Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  7 Jumada II 1447 Na: H.T.L 1447 / 13
M.  Ijumaa, 28 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kauli za Patriarch Bechara Al-Rahi Kuhusu Wakristo katika Eneo Hili Mshikamano wa Kudumu kwa Fahamu ya Marekani na Kimagharibi ya “Walio wachache”, iliyo ngeni kwa Watu wa Eneo Hili na Historia Yao!
(Imetafsiriwa)

Katika mahojiano yake na chaneli ya Lebanon Al-Jadeed katika kipindi cha “Huyu ni Mimi” na mwandishi wa habari Samar Abu Khaleel, kauli za Patriarch Bechara Al-Rahi zinaambatana na ziara ya Papa Leo XIV katika eneo hili, ikiwa ni pamoja na Lebanon, hasa kuhusu suala la kubadilisha utawala wa Syria na kauli yake: “Wakristo wanaondoka Syria leo kwa sababu dola iliyopo ni dola ya Kiislamu! Ingawa haikuwa hivyo wakati wa utawala uliopita...” Na msimamo huu ni uthibitisho wa msimamo uliopita wa Patriarch mwenyewe; ambapo alisema mwaka wa 2011 wakati wa ziara yake nchini Ufaransa chini ya Sarkozy: “Kukiri kwamba makosa na ukiukwaji wa sheria uliotokea nchini Syria hakubatilishi ukweli kwamba Rais Bashar Al-Assad alikuwa ameanza mageuzi, na angepaswa kupewa nafasi”! Mtazamo wake kuhusu Mapinduzi ya Kiarabu ulikuwa kwamba ni: “tukio na maendeleo yanayotia wasiwasi zaidi kuliko faraja, kwa sababu si lazima iwe ni kuingia kwa enzi ya demokrasia na uhuru bali ni katika enzi ya msimamo mkali na tawala ngumu zaidi ambazo haziheshimu uhuru, demokrasia, wala haki za (walio wachache)”! Kwa hivyo je, msimamo huu wa Patriarch ni msimamo wa mapema wa kuimarisha ziara ya Papa katika mwelekeo wa kile kinachoitwa ulinzi wa (walio wachache), au kuimarisha hofu isiyo na msingi ya Uislamu — “Chuki dhid ya Uislamu” — na hofu ya kusimamishwa kwa dola ya Kiislamu katika eneo hili?!

Na sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon tunaelekeza risala zifuatazo:

Kwanza: Kinachotuhusu mwanzoni ni kuthibitisha kwamba katika Uislamu na ndani ya dola yake halisi ambayo itainuka hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume — hakuna kuwepo kwa kile kinachoitwa (walio wachache), sio kama fahamu wala kama uhalisia, kwa maana iliyoelekezwa na Patriarch au wale walioathiriwa na fikra ya Kimagharibi. Bali, yale yaliyokuwepo ndani ya dola ya kwanza ya Kiislamu kutoka miongoni mwa wasiokuwa Waislamu, tangu Mtume (saw) alipoisimamisha hadi Khilafah ilipovunjwa mwaka 1924, ni kwamba walikuwa chini ya ulinzi wa Dola, katika uangalizi wake, maagano, dhamana na mkataba wake – kauli mbiu ya hadhi yao ndani yake ikiwa ni kauli ya Mtume (saw):

«مَن ظَلَم مُعاهَداً أو تَنَقَّصَه حقَّه وكَلَّفَه فوقَ طاقتِه أو أخَذ منه شيئاً بغيرِ طِيبِ نفْسٍ فأنا خَصمُه يومَ القيامةِ» “Mwenye kumdhulumu aliye fungwa ahadi naye, au akampunguzia haki yake, au akamtwika zaidi ya uwezo wake, au akamnyang’anya chochote bila ya ridhaa yake, basi mimi ni mpinzani wake Siku ya Kiyama.” Na kielelezo chao kikuu katika utekelezaji ni kile kilichojulikana kama Agano la Omar katika mwaka wa 15 H / 638 M, ambapo Khalifa Ar-Rashid Omar ibn Al-Khattab — Mwenyezi Mungu awe radhi naye — aliwapa usalama juu ya makanisa yao na mali zao. Agano la Omar lilizingatiwa kuwa moja ya hati muhimu zaidi katika historia ya Jerusalem. Na tunamregesha Patriarch na wale wanaobeba maoni sawa kwa maneno ya mwandishi Gustave Le Bon, ambaye alielezea kuingia kwa Omar ibn Al-Khattab — Mwenyezi Mungu awe radhi naye — ndani ya Jerusalem: “Mwenendo wa Kamanda wa Waumini Omar ibn Al-Khattab katika mji wa Jerusalem unatufunulia upole mkubwa ambao washindi wa Kiarabu waliwatendea watu walioshindwa — muamala unaogongana kabisa na kile ambacho Makruseda walifanya baadaye huko Jerusalem karne nyingi baadaye. Omar hakutaka kuingia mjini na zaidi ya kundi dogo la maswahaba wake, na alimwomba Patriarch Sophronius aandamane naye katika kutembelea maeneo yote matakatifu. Aliwapa wakaazi usalama, akaapa kuheshimu makanisa yao na mali zao, na akawakataza Waislamu kufanya ibada katika maeneo yao matakatifu.”

Kisha anaendelea: “Na mwenendo wa Amr ibn Al-As nchini Misri haukuwa wa upole kidogo; kwani aliwapa Wamisri uhuru kamili wa kidini, haki kamili, heshima ya mali, na jizyah ya kila mwaka isiyozidi franc kumi na tano kwa kila mtu — badala ya kodi nzito za watawala wa Byzantino. Kwa hivyo Wamisri walikubali kwa khiyari na shukrani chini ya masharti haya.”

Pili: Nafasi hapa haitoshi kutaja historia tukufu ya Waislamu na Wakristo walioishi miongoni mwao, wala hata kuorodhesha misimamo ya waandishi na wanafikra waliokuwa waadilifu katika kuelezea jinsi Waislamu walivyoamiliana na Wakristo — kama vile Amin Maalouf na Shakib Arslan. Hata hivyo tunathibitisha kwamba mtazamo huu wa Kiislamu na mtazamo wa dola yake kuhusu Wakristo uko wazi kwa Patriarch Al-Rahi haswa — hasa baada ya ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon kumtembelea mnamo 12/1/2021 na kumpa kitabu cha kina kuhusu jambo hili. Miongoni mwa yaliyokuja hitimisho lake: “Jihadharini - tahadhari zote - kuhusu miradi inayoendeshwa na Magharibi nchini Lebanon, hasa Amerika, sasa kwa kuwa pwani za Lebanon zinaelea kwenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi - na kuifanya Lebanon kuwa kitu cha kutamaniwa katika rasilimali zake baada ya Amerika kuimaliza kisiasa na kijamii ... Na pia jihadharini na kushiriki katika ushindani wa kimataifa kuhusu Lebanon, haswa kati ya Amerika na Ufaransa, kama mwendelezo wa mzozo kuhusu utajiri mkubwa wa gesi katika Mediterania ya Mashariki ... Kwa hivyo, ni muhimu kwamba msisitizo wenu uwe juu ya kuiunganisha Lebanon na asili yake, eneo lake, na mazingira yake - na juu ya kuwaunga mkono wale wanaofanya kazi kwa dhati kuokoa Lebanon na eneo lake kutoka kwa makucha ya utegemezi wa Magharibi, iwe Magharibi hiyo ni ya Marekani, Ufaransa, au vyenginevyo." Na pia ilisema: “Na leo Lebanon inaishi katika mkondo uleule wa uchochezi ‘mpya wa zamani’ unaotokana na uingiliaji kati wa nje (Amerika-Ulaya) - na ikiwa itazalisha chochote kipya, itakuwa fomula nyingine tu inayofeli. Fomula hizi zote zinasimama juu ya sheria ya mshindi na mshindwa - na serikali hii imefunikwa na aina elfu za uzushi zinazoifanya kuwa hifadhi takatifu, huku kikiwa ni chombo kilichoshindwa kujitengenezea kitambulisho kimoja, na mfumo wake wa kisiasa ni dhaifu.”

Tatu: Amani ambayo propaganda yake inaongezeka katika siku hizi na kuongozwa na Amerika katika kampeni ya kimfumo dhidi ya Lebanon na eneo hili - haitakuwa suluhisho la matatizo ya Lebanon. Badala yake, ni kujisalimisha, uhalalishaji mahusiano, na utambuzi zaidi wa umbile nyakuzi linalokaliwa kimabavu, na udhibiti wake juu ya ardhi iliyobarikiwa ya Palestina - ikiwemo Al-Quds (Jerusalem) na Kanisa la Ufufuo (Al-Qiyamah)! Mbinu ya amani na umbile nyakuzi ni mbinu ya Kimagharibi inayotumikia maslahi ya Magharibi - si yenu - na inaimarisha uwepo wenu kama walio wachache si kama watu wa nchi, kuwa na kile walichonacho kwa haki na deni la kile wanachodaiwa kwa haki.

Kwa kumalizia — mradi ambao kwao Hizb ut Tahrir inafanya kazi ni kusimamishwa kwa Khilafah Rashida katika ardhi za Waislamu, ikiwemo Lebanon — dola ya uadilifu na uongofu kwa njia ya Utume. Hizb ut Tahrir imeiandalia rasimu yake ya katiba, iliyo na haki na wajibu wa Watu wa Kitabu katika kazi yake “Utangulizi wa Katiba au Sababu Zinazoiongoza” — sehemu zote kwa jumla, na vifungu (5, 6, na 7) chini ya Vipengee Jumla haswa. Rasimu hii ya katiba ndiyo njia ya kuiokoa Lebanon na eneo hili kutokana na mgawanyiko wa kidini na wa walio wachache — sio kushikamana na masharti, fikra, na sera za mkoloni Magharibi. Ni njia ya kumfukuza mkaliaji wa kimabavu anayebeba uzito juu ya ardhi na watu — sio kusalim amri na kuhalalisha mahusiano. Kushikamana na Magharibi, haswa Amerika, na mradi wake ni kukubali ukoloni wake wa eneo hili na kukubali istilahi zake potofu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[لا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ * إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]

“Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Mumtahanah:8-9].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.