Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  27 Rabi' II 1447 Na: H 1447 / 14
M.  Jumapili, 19 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watu Wapendao Uislamu wa Nchi Wameukataa Mkataba wa Julai, ambao umejengwa juu ya Msingi wa Usekula na Demokrasia Batili ya Magharibi, Na Wanataka Mkataba wa Madina uliojengwa juu ya Msingi wa Imani yao Safi ya Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Mnamo 17 Oktoba 2025, kipote cha wanasiasa wenye uchu wa madaraka nchini humu walitia saini ‘Mkataba wa Julai - suluhisho la kisiasa lililoandikwa kwa kuzingatia imani potofu za kidemokrasia ya kisekula na mfumo wa Wakoloni makafiri wa Magharibi hasa Marekani-Uingereza, na kuweka mfano mwengine wa kuchukiza wa usaliti kwa Uislamu na Waislamu, na utiifu kwa nchi za Magharibi. Mfumo huu wa kisekula wa kibepari uliotungwa na wanadamu umefeli katika nchi zote duniani. Jambo hili ni la kweli mithili ya mwangaza wa mchana kwamba, mfumo huu wa ukandamizaji unalinda maslahi ya tabaka tawala, mabepari wachache na wakoloni wa Magharibi, na kuwanyonya watu wengi zaidi. Mnashuhudia kwamba kizazi cha vijana (Gen-Z) katika nchi nyingi wanaasi tabaka tawala la kibepari moja baada ya jengine na kuwaangusha watawala. Baada ya maasi ya Julai 2024, matabaka ya wanasiasa ya nchi hii wenye uchu wa madaraka, hawakujali matamanio ya watu kwa utawala wa Sharia, imani na hisia za Kiislamu, bali walijitenga na watu na kuwalazimisha kufunga ndoa chini ya uongozi wa Wamarekani na kutia saini kile kilichoitwa ‘Mkataba wa Julai’- suluhisho la kifisadi la kisiasa la kidemokrasia ya kisekula. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْمًا لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ]

Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini? [Surah Al-Ma'idah: 50]. Mbali na kubadili masaibu ya watu, suluhisho hili la kisiasa litahifadhi tu mwendelezo wa utawala dhalimu wa sasa. Matokeo yake wananchi hawana imani na sarakasi hizi za kisiasa za kidemokrasia na wananchi hawapendezwi na mambo haya.

Enyi Watu, lazima mlishuhudia kwamba Mapinduzi ya Kiarabu yalianza wimbi la mporomoko wa watawala dhalimu, lakini katika pazia la mageuzi ya serikali na masuluhisho mapya ya kisiasa yaliyoongozwa na Magharibi, mfumo wa kibepari ulioshindwa na mporomoko wa ubepari wa kisekula bado ungalipo. Kutokana na hali hiyo, masaibu ya watu katika nchi hizi hayajabadilika, bali udhibiti wa nchi za Magharibi umeongezeka. Katika nchi hii pia, munashuhudia jinsi Marekani-Uingereza wanavyojaribu kudhibiti siasa, uchumi na jeshi letu kupitia vibaraka wao. Zaidi ya yote, Mkataba huu wa Julai utawaunganishaje wananchi wakati haukuweza hata kuunganisha tabaka hili la vibaraka wa kisiasa?

Enyi Watu, lazima mjue jinsi suluhisho la kisiasa ‘Mkataba wa Madina’ ulivyoanzishwa kwa msingi wa imani ya Kiislamu ulivyoweka msingi wa dola ya Kiislamu mjini Madina. Chini ya dola ya Kiislamu, raia waliunganishwa chini ya utawala adilifu bila kujali dini na rangi na waliishi maisha yenye neema. Baadaye, Khilafah ilieneza utawala huu adilifu wa Uislamu duniani kote. Hata hivyo, mfumo wa kidemokrasia wa nchi za Magharibi umeeneza unyonyaji, ukandamizaji na vita duniani kote kwa muda mfupi sana. Kwa hiyo, ili kuregesha izza na adhama yetu, ni lazima tuitishe suluhisho ya kisiasa kwa kuzingatia Mkataba wa Madina na kuungana ili kusimamisha Khilafah.

Enyi Maafisa Wanyofu wa Jeshi, katika kipindi hiki cha kisiasa nchini, tunapenda kukumbusha juu ya Kiapo Tiifu (Bay’ah) cha Pili cha Aqabah, pale jeshi likiongozwa na Saad bin Mu’adh (ra) lilipompa Mtume (saw) nusrah (mamlaka) ya kusimamisha dola ya Kiislamu, yeye (ra) hakujali nguvu yoyote duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt). Ibn Is-haq amesema: قال ابن إسحاق لما اجتمع الأنصار لبيعة رسول الله ﷺ في العقبة الثانية، قال لهم العباس بن عبادة بن نضلة الأنصاري "يا معشر الخزرج، هل تدرون على ما تبايعون هذا الرجل؟ إنكم تبايعونه على حرب الأحمر والأسود من الناس. فإن كنتم ترون أنكم إذا نُهكت أموالكم وأشرافكم قتلاً أسلمتموه، فمن الآن، فهو والله خزي الدنيا والآخرة. وإن كنتم ترون أنكم وافون له بما دعوتموه إليه على نهكة الأموال وقتل الأشراف، فخذوه، فهو والله خير الدنيا والآخرة. فقالوا: إنا نأخذه على ذلك. فقالوا للنبي ﷺ: فما لنا على ذلك يا رسول الله إن نحن وفينا؟ “Walipokusanyika kwa ajili ya kiapo, Al-Abbas bin Ubadah bin Nadlah akasema: “Je, mnajua ni mapatano gani mnayoingia na mtu huyu, kwa hakika mnatangaza kwamba mtapigana na watu mbalimbali, ikiwa mnaogopa kwamba mali yenu itakuwa hatarini au maisha ya watukufu wenu yatakuwa hatarini, basi muachilieni hivi sasa, kwa sababu mkifanya hivi baada ya kiapo, itakuwa ni udhalilifu kwenu duniani na Akhera. Lakini ikiwa mwadhani mnaweza kutekeleza yale mnayoombwa kuyafanya licha ya upotevu wa uhai na mali, basi lipokeeni jukumu hili zito, na wallahi humo imo kheri ya dunia na Akhera.” Wakajibu, ‘Tayari tumezingatia upotevu wa mali zetu na kuuawa kwa vigogo wetu, lakini tunatangaza utiifu wetu kwake. Lakini itakuwaje malipo yetu ikiwa tutatekeleza masharti yote ya mapatano haya?’ Mtume (saw) akajibu, ‘Pepo ndio makaazi yenu.’ Wakasema, ‘Inua mkono wako,’ kisha akainua mkono wake na wakatangaza utiifu wao kwake. Basi unganeni na Hizb ut Tahrir katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume na toeni Nusrah (msaada wa kimada) kwa Hizb ut Tahrir bila ya kuogopa Amerika-Uingereza-India. Tunataka kukuhakikishieni kwamba Ummah wote wa Kiislamu, isipokuwa matabaka ya vibaraka wanaotawala, unangojea kudhihiri Khilafah, na uko pamoja nanyi. Zaidi ya hayo, iwapo vibaraka hao watatenganishwa, dola hizi kubwa hazitakuwa na njia ya kuingilia katika ardhi yetu, Insha’Allah.

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ ...]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao …” [An-Nur: 55].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.