Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  2 Rabi' II 1447 Na: H.T.L 1447 / 07
M.  Jumatano, 24 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kujibu Matamshi ya Mjumbe wa Marekani Tom Barrack

(Imetafsiriwa)

Kwa mara nyingine tena utawala wa Marekani unaonyesha sura yake halisi kupitia taarifa za mjumbe wake Tom Barrack, katika mahojiano yake yaliyotangazwa na Sky News na mtangazaji mkuu wa IMI International Hadley Gamble, ambaye alijiruhusu kuingilia waziwazi katika masuala ya Lebanon na kubainisha sifa za dori za taasisi ya Jeshi.

Sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon, na mbele ya mazungumzo haya ya kiburi, tunasisitiza kwamba Lebanon sio koloni la Marekani, na Magharibi kwa jumla na Marekani hasa hawana haki ya kuwa walinzi juu yake, na kwamba kufafanua kazi za Jeshi na kuligeuza kulinda mipaka ya umbile la Kiyahudi na kulifanya kuwa ala mikononi mwa dola za kigeni hakutatokea,  kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Mazungumzo ya Barrack kuhusu kuzuia kulipa silaha Jeshi ili lisipigane na umbile la Kiyahudi, na kuridhika na kulifanya kuwa ni nguvu ya kulinda ndani, ni tusi kwa Lebanon na taasisi ya jeshi, na dhihirisho wazi la mradi unaolenga kudhoofisha Jeshi na kuainisha kazi zake kulingana na maslahi ya Magharibi na umbile la Kiyahudi.

Wanasiasa wenye busara nchini Lebanon lazima watambue kwamba asili ya uhusiano kati ya umbile la Kiyahudi na Amerika ni sehemu ya mwili mzima, kufikia malengo ya kimkakati kwa ajili yake, na ni mradi wa kiutendaji uliowekwa na nchi za Magharibi katika moyo wa Umma wa Kiislamu kutekeleza dori maalum: kugawanya eneo hili, kushambulia mwamko wake, na kuwabakisha watu wake katika mizozo endelevu.

Usaidizi wa Marekani kwa Lebanon ni kama chembe chembe tu, wakati usaidizi wa kweli kwa umbile hilo nyakuzi ni mamlaka ya wazi ya kufanya uvamizi bila kikomo, kuanzia kwa ukaliaji kimabavu, uhamishaji na mauaji hadi vita vilivyopangiliwa huko Gaza, Lebanon na Syria na ardhi zengine za Waislamu.

Ukweli ni kwamba tabia ya hivi sasa ya Mayahudi katika eneo hilo haingetokea bila kinga ya Marekani inayowalinda, kufadhili maghala yao ya silaha, na kuwapa “uhalali wa kimataifa.”

Uadui hapa sio tu “mzozo wa ndani,” lakini dhihirisho la utasho wa Amerika ambayo inaona uwepo wa umbile hili kama mstari mwekundu, ambao unachangia kimsingi kudhoofisha Waislamu na kupora rasilimali zao.

Kwa hiyo mjumbe huyo wa Marekani yuko kwenye misheni chafu na wenye busara lazima wakomeshe uingiliaji kati wa mambo ya Lebanon, na wasiruhusu mtu yeyote kuamua majukumu ya taasisi za serikali, na hawapaswi kutarajia kheri kutoka kwa Amerika na mjumbe wake, na wanapaswa kutambua kwamba maneno yaliyosemwa na wajumbe wa Amerika kwa wanasiasa nchini Lebanon ni udanganyifu, ucheleweshaji na hila ambazo hutumikia maslahi ya Marekani ambayo haina uhusiano wa ikhlasi kwa yeyote isipokuwa maslahi yao wenyewe kama dola ya kivitendo ya kibepari ambayo msingi wake ni kutenganisha dini na maisha, na chombo chake katika hilo ni ukoloni katika aina zake mbalimbali za zamani na mpya.

Kwa hivyo mtazamo wa Amerika na mjumbe wake lazima usiwe kwamba ni dola ya upatanishi isiyoegemea upande wowote, bali ni dola inayounga mkono umbile angamizi la unyakuzi.

[الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا]

“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [Surat An-Nisa: 139].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.