Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  27 Rabi' I 1447 Na: H 1447 / 011
M.  Ijumaa, 19 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Turkestan Mashariki: Machafuko ya Kuangamiza Watu Wote
(Imetafsiriwa)

Huko Turkestan Mashariki, kina mama wanakamatwa, watoto wanatenganishwa na familia zao, na wasichana wenye umri mdogo wanafungwa kizazi... Katika Turkestan Mashariki, kundi la watu linachinjwa na kuangamizwa kimya kimya (Shirika la Habari la Turkestan Mashariki, 12/9/2025)

Juhudi za kihalifu za serikali ya China huko Turkestan Mashariki (eneo la Uighur) za kufuta kitambulisho cha watu wake Waislamu hazifichiki tena kwa mtu yeyote. Inawakandamiza na kuwatiisha wanawake, inawazuia kuvaa mavazi yao ya Kiislamu na kuswali. Inawatenganisha watoto na familia zao ili kuwabadilisha fikra, kuwafunza thaqafa yake ya upagani, na kuwakengeusha na Uislamu. Pia inawafunga kizazi wasichana wa umri mdogo ili kuwazuia kuzalisha kizazi kipya cha Waislamu.

Kile China inachofanya huko Turkestan Mashariki ni vita hatari zaidi kuliko vita vya Mayahudi huko Gaza; vita vya mauaji ya halaiki vinavyodhihirisha chuki kubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu, vita vinavyoendeshwa na maadui wa Uislamu kila mahali.

Vita vya China huko Turkestan Mashariki ni vita vya kimya kimya, vinavyotaka kuangamiza watu, kufuta kitambulisho chao, kuwang'oa, na kuwageuza kutoka kwa Dini yao hadi waingizwe katika thaqafa yake ya kikomunisti. Ama kuhusu vita vya umbile la Kiyahudi, vinatangazwa kwa silaha na njaa, vinavyofanywa na umbile hilo nyakuzi na washirika wake ili kuangamiza nasaba ya watu wa Gaza, kukalia kimabavu ardhi yao, na kutimiza ndoto kubwa wanayopanga.

Vita hivi vinavyofanywa na madhalimu si chochote ila ni vita vya maangamizi, lengo lake ni kuondoa kila kitu kinachohusiana na Uislamu na Waislamu na kusimamisha hadhara ya kikafiri ya madhalimu. Wakisaidiana wao kwa wao, wanamwaga heshima na damu, wanakiuka matukufu, na kunyakua ardhi zao.

Mbele ya dhulma na ukandamizaji huu wote, tunawakuta watu wa Gaza wakiwa imara na thabiti, wakitoa funzo kwa ulimwengu katika kujitolea mhanga na ustahamilivu katika kulinda ardhi yao. Tunawakuta Waislamu wa Uyghur wakiwa imara, wamesimama wima mithili ya mizizi ya ardhi ambayo hakuna joka linaloweza kuing'oa.

Licha ya dhuluma, ukandamizaji na ukiukwaji unaofanyiwa watu wa Turkestan, ambao unadhihirisha uhalifu wa kikatili na vita vya maangamizi, wanapinga kimya kimya ukandamizaji wa mamlaka za China na kulazimishwa kwao kuikana Dini yao kwa njia ya vitisho.

China imeanzisha kambi nyingi za kumuweka kizuizini kila Muislamu, kuwatesa, na kuwalazimisha kuacha Dini yao na kuritadi. Kambi hizi zinatumika kuwabadilisha fikra na kuwafunza thaqafa yake ya kikomunisti ya kipagani, na kuficha kwa makusudi vitendo vyake vya ukandamizaji na sera za kikatili zinazolenga kuwaangamiza watu wote. Licha ya hayo, uvundo wa vitendo vyake vya kutisha umejulikana vyema. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilikariri katika Ripoti yake ya Mwaka 2024 kuhusu Hali ya Haki za Kibinadamu, iliyotolewa Agosti 12, kwamba China inaendelea kufanya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu huko Turkestan Mashariki. Ili kuficha uozo wa sera na uhalifu wake, China inafanya vikao kama vile “Jukwaa la Maendeleo ya Haki za Binadamu huko Xinjiang” ambapo inalenga kuficha ukweli wa matendo yake. Mada zote zilizotolewa zilikuwa ni jaribio la kuhalalisha jinai zake dhidi ya haki za binadamu katika Turkestan Mashariki na kuipamba sura yake chafu mbele ya walimwengu kupitia hafla za kirongo zenye lengo la kuficha uhalisia wa kidhalimu, kuficha ukweli, na kuficha ukiukaji unaofanya dhidi ya Waislamu wa Uyghur.

Kwa miaka kadhaa, China imeendelea kuandaa maonyesho ya urithi wa kitamaduni usioonekana kama sehemu ya sera yake ya kupendezesha ukaliaji wake wa Turkestan Mashariki na kukuza sera ya kuanzishwa kwa utaifa, ambayo ni moja ya nguzo za uhalifu wake wa mauaji ya halaiki. Kupitia maonyesho haya, propaganda za China zinalenga kukuza wazo kwamba urithi wa watu asilia wa Turkestan Mashariki, kama vile Wauyghur, Wakazakh, na Wakyrgyz, ni sehemu ya utamaduni wa China au uliundwa chini ya ushawishi wake.

Enyi Ummah wa Kiislamu: Mko wapi kuhusiana na yanayowapata wana wenu wa kiume na wa kike huko Turkestan Mashariki? Kwa nini udhalilifu na kimya hiki? Wana na binti zenu wanapinga licha ya ukatili na uonevu wanaoukabili. Wanapigana kwa imani imara na thabiti, na wanabaki na fahari licha ya kudhalilishwa na mamlaka za China. Kwa hiyo, munasubiri nini kuwanusuru?!

Makafiri hawa madhalimu wanaupiga vita Uislamu, uliomo ndani ya Wauyghur, wakitaka kuutokomeza na kuuondoa kwenye nyoyo zao. Lakini wanabaki imara na kutafuta msaada kutoka kwa ndugu na dada zao katika Dini. Mtafanya nini enyi Waislamu?

Enyi Wanazuoni wa Kiislamu: Ndugu zenu wa Turkestan wanauawa ili Uislamu usichukuliwe kutoka kwao. Hao ndio wanavyuoni wanaoeneza na kubainisha hukmu zake. Lakini China inataka kuwanyamazisha. Muko wapi kuhusu kueneza ujumbe wenu? Je, mumezungumza kuhusu vita hivi ambavyo China inavifanya kimya kimya dhidi ya Waislamu wa huko, kuvifichua kutoka kwenye mimbari na kuhabarisha umma kwa jumla? Je, mumetoa wito kwa majeshi ya Waislamu na kuyahimiza kuharakisha kukomesha mauaji haya ya halaiki na mauaji ya kikabila?

China ilidai kuwa inapambana na ugaidi, na kongamano la “amani” likaandaliwa chini ya kichwa “Kupambana na Ugaidi na Kudumisha Usalama wa Kimataifa katika Hali Mpya: Majukumu ya Kikanda na Kimataifa.” Imetoa wito kwa mfumo wa kimataifa kushirikiana katika kupambana na ugaidi na kuweka usalama wa kimataifa. Imedhihirika wazi maana ya “ugaidi” ni Uislamu na kila kitu kinachoashiria kuwa ni hadhara tukufu na ya kale, na kufanya kazi ya kuregesha hadhi yake na kuiregesha maishani ili kuwaongoza watu kwenye njia ya wokovu na ukombozi, na kufuta kila chembe ya hadhara hii mbovu na fisidifu ya Magharibi.

Enyi Waislamu: Sisi, Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) ashuhudie kwamba tumewalingania watu wenye nguvu na ulinzi na kutoa kilio kimoja baada ya chengine cha kuomba msaada, tukiwataka wanazuoni, majeshi na wale wote wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kisiasa kukomesha mauaji haya ya halaiki. Tumethibitisha kwamba hili litatokea tu ndani ya dola ambayo itawaunganisha Waislamu waliotawanyika na kuzuia mikono ya makafiri wahalifu.

Enyi Waislamu: Maadui zetu wanatuona kama Ummah mmoja na wanaamiliana nasi katika ardhi zote za Kiislamu kama maadui zao. Wanachukia na kuua watoto wetu na wanataka kutuangamiza sisi sote. Kwa hiyo, mutachukua hatua lini? Je, ni lini damu yenu itachemka kwenye mishipa yenu na kuwa na yakini kwamba hivi ni vita vya uwepo? Ni lini mtaelewa kuwa vita hivi ni vita kati ya hadhara mbili: hadhara yetu ya Kiislamu na hadhara yao ya Kimagharibi?

Ni lini mtatambua kwamba watu hawa hawatatosheka na kuangamizwa kwa watu wa Turkestan, wala watu wa Gaza, wala Jamhuri ya Afrika ya Kati, wala Waislamu wengine popote pale?

Suala hili ni zaidi kuliko hilo; ni vita kati ya hadhara iliyoundwa na Mjuzi wa kila kitu, Mwenye hekima, na hadhara iliyobuniwa na akili ya mwanadamu tasa ambaye alisubutu kumkaidi Muumba wake na kuweka sheria na kanuni. Ni tofauti ni kubwa kiasi gani kati ya hadhara iliyoanzishwa na Muumba wa ulimwengu, Mwenye Hekima zaidi, Mjuzi wa yote na hadhara iliyoanzishwa na mja asiye na shukrani, mwenye kudharauliwa!

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.