Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  9 Rabi' II 1447 Na: H.T.L 1447 / 08
M.  Jumatano, 01 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Lebanon Atoa Wito wa Kuidhinishwa Haraka kwa Mpango wa Trump wa Gaza!
(Imetafsiriwa)

Enyi Watu wa Lebanon, Enyi Watu wa Palestina, Enyi Umma wa Uislamu: Rais wa Lebanon alitoa wito wa kuidhinishwa haraka kwa mpango wa Trump wa kusimamisha vita mjini Gaza, akijua kwamba ni mpango wa kufikia maslahi ya umbile la Kiyahudi, ambalo limeshindwa kulazimisha kupitia nguvu ya silaha, kama vile kujisalimisha kwa mujahidina, kuachiliwa huru kwa wafungwa wa Kiyahudi na malengo mengine. Ili kufikia malengo haya kwa umbile halifu kupitia ujanja wa Trump.

Imedhihirika wazi kuwa Trump, muungaji mkono mkuu wa umbile la Kiyahudi katika jinai zake za kutisha huko Gaza na Palestina yote, anatoa suluhisho la hasara kwa Gaza. Analilazimisha hata kwa kundi la watawala katika nchi za Kiislamu, na anawasaidia watawala hawa, ambao wengi wao wamekimbilia kuliunga mkono kana kwamba damu ya makumi ya maelfu ya mashahidi, mamia ya maelfu ya waliojeruhiwa na waliokimbia makaazi yao, na uharibifu wa Gaza, miji na vijiji vyake - nyumba, hospitali, shule, na hata misikiti si lolote ikilinganishwa na amri za Ikulu ya White House. Ni kana kwamba yule aliye nyuma ya mhalifu muuaji amekuwa ndiye mtawala!

Wito wa kukubali haraka mpango huu muovu, ambao Mayahudi walishiriki katika kila kipengee, hauonyeshi chochote ila kujisalimisha kidhalilifu kwa mfumo wa kikoloni wa Marekani na kujihusisha upya katika njia ya kuhalalisha mahusiano ya kisiasa ambayo inakusudiwa kulazimishwa kwa Ummah, kama ilivyokusudiwa hapo awali kupitia mikataba ya kisaliti ya Camp David, Oslo, na Wadi Araba.

Uamuzi wa Trump wa kusitisha vita sio huruma kwa watu wa Gaza. Badala yake, inaimarisha umbile la Kiyahudi na kuruhusu mashini ya mauaji kupata afueni yake baada ya kukanyagwa chini na makombora ya mujahidina. Inadhihirisha udhaifu wa jeshi linalokalia kimabavu, ambalo halijaweza kuvunja nia ya watu mashujaa wa Gaza, kufufua kadhia ya Palestina kama kadhia hai ya Kiislamu, na kuileta karibu na kusafishwa na uchafu wa Mayahudi.

Enyi Watu wa Lebanon: Kana kwamba watawala wa Lebanon hawajajifunza kutokana na hila, khiyana, usaliti, na ukaidi wa umbile la Kiyahudi, ukiukaji wake wa makubaliano yote, na kuendelea kulipua na kuwaua watu wa Lebanon, rais wake anawezaje kupigia debe mpango huu wa dhambi na hali anajua kwamba Mayahudi hawatautekeleza, ikiwemo kusimamisha vita vyao dhidi ya Waislamu, na kwamba uamuzi wowote na kwamba Trump hatalazimisha uamuzi wowote juu yao?

Ni hakika kwamba watawala wa nchi hii hutenda tu kwa mujibu wa amri za balozi za Magharibi, na hawaheshimu damu ya watu wao au utakatifu wa maeneo yako matakatifu. Kama vile watawala wote wa Waislamu, wako upande wa maadui zao kwa gharama ya nchi na watu wao. Hujaona jinsi baadhi yao walivyoshirikiana katika kuizingira Gaza, na leo wanakimbilia kuidhinisha amri za Trump? Kwa kweli hili linashangaza na linachukiza! La kustaajabisha zaidi ni kutoweza kwa Waislamu kupindua viti vyao vya enzi na kuwatupa kwenye shimo refu.

Enyi Waislamu: Kitakachositisha vita vya Mayahudi ni majeshi yenu, ikiwa yatakusanyika kunusuru dini yao, kuikomboa ardhi hiyo, na kulinda heshima yao, sio maazimio ya Baraza la Usalama, wala mipango ya Trump, wafuasi wake, na wahalifu wengine.

Wajibu wa leo ni kuondoa tawala hizi za vibaraka, kuvunja mipaka iliyochorwa na makafiri, wakoloni wa Magharibi baina ya ardhi za Waislamu, na kutaka haraka kuhamasishwa kwa majeshi kuelekea ukombozi wa Palestina yote. Wala sio kukarabati uvamizi kwa masuluhisho ya kivipande au kufikia suluhisho kwa gharama ya damu ya mashahidi kwenye meza ya maadui wa Mwenyezi Mungu.

Enyi Waislamu: Wakati umewadia wa kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hiyo peke yake ndio itakayokuunganisheni, kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa, na kuondoa ushawishi wa Amerika na Magharibi katika ardhi zetu.

[وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّهِ]

Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” [Al-Anfal 8:39]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.