mnamo Jumanne jioni kwamba usitishaji wa mapigano kati ya India na Pakistan, kufuatia mzozo wa siku nne mnamo Mei, ulifikiwa kupitia mazungumzo ya moja kwa moja kati ya majeshi hayo mawili, sio kupitia upatanishi wa Amerika. Hasa, Pakistan haikukataa taarifa ya Misri. Hili linathibitisha kwamba uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan ulitapanya ushindi uliopatikana na askari shupavu wa jeshi, ima kupitia upatanishi wa Marekani, au uwezekano mkubwa zaidi kupitia utiifu wao wenyewe wa moja kwa moja, na usaliti wa wazi, kwa kufanya mazungumzo na adui mkuu, India! Kwa hiyo je, kuna mtu yeyote mwenye akili timamu anayeamini kwamba Asim Munir alikwenda Washington kutafuta kukomesha uchokozi dhidi ya Iran, huku yeye mwenyewe akiharibu ushindi wa Pakistan dhidi ya India?

Vinywa vya utawala huu, wale wanaojiita "maafisa na wataalamu" nchini Pakistan, lazima wajihadhari kwamba ziara ya Asim Munir kwa Trump si chochote zaidi ya jaribio la kusaidia Amerika katika kuangusha utawala wa Iran, jambo la kusikitisha jinsi itakavyokuwa, kama ambavyo uongozi wa Pakistan ulifanya hapo awali nchini Afghanistan na Iraq. Ni utiifu ule ule wa kipofu ulioonyeshwa kwa Amerika katika suala la Kashmir, kwa kukubali kushindwa na India, mshirika wa Amerika, na kutochukua hatua kwao kikamilifu juu ya uhalifu uliofanywa na Amerika na umbile la Kiyahudi katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Kinachopaswa kuogopwa ni kwamba ziara hii inaweza kuwa hatua katika njama mbaya ya kusambaratisha, au kuharibu, mpango wa silaha za nyuklia wa Pakistan, ambao unaweza kuwa shabaha inayofuata mara tu mradi wa nyuklia wa Iran utakaposhughulikiwa.

Enyi maafisa waaminifu katika jeshi la Pakistani! Enyi Waislamu nchini Pakistan! Uongozi wenu, ambao ulipoteza ushindi huko Kashmir, hauwezi kuaminiwa, kwa hivyo jihadharini nao. Fahamuni kabisa kwamba mkutano wa Asim Munir na Trump si chochote ila ni kikao cha kupokea amri na maelekezo kutoka kwa mkuu wa makafiri Amerika. Basi jihadharini nao. Na kumbukeni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu,

[وَلَا تُؤْمِنُوا إِلَّا لِمَنْ تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ الْهُدَىٰ هُدَى اللَّهِ]

“Wala msimuamini ila anaye fuata dini yenu. Sema: Hakika uwongofu ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu.” [Surah Aali Imran 3:73].

Jueni kwamba njia ya wokovu wenu, na ukombozi wa Ummah mzima, upo katika kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Basi fanyeni kazi na Hizb ut Tahrir na muipe nusrah (msaada) katika kusimamisha Khilafah kabla ya kuchelewa. Zamu ya Pakistan hakika inakuja mara tu Amerika na umbile la Kiyahudi zitakapomaliza faili la Iran, ili umbile la Kiyahudi liweze kutawazwa kama bwana wa kanda upande wa Magharibi, pamoja na India katika upande wa Mashariki. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[فَسَتَذْكُرُونَ مَا أَقُولُ لَكُمْ وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ]

“Basi mtayakumbuka ninayo kuambieni. Nami namkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu. Hakika Mwenyezi Mungu anawaona waja wake.” [Surah Ghafir 40:44].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.