Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
H. 15 Muharram 1447 | Na: H.T.L 1447 / 01 |
M. Alhamisi, 10 Julai 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ziara za Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon kwa Wabunge
(Imetafsiriwa)
Ujumbe kutoka Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Lebanon, unaojumuisha Dkt Muhammad Jaber na Mhandisi Saleh Salam, kama sehemu ya kampeni ya kuwatembelea wabunge, walimtembelea Mbunge Dkt. Imad Al-Hout jijini Beirut kwa takriban saa moja. Katika ziara hiyo, ujumbe huo ulisisitiza mambo yafuatayo, ambayo yanahitaji misimamo na hatua za wabunge katika bunge la Lebanon:
1. Umuhimu wa kukabiliana na mradi wa kulitambua rasmi umbile la Kiyahudi, ambalo matayarisho yake yanaongezeka kwa kasi miongoni mwa wanasiasa na vyombo vya habari kwa kisingizio cha mashinikizo ya Marekani inayotaka kuhalalishwa kwa mahusiano nalo.
2. Kwamba majeshi lazima yatimize wajibu wao wa Shariah kwa kutumia silaha dhidi ya adui wa Ummah, Mayahudi; na kwamba makamanda wa majeshi haya lazima wajue kwamba wasipofanya hivyo, silaha zao ima zitaondolewa kutoka kwao au zitaangamizwa, kwa ushirikiano na serikali zao tawala ambazo zimefungamana na Magharibi na zinazolinda umbile hilo.
3. Kila mtu lazima ajiepushe na fitna za kimadhehebu na chochote kinachochochea au kuwasha moto wake miongoni mwa Waislamu, kwa sababu jambo hili linamtumikia adui tu na linawagawanya Waislamu wanaopaswa kuunganishwa chini ya dola moja, Dola ya Khilafah, licha ya tofauti zao za kifiqhi na ijtihadi zao za kisiasa.
4. Umuhimu wa kutangaza kwa waziwazi mradi wa kina wa Dola ya Kiislamu ambao tunaubeba, yaani mradi wa Khilafah, pamoja na watu wote, bungeni, katika kila mkutano wa kisiasa, na kila mara, na kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu, kama vile Hizb ut Tahrir inavyofanya bila ya kusitasita, bali kwa furaha, tukiwa na yakini kwamba huu ndio ukombozi wetu na wengine kutokana na hali hii ngumu.
Mwishoni mwa ziara hiyo, ilikubaliwa kudumisha mawasiliano endelevu kwa yale yenye kheri kwa Ummah huu.
Ujumbe huo huo pia wiki iliyopita ulimtembelea Mbunge Nabil Badr jijini Beirut kujadili masuala hayo hayo, kuwaweka wabunge wa watu wa Lebanon mbele ya majukumu yao, hasa katika kupendekeza suluhisho msingi na kuwawajibisha watawala.
Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon itaendelea na mawasiliano yake na Wabunge kuwasilisha mradi wake wa suluhisho katika siku zijazo, InshaAllah Subhanahu wa Ta’ala.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |